Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, April 8, 2010

Kapuya asema Wanaotaka ajiuzulu Hawajielewi!!


Wakati bado mizozano ya baadhi ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wanasiasa na watu mbalimbali yakiwa yanaendelea,Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Juma Kapuya, amesema wanaomtaka kujiuzulu hawana maana, hivyo amewataka kupeleka hoja zenye msingi wa sababu za kujiuzulu kwake, badala ya kumjadili.

“Ukimuona kiongozi wa wafanyakazi anasema hivyo, hajui kazi wala wajibu wake... hana maana, hajui dhamana aliyonayo. Wanatakiwa walete hoja mezani tuzungumze; matokeo ya hoja hizo yataamua kama nijiuzulu ama la na mimi niko tayari,” alisema Kapuya.

Profesa Kapuya alisema hayo Dsm jana kwenye ofisi ndogo za Bunge, alipokutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia Huduma za Jamii.

Kauli ya Kapuya, ilikuja muda mfupi baada ya kutakiwa kutoa tamko lake kuhusu ombi la chama kimoja cha wafanyakazi kilichounga mkono mgomo usio na mwisho unaotarajia kuanza Mei 5, kumtaka Rais Jakaya Kikwete kumfukuza kazi waziri huyo.

Kadhalika, aliendelea kupuuza kauli ya kumtaka ajiuzulu iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano nchini (TEWUTA), Junus Ndaro, kwa madai kwamba kiongozi huyo wa wafanyakazi, hajui wajibu wala dhamana aliyonayo.

Waziri Kapuya alihoji msingi wa wafanyakazi kumtaka ajiuzulu na kubainisha kwamba hawezi kufanya hivyo bila kuwepo kwa hoja za msingi kwa sababu, madai ya wafanyakazi hayawezi kuamuliwa na mtu mmoja.

No comments:

Post a Comment