Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, March 11, 2010

Wasomi ovyooo: Ni wa Chuo Kikuu, wapiga picha chafu

Wasomi hao ambao wadau wa mtandao wa picha zisizozingatia maadili wamewaita kuwa ni watu wa ovyo, huku wawili kati yao wakitajwa kuwa ni wa mwaka wa tatu wakichukua shahada ya mawasiliano ya umma (mass communication).
Hata hivyo, haikuweza kufahamika sababu hasa ya wasomi hao kupiga picha hizo chafu, zinazowaonyesha wakiwa watupu, huku wakikaa katika staili tofauti (pozi).

Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, ambaye amedai kuwafahamu mabinti hao vema, mara baada ya picha zao hizo kuenea mtandaoni, uongozi wa chuo hicho, uliwaita na kuwahoji sababu ya kufanya upuuzi huo.

Haikuweza kufahamika mara moja kama wanafunzi hao wamechukuliwa hatua gani baada ya kuhojiwa na uongozi wa chuo.

Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa suala hilo limewakera sana viongozi wa juu wa chuo hicho, ambapo wamekuwa na vikao vya mara kwa mara kujaribu kufikiria nini cha kufanya.

Chanzo chetu cha habari kilisema kuwa taarifa za wasomi hao kupiga picha chafu tayari zimewafikia wazazi wa wasichana hao kupitia uongozi wa chuo pamoja na mtandao uliozianika.

Habari zaidi zinasema kuwa baba wa mmoja wa wasichana hao aliwahi kuwa mtu maarufu katika chama kimoja cha siasa nchini.

Aidha, mwingine anatajwa kuwa wazazi wake ni watu wa dini na ni wana taaluma ya udaktari.
Hata hivyo, meseji mbalimbali za kuwafariji zimetumwa kupitia mtandao huo, huku nyingine zikiwaponda kwa kitendo hicho kisichoendana na utamaduni wa Kitanzania.

Baadhi ya meseji zilisomeka kama ifuatavyo: “Dada yangu ninakukana hadharani, wewe si dada yangu tena, ndio upuuzi gani huo unauonyesha? Mama kafungua hii ‘site’, amelia sana alivyokuona, ni mimi kaka yako Deo,”

“Roho inasikitika sana dada, umetoka kwenye familia yenye nidhamu sana, Dk. Swai na Mama Swai ni watu wanaoheshika sana hapa Moshi, dada yako pia na familia nzima. Ni uchafu gani huo unafanya huko chuoni? Unashida gani mdogo wangu?”

“Deo usiumie sana, cha msingi ni kukaa na kuongea naye, naamini hayuko katika hali nzuri kwa sasa anahitaji kupewa tumaini jipya! Mimi nimeshafanya hivyo kwa kumtumia ujumbe katika email yake, nadhani atausoma na akiuzingatia utampa tumaini jipya katika maisha yake yaliyobadilishwa kwa kiasi kikubwa kupitia suala hili,”.

“Nafikiri… na mwenzio mtumie fursa hii kuyatupa mawe mliyoyakusanya kwa muda mrefu na kuanza kuokota dhahabu. Hawa ndio marafiki mliojijengea na mliotumia muda wenu na hata fedha kuwatunza.”

“Wanapoteza muda wao kukusema, zidi kusonga mbele. Jitahidi kwenye masomo yako na haya yatapita. Wanakuchukia, lakini tupo wachache tunaokupenda na tutaendelea kukupenda!,” ni baadhi ya meseji hizo mtandaoni.
Mwandishi wetu, jana Ijumaa, alimpigia simu mkuu wa chuo hicho, alipokea. Alipoambiwa kuwa anaongea na mwandishi wa habari alisema yuko kwenye kikao, kisha alikata simu.

Juhudi za kupata kauli ya uongozi wa chuo hicho zinaendelea na mara tukiwapata tutachapisha muendelezo wa habari hii.
Gazeti hili linalaani vikali vitendo vya akina dada kupiga picha za utupu. Mhariri

Wasomi ovyooo: Ni wa Chuo Kikuu, wapiga picha chafu
Kumradhi wasomaji wetu tumeshindwa kuweka picha ya tukio hili kwasababu za kimaadili kwani nichafu kupita maelezo!

No comments:

Post a Comment