Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, April 14, 2010

Shoga taabani jela ya Malawi!


Mwanaharakati wa haki za binadamu wametoa wito wa kumpatia msaada wa haraka mwanaume mmoja anayehjihusisha na mapenzi ya jinsia, aliye gerezani nchini Malawi anayeelezewa kuumwa sana.

Mwanaharakati Peter Tatchell amesema amepokea taarifa kutoka gereza la Chichiri kwamba Steven Monjeza anayeendelea na kesi ya uhusiano wake wa kimapenzi na mwanaume mwenzake, hajatibiwa na amekuwa akitapika na kulalamika maumivu ya kifua kwa zaidi ya siku kumi.

Taarifa zaidi zimesema anazuiliwa katika jela yenye msongamano mkubwa na ni chafu.

Monjeza na mpenzi wake Tiwonge Chimbalanga, wanashtakiwa kwa kuikuka sheria iliyowekwa nchini Malawi inayopiga marufuku ndo za watu wa jinsia moja .

Wapenzi hao walifanya sherehe ya ndoa yao mwezi wa Desemba na wanakabiliwa na adhabu ya kifungo cha mika kumi na minne jela ikiwa watapatikana na hatia.

No comments:

Post a Comment