Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, April 9, 2010

Wanasiasa wadatishwa na sifa za Wagombea


Wanasiasa wameendelea kupinga kipengele cha elimu katika Sheria ya Kanuni za Gharama za Uchaguzi, wasomi na wananchi wanaunga mkono kwa madai kuwa kitaleta mabadiliko katika masuala ya uamuzi na uchangiaji maendeleo ya nchi.

Kipengele hicho kilicho katika sheria hiyo, kinamtaka mgombea urais, udiwani na ubunge, kuweka bayana kiwango chake cha elimu.

Katiba inaeleza kuwa mgombea wa nafasi hiyo, sifa yake kielimu ni kujua kusoma na kuandika.

Wakizungumza na kwa nyakati tofauti, baadhi ya wenyeviti wa vyama vya siasa nchini, wameonesha wasiwasi wao juu ya kipengele hicho, huku wakidai kuwa elimu si kigezo cha kupata kiongozi bora.



Mwenyekiti wa Chama wa Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema katika uongozi, kinachohitajika ni kiongozi imara, mwadilifu na mwenye sifa ya uongozi na awe anajua kusoma na kuandika.

“Hii ndiyo demokrasia, lazima watu wakupime kwa uwezo wako, utendaji wako na uwajibikaji na si kielimu pekee, suala la kutaka viongozi wenye vyeti pekee ni kinyume na demokrasia yetu ingawa kweli elimu inasaidia,” alisema Profesa Lipumba.

Hata hivyo, alisema si lazima kiongozi awe na elimu kubwa ndipo aongoze kwa uaminifu, kwani wapo wenye uwezo mkubwa na sifa za uongozi bora, lakini kiwango chao cha elimu ni kidogo.

Mwenyekiti wa Chama cha Labour (TLP), Augustine Mrema, alikiri kuwa elimu inasaidia sana katika maisha ambapo mtu mwenye elimu, hata kiwango chake cha umakini ni kikubwa, lakini akaongeza kuwa muhimu wa elimu hiyo, si katika kila kitu hususani kwenye uongozi.

Alisema yeye Mrema haamini kama elimu ni suluhisho la matatizo ya uongozi nchini. “Mbona ukifuatilia wanaokula rushwa ni hao hao wasomi viongozi, wapo viongozi wasio na elimu kubwa kama akina Tony Blair (Waziri Mkuu wa zamani Uingereza), lakini waliongoza vizuri,” alisema.

No comments:

Post a Comment