Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, March 31, 2010

UWAZIRI PEMBENI! NIACHENI NILE RAHA!!!Waziri wa kazi, Ajira na maendeleo ya Vijana Mheshimiwa Profesa Juma Kapuya akiwa amevalia sare sawa na waimbaji wa bendi ya Akudo, alijitosa ukumbini na kuanza kuyarudi mapigo ya pekecha pekecha ya bendi ya Akudo Impact iliyokuwa ikitoa burudani kwenye ukumbi wa Msasani Beach. Kapuya ambaye ndiye mmliki wa bendi hiyo alijimwaga stejini na kusakata muziki kwa nguvu zote huku jasho likimtoka akiwa pamoja na mpambe wake ambaye jina lake halikufahamika. Kapuya anakuwa kiongozi wa pili wa juu serikalini kumiliki bendi wa kwanza alikuwa Waziri Mdhihiri Mdhihiri ambaye aliwahi kumiliki bendi ya Mchinga Sound ambayo baadaye ilivunjika. Kutokana na jinsi anavyoithamini bendi yake, waziri Kapuya amefanikiwa kuifanya bendi ya Akudo iwe miongoni mwa bendi zinazopendwa sana nchini kiasi cha kuleta ushindani mkubwa katika medani ya muziki wa dansi hapa nchini

1 comment:

  1. HIYO NI BENDI YAKE NA WANAWE ATHUMANI[A]KURWA[KU] DOTTO[DO] VIFUPI VYA MANENO VIMETUMIKA

    ReplyDelete