Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, March 13, 2010

DAAAAH ETI IRENE ATHAMINI FILAMU KULIKO NDOA YAKE!Inaweza ikawa kweli japo hatuna uhakika wowote juu ya minong’ono ambayo imezagaa kila kona ya jiji la Dar es Salaam kuwa, mkali wa muvi za Kibongo Irene Uwoya ameonekana kuithamini zaidi tasnia ya filamu kuliko ndoa yake...Minong’ono hiyo kutoka kwa wanazi wa filamu za Kibongo imesikika kitaani ikidai kuwa, tangu mwanadada huyo aolewe na msukuma kandanda la kulipwa nchini Cyprus, Hamad Ndikumana ‘Katauti’ ambaye ni raia wa Rwanda hajawahi kukaa naye angalu mwaka mmoja ndani ya ndoa yao kwani amekuwa na ziara za mara kwa mara hapa Bongo.

Msanii huyo aliyehamishia maskani yake Cyprus yupo nchini akiwa katika hatua za mwisho za kukamilisha kucheza muvi inayokwenda kwa jina la My Dreams akiwa pamoja na mastaa kibao walioshiriki katika filamu hiyo iliyoandaliwa na RJ Company chini ya mkurugenzi wake Vincent Kigosi ‘Ray’.

Juhudu za kumnasa mwanadada huyo ili ajibu hoja za msingi za minong’ono hiyo ziligonga mwamba baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila mafanikio huku swahiba zake wa karibu wakidai kuwa alikuwa katika shooting ya filamu hiyo.
NA inno lyimo!

No comments:

Post a Comment