Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, March 16, 2010

POLISI WALA MZINGA USIKU WA MANANE


Gari la polisi likiwa limepinduka na kuingia kwenye mtaro katika barabara ya Kilwa mnamo majira ya saa nane usiku kuamkia leo.Mashuhuda wa ajajli hiyo walionena na mwandishi wetu walisema walishtushwa na mshindo mkubwa, baadhi yao walikimbia kuokoa maisha yao kwa kudhani mabomu mengine yamelipuka. Baada ya muda walirudi kucheki kilichotokea, si unajua wabongo hawapitwi!! Ndipo walipokuta kitu cha maafande kimezama mtaroni. Hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa. Chanzo cha ajali bado hakijafahamika! Mapolisi wetu wajitahidi kuwa makini zaidi, hapo wangekuwa wanamfukuza jambazi, ingekuwa imeshakula kwao!!!!!

No comments:

Post a Comment