Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, April 4, 2010

Nakuja Kupora Benki, Niandalieni Pesa Zangu!!


Albert Bailey (pichani juu) ambaye wiki hii naye ameushangaza ulimwengu kwa alichowaza baada ya kupiga simu kwenye benki kuwapa taarifa kuwa atakuja kupora kiasi cha pesa hivyo wamuandalie pesa hizo kwa kuziweka kwenye mfuko (naamini ili kuharakisha uporaji). Na baada ya dakika kumi, alikuja "kuchukua pesa alizoweka miadi" lakini kwa bahati mbaya waliompokea sio wahudumu na pesa, bali akapokelewa na askari wakiwa na pingu. ALIWAZA NINI? Lakini wazo lake lilisaidia kurahisisha kazi kwa polisi, kupunguza makimbizano na hata kuokoa maisha (kama angefanya uporaji kwa kutumia silaha).

No comments:

Post a Comment