Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, April 3, 2010

MADEREVA WAZEMBE WAONYWA KATIKA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU!!


DAR ES SALAAM IJUMAA APRILI 02, 2010.9(jana) Jeshi la Polisi nchini kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani kimewaonya vikali madereva wote watakaoendesha magari yao kwa uzembe na kusababishwa ajali kuwa watafutiwa leseni na kufikishwa mahakamani kwa kutumia sheria za SUMATRA.
Hayo yamebainishwa na Kamanda mpya wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamisna Msaidizi Mwandamizi (ACP) Mohammed Mpinga, wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam kubainisha mikakati walioiweka katika kupambana na ajali za barabarani hasa katika kipindi hiki cha siku kuu za pasaka.

Kamanda Mpinga amesema kuwa wakati wa siku zote hizi watu wengi watakua na pilikapilika za hapa na pale na wengine kutumia siku hiyo kwenda katika kumbi mbalimbali za burudani kwa ajili ya kunywa pombe na kulewa kupita kiasi.
Amesema kuwa Askari wote wa kikosi hicho hawatapunzika na watakuwa kazini kuhakikisha kuwa hakuna Dereva ama mtumiaji mwingine wa barabara atakayeendesha vunja taratibu na sheria za ulama barabarani na hata kusababisha ajali kwa uzembe ama kutokana na vitendo vya ulevi.
Kamanda Mpinga amewataka Madereva na watumiaji wengine wa barabara wakiwemo waendesha bajaji, pikipiki, baiskeli, maguta, mikokoteni na wale waendao kwa miguu, kujidhari na kujiepusha na vitendo vyovyote vitakavyopelekea ajali.
“Tunawataka pia Madereva wote wa mabasi yaendayo mikoani, na wale wanaofanya safari zao kati ya mkoa mmoja na mwingine, kuacha kabisa kwenda mwendo wa kasi ama kuendesha magari hayo wakiwa wamelewa ili kuepusha ajali”. Alisema Kamanda huyo mpya wa kikosi cha Usalama Barabarani nchini.
Kamanda Mpinga amewataka Makondakta na mawakala wa mabasi hayo, wasiruhusu basi kujaa kupita uwezo wake na kwamba yeyote atakayekaidi na kukiuka maagizo hayo atachukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine watakaoiga.
Aidha Kamanda Mpinga pia amewaomba abiria na wananchi kwa ujumla kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za siri na za haraka pale wanapoona ukiukwaji wa makusudi wa sheria na kanuni za usalama barabarani, kwani nia ya kila abiria ni kufika salama kule anakokwenda na sio kuishia njiani kwa kusababishiwa majeraha ama kufariki kutokana na ajali za barabarani.

Amesema Askari wa Kikosi cha Usalama barabarani kwa kushirikiana na makachero wa Polisi na wale wenye sale za kawaida, watatawanywa katika maeneo mbalimbali kuhakikisha kuwa ajali za barabarani hasa katika kipindi hiki cha mfululizo wa siku hizi za mapumziko zinakoma.

No comments:

Post a Comment