Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, April 16, 2010

MAZISHI YA RAIS WA POLAND YAZUA MVUTANO!!!


Kaka wa Marehemu Jaroslaw Kaczynski akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lililobeba Mwili wa Rais wa Poland Lech Kaczynski.

Mvutano umeibuka juu ya uamuzi wa kumzika rais wa Poland Lech Kaczynski katika kanisa la Wawel mjini Krakow, sehemu iliyotengwa kwa ajili ya wafalme na mashujaa wa Poland.

Mamia ya watu wameandamana kwa katika mitaa ya mji wa kusini siku ya pili mfululizo wakipinga uamuzi huo, huku wengine kwa maelfu wamejiunga katika kampeni ya kwenye mtandao kupinga mpango huo.

Rais Kaczynsi alifariki katika ajali ya ndege jumamosi iliyopita pamoja na mkewe na maafisa wengine kadhaa wa serikali ya nchi hiyo.

Tarehe ya uchaguzi wa rais itapangwa na kutangazwa baada ya mazishi ya kiongozi huyo siku ya jumapili.

No comments:

Post a Comment