Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, April 2, 2010

59 Wajitokeza Kumrithi Maximo

Makocha 59 Wameweza kujitokeza kutaka kurithi nafasi ya Kocha Marcio Maximo, ya kuinoa timu ya taifa ya soka 'Taifa Stars' na hayo yalisemwa na Shirikisho la soka Tanzania (TFF).Raisi wa TFF, Leodegar Tenga, alisema kuwa miongoni mwa maombi hayo 59 waliyopokea, makocha watatu ni wazalendo, na watatu wengine wanatoka nchi za Afrika ambazo ni Kenya, Cameroon na Ghana huku wengine wakitokea bara la Asia na wawili wakitokea Amerika ya Kusini.

Alisema kwamba makocha 48 waliobaki, wanatoka barani Ulaya na akaongeza kuwa wengi wao wana uzoefu na uwezo mkubwa wa kufundisha timu za taifa.

Mbali na hilo alisema walipokea ombi moja kutoka kwa kocha Mzalendo, ambaye aliomba nafasi ya kuwa kocha msaidizi lakini ombi lake limetolewa kwa sababu lengo ni kutafutwa kwa kocha mkuu.

Mpaka sasa mchakato wa kupitia maombi hayo na hatua waliyopo, ni kwamba baadhi wameandikiwa barua ya waombaji ya kutaka kufahamu sasa wanafanya nini.

Kwani wanahitaji walipwe kiasi gani cha mshahara, na muda gani ambao wanaweza kujiunga na Stars endapo watakuwa wamefikia makubaliano.

"Tumewaeleza kwamba watupe majibu kabla ya Aprili 15. Kwa ufupi tumefurahishwa na idadi kubwa ya maombi yaliyojitokeza safari hii ukilinganisha na ilivyokuwa huko nyuma, wakati ule tulipokea maombi 18 tu na kati ya hayo, 15 tuliwaomba kwa kuwabembeleza," alisema Tenga.

Aliongeza kwamba mchakato huo ni mgumu sana na wanaufanya kwa umakini ili waweze kupata kocha bora atakayeendeleza mafanikio yaliyopo hivi sasa.

Mbali na kuwa na sifa za ziada, shirikisho litatoa kipaumbele kwa kocha ambaye atakuwa na uzoefu wa kufundisha makocha wengine na mwenye cheti kinachotambulika kimataifa.

Alimalizia kwa kusema kwamba si vyema kutaja majina ya makocha walioomba, ili kulinda heshima na pia kuthamini maamuzi yao waliyoyafanya ya kuomba ajira hiyo.

No comments:

Post a Comment