Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, March 12, 2010

BALAA KUBWA LA PETROLI LANYEMELEA!!Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) imevinyima leseni zaidi ya nusu ya vituo vya kuuzia bidhaa ya petroli nchini na sasa sheria inaitaka kuvifungia ili visijihusishe na uuzaji wa bidhaa hiyo.

Iwapo Ewura watatekeleza sheria hiyo ya mwaka 2008, kuna hatari kubwa kwa nchi kukumbwa na uhaba wa bidhaa ya petroli jambo ambalo ni hatari kwa uchumi wa nchi, kwani wauzaji watakuwa wachache kuliko ilivyo sasa.

Habari zilizopatikana jana, zilisema hadi Februari mwaka huu jumla ya vituo 1,250 ambavyo vimetuma maombi ya kufanya biashara ya kuuza bidhaa hiyo ya petroli, ni 541 tu ndivyo vimepewa leseni baada ya kukidhi masharti hayo na vituo 709 vimenyimwa leseni.

Kati ya vituo vilivyotuma maombi, 1,031 vimeomba kuuza mafuta ya rejareja na kati ya hivyo, vilivyokidhi masharti ni 487 tu, hivyo zaidi ya nusu havikidhi masharti kisheria.

Bunge lilipitisha Sheria ya Petroli mwaka 2008 na Ewura ikatoa muda wa mwaka mmoja kuanzia Aprili mosi mwaka jana, baada ya sheria hiyo kuanza kutumika, kuwa vituo vya mafuta ndani ya muda huo viwe vimetimiza masharti yanayoelezwa kwenye sheria hiyo.

No comments:

Post a Comment