Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, April 24, 2010

Madini ya Vito Sasa Kuchimbwa na Wazalendo tu!!


Mswada wa Sheria ya Madini wa mwaka 2010 unaoendelea kujadiliwa Bungeni, umeweka kipengele kinachodhibiti uchimbaji wa madini ya vito kufanywa na Wantanzania peke yao.
Akichangia hoja hiyo miongoni mwa Wabunge wengine, Mbunge wa viti maalumu Bungeni kupitia CHADEMA Halima James Mdee, amesema madini hayo kama Tanzanite ya Mererani, safaya na mengine, hayahitaji nguvu ya teknolojia kubwa kutoka nje.

Amesema wenyeji wanaweza kutekeleza jukumu hilo hadi kuinua pato la Taifa iwapo watawezeshwa kwa kupelekewa viwanda, kuandaliwa soko na vifaa vingine pia kupewa miongozo na usimamizi thabiti.

Kadhalika sheria hiyo itatoa fursa ya ushirikiano baina ya wenyeji na wageni kutoka nje pale itakapobidi kwa makubaliano maalumu yatakayoridhiwa na pande zote mbili na kwa maslahi yanayotambulika kwa uwazi.

Aidha madini mengine kama Uranium, Copper, plutonium, mafuta na mengine yenye kuhitaji usimamizi mkubwa Serikali kutokana na umuhimu wake yatabakia kuwa chini ya uangalizi wa Serikali kama mdau mkuu na kupewa wawekezaji kwa mikataba ya wazi na Serikali.

No comments:

Post a Comment