Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, April 10, 2010

LIYUMBA AFUTIWA SHITAKA


Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba aliyekuwa akikabiliwa na mashitaka mawili, kutumia vibaya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 221 leo ameondolewa shitaka la kutumia vibaya madaraka na hivyo kubaki na kosa moja.

Liyumba aliyekuwa akikabiliwa na kesi hiyo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, alifutiwa shitaka hilo baada ya mawakili wa upande wa utetezi kutoa vielelezo vilivyothibitisha kuwa mteja wao hakuwa na kesi ya kujibu.

Mshitakiwa huyo amerudishwa Keko mpaka Aprili 22 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.

No comments:

Post a Comment