Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, April 6, 2010

Chama cha waajiri chasema mgomo wa wafanyakazi nchi nzima ulioitishwa na TUCTA ni batili


Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waajiri nchini (ATE) Dk. Aggrey Mlimuka akitoa Tamko la la chama hicho kuhusu mgomo wa wafanyakazi ulioitishwa na Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA). Kushoto kwake ni Wakili Cornellius Kariwa - Makamu Mwenyekiti ATE na Cisse Mwirabi - Afisa habari Maelezo
Tamko lililotolewa na ATE linasema:
Notisi iliyotolewa ni ya mgomo usiohalali
kwa kuwa sababu za mgomo hazipo.

(a) Njia za majadiliano bado zipo wazi na wala majadiliano hayajafungwa wala kushindikana.
(b) Mgomo uliotangazwa hauna kipindi maalum kinyume na matakwa ya kisheria.
(c) Mgomo uliotangazwa unahusu sekta zote za uchumi wa nchi ikiwemo sekta binafsi ambayo ina taratibu zake za kuhakikisha na kulinda maslahi ya Wafanyakazi
(d) Mgomo huu utahusu pia sekta ya huduma muhimu kwa jamii (essential servises) ambazo haziruhusiwi kisheria kugoma.

Kwa kuwa mgomo huu si halali, waajiri watakaoathirika watakuwa na haki ya kuwachukulia hatua za kinidhamu wafanyakazi watakaoshiriki mgomo haramu ikiwemo kuwafukuza kazi, kutokuwalipa mishahara kwa kipindi cha mgomo na hata kuajiri wafanyakazi mmbadala.

Ijulikane kwa kwa wadau wote kwamba sheria zilizopo hazilindi Wafanyakazi wanaoshiriki mgomo haramu. Iwapo mgomo huu utatekelezwa waajiri watakaoathirika watakuwa na haki ya kudai fidia kwa hasara itakayosababishwa na mgomo huo dhidi ya TUCTA iliyoitisha mgomo usio halali.
Tunatoa rai kwa TUCTA na wadau wote waliohamasishwa na TUCTA, waachane na harakati za kuitisha mgomo usio halali na ambao utakuwa ni hasara kwa pande zote.

Tunaisihi TUCTA washiriki kwa dhati majadiliano yenye lengo la kuleta muafaka wa pamoja, kwa hili hakuna njia ya mkato. TUCTA itambue kwamba majadiliano baina ya wadau yanajenga hali ya kuaminiana na mahusiano mazuri endelevu.

Ikumbukwe kwamba, amani na utulivu sehemu ya kazi ni nguzo muhimu za kuongeza na kukuza uchumi na tija kazini, kuwepo kwa ajira endelevu na kupambana na umasikini. Vyama vya wafanyakazi ni wadau muhimu katika kuendeleza amani na utulivu mahali pa kazi.
Habari kamili
BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment