Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, April 14, 2010

MARUFUKU KUPIGA MUZIKI RADIONI SOMALIA


Haya tena, huko Somalia stesheni za radio zimepigwa marufuku kurusha matangazo yanayoambatana na muziki. Amri hiyo iliyotolewa na waasi wa kundi la Hizbul-Islam, ambao ni waislamu wenye msimamo mkali, inaanza kufanya kazi mara moja.

Kinyume na utekelezaji wa amri hiyo, vituo na watangazaji wa radio watakuwa katika hatari ya kupoteza maisha yao. Mwandishi wa habari wa BBC aliyeko Mogadishu amesema amri hiyo inafanana sana na ile ya Taliban ya kule Afghanistan.

No comments:

Post a Comment