Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, March 26, 2010

SHEKHE YAHAYA ATOA TAMKO!Sheikh Yahya Hussein, akiongea na wanahabari leo na kutabiri kuwa hakutakuwa na uchaguzi mkuu mwaka huu!

Waandishi wa habari,
Siku ya Jumatatu Tarehe 27/12/2009 niliitisha kikao kama hichi cha Waandishi wa Habari kuwapa utabiri wa mwaka wa 2010 na nilitabiri mambo mengi ambayo mengine mpaka leo bado yanazungumzwa kwa sababu aidha watu hawakunielewa au wengine hawakukubaliana na utabiri huo kwa maslahi yao.
Kuna wengine walifikiri nimewalenga wao, kuna wengine walisema nimetumwa niseme niliyoyasema, na kuna wengine watu binafsi na viongozi wa dini waliyakejeli maneno yangu kila mtu kwa sababu zake anazozijua yeye mwenyewe.

Kwanza napenda kuwafahamisha kwamba mimi ninapotoa utabiri wangu huwa simlengi mtu wala simtabirii mtu natoa utabiri kwa manufaa ya jamii kwa hiyo ni wajibu wa kila mtu aidha kukubali au kukataa haya ambayo niliyoyasema. Katika mkutano huo nilitabiri kutokea kifo cha kiongozi wa wa zamani wa kitaifa na baada ya siku chache alifariki Mhe Rashidi Mfaume Kawawa.
Nilitabiri atakayempinga Rais Jakaya Mrisho Kikwete ndani ya CCM kufa ghafla, kauli hiyo ilileta utata mkubwa lakini hilo bado lipo kwa sababu muda wake bado, na kwa ufafanuzi sikusema viongozi wa upinzani nilisema ndani ya CCM.
Nilitabiri upinzani ndani na nje ya CCM
Nilitabiri kutokea kwa serikali ya Serikali ya Mseto

Nilitabiri kwamba hali Hali ya uchumi Tanzania itaboreka

Nilitabiri kwamba Waziri Mkuu ajaye atatokea upinzani

Nilitabiri kwamba kutatokea Maandamano makubwa kupinga matokeo ya uchaguzi hasa katika uchaguziwa wabunge
Na Nilitabiri kwamba kutatokea Kutokea ajali nyingi kwa vyombo vya usafiri na vyombo vya angani
Katika hayo kuna mengi yameshatokea kimataifa na hapa nchini, na muda wake ukifika hayo niliyoyasema mtayaona.
Niliwaahidi kwamba kipindi hiki nitawaita tena ili kutoa tena utabiri kwa sababu mwaka wa kinyota unaanzia tarehe tarehe 21/ Machi kwa hivyo kinyota leo ni siku ya tano tangu mwaka wa kinyota kuanza.

Vile vile mnamo tarehe 15/1/2010 jua lilipatwa na hiyo kinyota ni ishara ya kwamba kuna mambo mengi ambayo sikuwaambia wakati ule yatatokea kwa kupatwa huko kwa jua Huu ni mwaka 2010 na mwaka huu unatawaliwa na nyota ya kumi ambayo ni nyota ya Mbuzi Nyota hii inasimamiwa na sayari ya Saturn au Zohal na inahusika na Mambo Mabaya, Kutenganisha wanandoa, vita, Kukusanya zana za vita, Kuvunjika mambo, kuvunjika Shughuli zozote, kufifia kwa mambo. kushamiri Fitina, na uvumi au mambo ya umbea, Kugombanisha watu, na kutokea magomvi kati ya viongozi wa kisiasa.

Kupatwa kwa jua tarehe 15/1/2010 kunaashiria vurugu , umwagikaji wa damu, harakati za kijeshi na kashfa za kipolisi , mabadiliko ya uongozi katika ngazi mbali mbali , uasi wa ghafla katika serikali katika nchi ambazo ambazo zilipitiwa na kupatwa kwa jua ,nchi za Chad, Somalia, Tanzania, Zanzibar ,Congo, Kenya, India, Sri Lanka, Bangladesh na Mayanmar, Vile vile kutokea vurugu za uchaguzi katika nchi hizo.watu kufanya maasi na matukio ya kigaidi kushambuliwa kwa vyombo vya usafiri, kupotea kwa maisha ya watu na mali

Vile vile kutatokea harusi za viongozi na mazishi ya kitaifa. Vifo vya watu maarufu, matatizo ya kifedha na uchumi, ukame, matetemeko ya ardhi, kulipuka kwa volcano na habari nyingi zitakuwa ni zile zinazihusiana na majanga ya kidunia.

Kutokana na hayo:-

Natabiri kwamba hakutakuwa na Uchaguzi Mkuu Mwaka huu


Natabiri kwamba Hakutakuwa na mpasuko ndani ya CCM

Natabiri Uchaguzi ujao robo tatu ya Wabunge wengi walioko madarakani wataanguka.

Natabiri Bunge lijalo litakuwa litakuwa na sura nyingi mpya na wanawake wataongezeka sana.

Natabiri Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume Kuongezewa Muda

Natabiri Nafasi ya urais Zanzibar itakuwa na ushindani mkubwa kuliko miaka mingine yoyote.


Sheikh Yahya Hussein
Mnajimu maarufu Afrika mashariki na kati
Alhamisi 25/3/2010

No comments:

Post a Comment