Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, March 23, 2010

Wizi kupitia mtandao watinga nchini


Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi Afande Abdallah Mssika

JESHI LA POLISI HALINA TAARIFA ZA KUIBWA KWA SHILINGI BILIONI 300 KUTOKA KATIKA MABENKI MBALIMBALI HAPA NCHINI

Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi nchini limesema halina taarifa za wizi wa shilingi Bilioni 300 zinazodaiwa kuibwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta kutoka katika mabenki mbalimbali yaliyounganishwa na mtandao huo hapa nchini.

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, amesema jana kuwa taarifa zilizoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na wizi huo hazijafikishwa Polisi.

Kamanda Mssika amesema kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Ma
kosa ya Jinai Kamishna Robert Manumba, aliyedaiwa kukaririwa na chombo hicho cha habari, amesema kuwa hana taarifa ya tukio la wizi wa shilingi Bilioni 300.

Kamishna Manumba amesema kuwa mawasiliano kati yake yeye na Mwandishi wa taarifa hiyo kwa upande wake binafsi yalihusu tukio la wizi wa fedha katika benki ya NMB Tawi la Bank House Jijini Dar es Salaam ambapo mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu, ambapo Jeshi la Polisi lilibaini kuibwa kwa shilingi milioni 360 kwa njia ya mtandao wa kompyuta fedha ambazo zilihamishiwa katika tawi moja wapo la benki hiyo lililopo mkoani Shinyanga.
Kamanda Mssika amefafanua kuwa, mara baada ya fedha hizo kufika Mkoani Shinyanga, zilitawanywa kutoka katika tawi hilo na kupelekwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta kwenda katika akaunti mbalimbali za watu binafsi kwenye matawi mengine ya benki hiyo katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Kutokana na wizi huo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Benki ya NMB limeshafanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 319 kati ya shilingi milioni 360 zilizoibwa na kwamba tayari baadhi ya watuhumiwa waliohusika katika wizi huo wakiwemo watumishi watano wa benki wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu shitaka lao.
Hata hivyo Kamanda Mssika amesema kutokana na taarifa za kuibwa kwa shilingi bilioni 300, kama ilivyoandikwa, ametoa wito kwa Makampuni ama Taasisi za Kifedha zinazoweza kuwa zimefanyiwa hujuma hiyo ya wizi na iwapo rasimu zao za ndani kiuchunguzi zimekamilika, basi wawasiliane na Mkurugenzi wa makosa ya Jinai nchini Kamishna Robert Manumba, ili hatua za uchunguzi ipasavyo kwa kuvishirikisha vyombo vya dola ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

No comments:

Post a Comment