Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, March 25, 2010

MAPYA YAIBUKA TENA NI KATI YA IRENE UWOYA NA KALALA...........


Baadhi ya wasomaji wetu wanasema wanashindwa kuamini kama kweli wawili hao wana uhusiano unaoweza kukaa kwenye vyombo vya habari ikizingatiwa kuwa, kila mmoja anawajibika mahali.

Utata unazidi pale inapobainika kuwa, Kalala Junior, licha ya kudaiwa ana ukaribu wa kimahaba na Irene, lakini ni mchumba wa mtu kwa asilimia mia moja huku Irene naye akiwa ameolewa kwa ndoa, tena ya kikristo, jambo linalozua ‘hatihati’ ya kuwepo kwa sintofahamu kutoka kwa pande za wenza wao.

“Hili jambo limejaa wasi wasi na shaka, hivi kweli watu wanaweza kuwajibika kwa wenza wao halafu ikaanikwa uhusiano mwingine kwenye vyombo vya habari kweli?” Alihoji msomaji wetu aliyepiga simu chumba cha habari cha gazeti hili.
Aliongeza kuwa, kinachoonekana ni kuwa, uhusiano wa wawili hao unakubalika kwa pande zote kwani hawajitokezi kila mmoja kusema kwa upande wake kuko vipi.

“Kama ingekuwa si kweli, wangechomoza kuweka wazi, lakini mbona kimya, labda wanakubaliana,” alisema msomaji huyo.

Aidha, aliendelea kuonesha wasiwasi wake kama kweli ndoa ya Irene yenye mwaka mmoja sasa inahema kwani aliko mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ (Cyprus) si mbali katika dunia ya sasa yenye utandawazi wa vyombo vya habari vya ‘kielektroniki’.

Katika mahojiano yake na gazeti hili Kalala, alipopigwa swali la hekima kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na Irene kuvujia magazetini, alikohoa kwanza, lakini mwisho wa yote alimjia juu Irene akidai mnyange huyo anataka kumvunjia penzi lake.

“Mimi nabisha, Irene sina uhusiano naye wa kimapenzi. Mimi nina mchumba wangu bwana, kama yeye (Irene) mji wake umemshinda huko (Cyprus), asiniharibie mji wangu hapa (Tanzania), Irene anataka kunivunjia penzi na mchumba wangu,” alikoroma Kalala.

Aliendelea kuweka wazi kuwa, mpaka sasa hajui skendo hiyo imechipukia mitaa gani, kwani hata yeye ameshtukia tu ipo kwenye ‘mapepa’.

Bado Irene amekuwa mgumu kupatikana kwenye simu yake ya mkononi ambapo inasemekana amebadili namba kutoka ile ya zamani (iliyozoeleka) na kujibanza kwenye namba mpya ambayo kila anayempa ‘wanaandikishiana’ kwanza kwa ahadi kuwa, naye hatampa mtu mwingine bila ridhaa yake.

No comments:

Post a Comment