Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, March 12, 2010

UNAMJUA BILIONEA MPYA WA DUNIA???


Pichani ni Carlos Slim Helu mwenye umri wa miaka 70 ambaye ni raia wa Mexico na ndiye mtu tajiri kuliko wote duniani kwa mwaka 2010 kutokana na matokeo ya mtandao wa Forbes.
Helu ambaye anaendesha biashara ya mambo ya mawasiliano ikiwamo simu amewapiku raia wa Marekani Bill Gates and Warren Buffett ambao wamekuwa wanatawala nafasi hiyo kwa miaka 14 iliyopita.

Utajiri wa Carlos Helu unakaribia kufikia kiwango cha dola za kimarekani bilioni 53.5 sawa na shs za Kitanzania 66,250,000,000,000 akiwa amemwacha Bill Gates katika nafasi ya 2 ambapo utajiri wake unafikia kiasi cha dola bilioni 53 na Buffet akiwa wa tatu.
Nafasi ya 4 na 5 zinashkiliwa na mabilionea wawili kutoka India Mukesh Ambani na Lakshmi Mittal.

Utajiri wa Helu unakadiriwa kuongezeka kwa kiasi cha dola bilioni 18.5 kwa miezi 12 tu iliyopita.

No comments:

Post a Comment