Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, March 22, 2010

ANISA, MBUNIFU ANAYEZIDI KUPAA LEVO ZA KIMATAIFA!Ndiye mtanzania wa kwanza kwa ubunifu ambaye ameweza kushiriki katika onesho kubwa la mitindo la New York Fashion Week ambaye February mwaka huu 2010, ameshiriki kwa kuonesha mavazi yake huko na kung'aa sambamba na wabunifu wakubwa akiwemo Deola Sagoe,BCBG Maxazria,Tommy Hilfiger,Calvin Klein,Venexiana na wengineo wengi

Namzungumzia mtanzania, Anisa Mpungwe (24), mkazi wa jijini Dar es Salaam, ambaye ameshinda tuzo ya mwanamitindo mpya wa Elle, katika hafla iliyofanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Septemba 15, 2009
Shindano hilo liliandaliwa na Kampuni ya Mitindo ya Elle ya Afrika Kusini ambayo hujishughulisha na maonyesho ya mitindo na urembo.
Anisa ambaye ni mtoto wa aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Ami Mpungwe. kuanzia mwaka 1994 hadi 1999, aliibuka kidedea baada ya kuchaguliwa katika wanamitimndo 100 walioshiriki katika shindano hilo kutoka nchi za Kusini mwa Afrika, ambapo baada ya mchujo walibaki washindi sita tu.
Kisha washindi hao sita waliweza kuchujwa tena ili kuweza kupata mshindi wa tuzo hiyo ya fahari ya mitindo ya Elle New, ambapo Anisa alitangazwa kuwa mshindi.

Kutokana na ushindi huo, Anisa amejinyakulia kitita cha dola 2000, ambazo ni sawa na zaidi ya sh milioni mbili za Kitanzania.
Zawadi nyingine aliyoipata Anisa katika shindano hilo ni pamoja na kuingia mkataba wa kubuni mitindo kwa ajili ya kampuni ya nguo ya Mr. Price ambapo nguo hizo zinapatikana kwenye nchi mbalimbali linapopatikana duka la kampuni hiyo.

Kwa upande wake Anisa alisema kuwa fedha alizozawadiwa atazielekeza katika kukuza kampuni yake ya uanamitindo aliyoifungua huko Afrika Kusini inayofahamika kwa jina la Loins Clothes & Ashes, ambayo itakua ikibuni mitindo na kuionyesha mavazi katika maonyesho mbalimbali hapa nchini.

No comments:

Post a Comment