Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, March 22, 2010

MABANGO YA ASKOFU KAKOBE YALA NGWARA!!
Mshkaji akiwa amejiokotea taa ya bure iliyokuwa ikimulika mabango hayo!

Mzimu wa Shirika la umeme nchini umeendelea kumwandama Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Bible Fellowship la Mwenge jijini Dar es Salaam, Zachary Kakobe baada ya mabango ya kanisa lake kuvunjwa, kupisha ujenzi wa njia ya umeme wa msongo mkubwa.

Kutokana na hali hiyo Askofu Kakobe atawajibika kuilipa serikali fidia ya ubomoaji huo, kwa kile kinachoelezwa kuwa alikaidi kuondoa mabango mbele ya kanisa hilo ili kuruhusu njia ya umeme kupita.

Wiki chache zilizopita, serikali ilipuuzia mbali malalamiko ya Kakobe ya kutaka njia hiyo ya msongo mkubwa wa umeme kupita mbele ya kanisa hilo.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mkoa wa Dar es Salaam, James Nyabakari alisema jana kwamba tayari wametoa baraka zote kwa Tanesco kufanya tathmini ya kuondoa mabango hayo ili Kanisa la Askofu Kakobe liwajibike kuzilipa.

Mafundi wa Tanesco jana walishuhudiwa wakiyaondoa mabango hayo mawili yenye urefu unakadiriwa kufikia futi 40 na upana futi 20 chini ya ulinzi wa polisi.

"Tutatoa agizo kwa Kakobe kulipa fedha hizo baada ya Tanesco kumaliza kazi na kuleta gharama walizotumia," alisema Nyabakari.

Awali baadhi ya waamini wa kanisa hilo walionyesha kutaka kutoa upinzani ili kuzuia zoezi hilo, lakini walishindwa baada ya kuona linasimamiwa na polisi.

Tanroads ilikuwa imetoa notisi ya siku saba kwa kanisa hilo kuyaondoa mabango hayo, tangu Machi 9, mwaka huu kwa sababu yalikuwa yamejengwa kwenye eneo la hifadhi ya barabara.

Nyabakari alisema kwamba hadi jana siku 20 zilikuwa zimepita na Askofu Kakobe alionekana kukaidi amri hiyo.

No comments:

Post a Comment