Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, March 11, 2010

RUBANI AFARIKI NDEGE IKIWA HEWANI!!


Katika kisa ambacho wengi watadhani ni muujiza, abiria 247 waliokuwa wakisafiri na ndege ya kampuni ya Continental kutoka Ubelgiji hadi Marekani waliponea chupuchupu wakati nahodha wa ndege yao alipofariki dunia.
Msemaji wa Halmashauri inayosimamia usafiri wa ndege Marekani, Arlene Salac alisema kulikuwa na marubani wengine wawili ambao waliidhibiti ndege hiyo aina ya Boeing 777 hadi uwanja wa ndege wa Newark Liberty ambako ilitua kwa dharura. Abiria hawakuambiwa lolote kuhusu mkasa huo.
Miongoni mwa abiria wa ndege hiyo alikuwepo daktari mmoja wa maswala ya moyo, Dr. Julien Struyven ambaye aliitikia tangazo lililoomba daktari yeyote kwenye ndege hiyo kujitokeza.

Abiria hawakujua kwamba mwito ulitolewa kwa ajili ya kumuokoa rubani wa ndege hiyo.
Dr Struyven alipomfikia rubani huyo alikuta kama tayari ameaga dunia.
“Hakukuwa na uwezekano wowote wa kumwokoa,” alisema Dr Struyven.
Alisema huenda rubani huyo mwenye umri wa miaka 60 na ambaye amehudumia kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 20 alifariki dunia kutokana na matatizo ya moyo

No comments:

Post a Comment