Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, March 29, 2010

Precision Air sasa yaenda Kusini


SHIRIKA la Ndege la Precision Air linakamilisha mchakato wa kuanza safari za kwenda kusini mwa Afrika baadaye mwaka huu.

Safari hizo zitaanza mara tu shirika hilo litakapokamilisha ununuzi wa ndege nyingine aina ya Boeing 737. Safari hizo zitaunga miji ya Johannesburg, Afrika Kusini na Lusaka, Harare.


Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Alphonce Kioko, wakati wa chakula cha usiku maalumu kwa ajili ya Mawakala wa Precision Air.

Pamoja na ununuzi wa ndege hiyo kubwa Precision Air pia ina mpango wa kununua ndege nyingine mpya tano aina ya ATR katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

"Tulianza na mpango wa kuboresha ndege zetu mwaka 2006 tulipoingia mkataba wa Dola za Marekani milioni 129 na ATR ya Ufaransa ili ituletee ndege mpya saba. Kati ya hizo ndege saba tayari tunazo tano, na mbili za mwisho zitaletwa mwezi Juni na Julai mwaka huu. Usafiri wetu utaweza kutegemewa zaidi, na tutazingatia zaidi muda, kadhalika wasafiri wataburudika sana kwa sababu ndege zetu mpya zina burudani ndani kwa safari fupi," alisema Kioko.

Pamoja na kuongeza idadi ya ndege, Kioko alisema kampuni yake ina mpango wa kuanzisha huduma ya SMS ili wateja wapate taarifa mbali mbali kuhusu safari za ndege kwa urahisi zaidi kupitia simu za mkononi.

Katika hafla hiyo, kampauni ya Uwakala wa Usafirishaji ya Bon Voyage Travels ndio waliotangaza washindi wakiongoza kwa mauzo ya tiketi za Precision Air na walipewa Tuzo.

No comments:

Post a Comment