Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, March 25, 2010

RISASI YAMKOSA JERRY MURO NA KUJERUHI MWINGINE!!


Habari ambazo gazeti hili ilizipata kutoka kwa chanzo chake cha kuaminika zilisema Jerry ambaye alikuwa mahakamani hapo katika kesi yake anayotuhimiwa kuomba rushwa na watuhimiwa wengine wawili, alinusurika kupigwa na kitu hicho kinachoaminika kuwa ni risasi na badala yake ikampata mtu aliyekuwa naye mahakamani hapo.

Mtu huyo alifahamika kwa jina la Dk. Paul Andrew ambaye ni mtaalamu wa tiba za binadamu na ilielezwa kuwa alikuwa amekuja mahakamani hapo kumsindikiza Jerry kwa maelezo kwamba ni ndugu yake.

“Sisi tunaamini aliyekusudiwa ni Jerry Muro kwa sababu Dk. Paul alikuja kwa bahati mbaya tu na hatufikirii kama waliorusha risasi walikuwa wakijua kuwa mtu huyo atakuja mahakamani lakini tunaamini waliofanya kitendo kile walijua kuwa Muro atakuwepo kortini na inawezekana walikuwa wakimngoja nje ndipo akapigwa mtu wake mguuni.” Kilisema chanzo hicho.

Habari zinasema, Dk. Paul baada ya kujeruhiwa akitokwa na damu nyingi, kitu kilichowashitua watu wengi walioshuhudia tukio hilo.

Mtoa habari huyo aliongeza kuwa walishuhudia gari moja dogo lenye ‘tinted’ ambalo hawakuweza kujua namba zake likitoka eneo hilo kwa kasi, kitu kilichowafanya waamini kwamba watu waliotenda kitendo hicho cha kurusha kitu kilichomjeruhi daktari huyo, walikuwa humo.

Chanzo hicho kilizidi kupasha kuwa baada ya watu, akiwemo Jerry kuona daktari huyo akivuja damu kupita kiasi mguuni huku akiwa ameanguka chini, waliamua kumkimbiza Hospitali ya Marie Stopes Mwenge ambako anafanyia kazi.
Habari zinasema alipofikishwa hospitalini hapo aliingizwa moja kwa moja chumba cha upasuaji ambako jeraha hilo lilishonwa.

Mwandishi wetu alimpigia Jerry ili kumuuliza kuhusu tukio la kurushiwa risasi iliyompata Dk. Paul lakini awali alikataa kusema chochote, hata hivyo, baada ya kubanwa sana akathibitisha kutokea tukio hilo.
“Ni kweli Dk. Paul nilikuwa naye mahakamani alinisindikiza na alijeruhiwa vibaya mguuni na watu wasiojulikana na akakimbizwa Hospitali ya Marie Stopes, lakini sitaeleza chochote zaidi ya hayo. Mtafuteni yeye awaelezee zaidi,” alisema Jerry.

Dk. Paul alipopigiwa simu alithibitisha kuumizwa mguuni na kitu anachoamini kuwa ni risasi na watu ambao hawajui.
Akisimulia mkasa huo, Dk. Paul alisema alikwenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumsindikiza Jerry anayekabiliwa na kesi ya kuomba rushwa na mara baada ya shauri kuahirishwa walitoka nje ya Mahakama.
“Tulitoka nje ya mahakama na nikiwa karibu na barabara ya lami gari moja lenye tinted rangi ya silver (fedha) lilipita kwa kasi na nikashitukia mlio wa chini pyuu, nikasikia mguu una ganzi na nilipoangalia nikakuta unavuja damu,” alisema Dk. Paul.

Alisema anaamini kitu hicho kilichomuumiza ni risasi kwa sababu kilitoboa hadi kiatu chake na kumjeruhi vibaya mguu wake, hali iliyosababisha avuje damu nyingi.
“Nilipata mshituko mkubwa ndipo ndugu na jamaa zangu wakanisaidia kunikimbiza Hospitali ya Marie Stopes ambako nilishonwa jeraha,” alisema Dk. Paul.

2 comments: