Habari mbalimbali toka pande za bongo bila kusahau matukio mbalimbali yanayorindima pande zote za dunia
Psquare Ft. J.Martins- E No Easy
Wednesday, March 31, 2010
SERIKALI YETU IKO WAPI!
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mateves iliyopo wilayani Arusha mkoani Arusha wakifanya mtihani wa majaribio wa nusu ya mwaka wakati wengine wakiwa wameketi chini kutokana na upungufu wa madarasa . Shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 910 ambao wanatumia madawati 320 tuuu katika madarasa hayo sasa hebu nambie upungufu uliopo. Piga picha hapo unambie wanasomaje hawa watoto wa A Town. Photo by Fredy Azzah
Tbl yaimwagia mashindano ya kili taifa cup mili 850
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Tanzania Breweriers Limited (TBL)David Minja akiongea mbele ya wanahabari leo wakati kampuni hiyo ilipotangaza udhamini wa jumla ya milioni 850 kwa ajili ya mashindano ya Kili Taifa Cup yanayotarajiwa kuanza mei 8 aprili mwaka huu.
Davidi Minja amesema vituo sita vitatumika katika mashindano hayo ambavyo ni Arusha, Mtwara, Tanga, Iringa, Mwanza na Dodoma, robo fainali za mashindano hayo zitafanyika kuanzania aprili 22 na fainali zitafanyika aprili 30 mwaka 2010.
Wengine wanaoonekana katika picha kushoto ni Ferdrick Mwakalebela Katibu mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF na kulia ni George Kavishe Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambayo ndiyo inadhamini mashindano hayo.
Khaaa!! Yule Mbwa aliyeibiwa si huyu hapa!!
Hapa ni mitaa ya Block 41 nyuma ya Best bite, kama unavyoona mbwa kabebwa na mshkaji. Hazijapita siku nyingi, mdau alitangaza kuibiwa mbwa wake mitaa ya sinza, mbwa mwenyewe ni huyu hapa. Mshkaji alikuwa anamuuza kwa sh elfu arobaini na tano.
Jamani mbwa kafundishwa kwa miaka kadhaa, halfu nasikia alikuwa mkali kupindukia lakini mshikaji akapita nae! Sasa kwa wale wenye mabull dog wanaouzwa sh millioni moja, kazi kwenu, wabongo hawachagui wala hawabagui. wabongo wameshindikana!!!
UWAZIRI PEMBENI! NIACHENI NILE RAHA!!!
Waziri wa kazi, Ajira na maendeleo ya Vijana Mheshimiwa Profesa Juma Kapuya akiwa amevalia sare sawa na waimbaji wa bendi ya Akudo, alijitosa ukumbini na kuanza kuyarudi mapigo ya pekecha pekecha ya bendi ya Akudo Impact iliyokuwa ikitoa burudani kwenye ukumbi wa Msasani Beach. Kapuya ambaye ndiye mmliki wa bendi hiyo alijimwaga stejini na kusakata muziki kwa nguvu zote huku jasho likimtoka akiwa pamoja na mpambe wake ambaye jina lake halikufahamika. Kapuya anakuwa kiongozi wa pili wa juu serikalini kumiliki bendi wa kwanza alikuwa Waziri Mdhihiri Mdhihiri ambaye aliwahi kumiliki bendi ya Mchinga Sound ambayo baadaye ilivunjika. Kutokana na jinsi anavyoithamini bendi yake, waziri Kapuya amefanikiwa kuifanya bendi ya Akudo iwe miongoni mwa bendi zinazopendwa sana nchini kiasi cha kuleta ushindani mkubwa katika medani ya muziki wa dansi hapa nchini
Tuesday, March 30, 2010
NAITWA JANE JOHN MFANYAKAZI WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI NCHINI TBC .NIMEFUNGUA BLOG AMBAYO ni janejohn5.blogspot.com hivyo nawakaribisha watanzania wote kuangalia ili mjionee mambo mbalimbali ya michezo,burudani na mengine mengi ambayo yatakuelimisha. pia unawezea kutuma maoni.
KARIBU picha na inno lyimo
KHAAA NI LAAANA AU MIUJIZA!
Kitu kikiwa kimeacha njia mchana wa leo hapa jijini dsm ikiwa ni siku chache tu baada ya lile lori lilipata ajali pale kibamba na kusababisha vifo vya watu kumi na moja!kwa ushauri wa bure tu madereva hata kama tunaamini magari yetu kwa kiasi kikubwa hatuna budi kufuata sheria za barabarani ili kuepukana na matatizo ya hapa na pale ikiwemo kusababisha ajali nk! picha na inno lyimo!
Mama salma kikwete ziarani mkoani mara
Mkurugenzi Mkuu wa Singita Grumeti Reserves Bwana Graham Ledger,kulia, akikabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete kwa ajili ya kazi za taasisi ya WAMA. Makabidhiano hayo yalifanyika katika hoteli ya Grumeti iliyoko katika hifadhi ya Serengeti .
HAROOO MWITA SIMAMAGAGA BWANAAAA!
Askari wa usalama barabarani kituo cha Migori Mtera katika wilaya ya Iringa vijijini aliyefahamika kwa jina moja ya Peter akiwa amekamata piki piki ambayo ilikuwa imevunja sheria za usalama barabarani kwa kupakizana zaidi ya abiria wawili huku wakiwa hawajavaa kofia ya kuzuia michubuko iwapo watapata ajali , madereva wengi wa piki piki katika eneo hilo wamekuwa wakiendesha bila leseni wala kuvaa kofia kwa madai kuwa chombo hicho ni mali yao haina haja na kuwa na leseni na kuwa wanaweza kupakizana idadi yoyote.Picha hii kwa hisani ya INNO LYIMO
Monday, March 29, 2010
Bingwa wa Hesabu afumbua swali lililoshindikana kwa miaka 50!
Mwanamahesabu mmoja mzaliwa wa Urusi, Grigori Parelman amefanikiwa kuchambua kila kona ya hesabu iliyoumiza vichwa wanasayansi kwa zaidi ya miaka hamsini. Genius huyo alitatua swali ambalo litawasaidia wanasayansi kujua umbo halisi la dunia.
Taasisi moja nchini Marekani inataka kumtuza kwa kiwango cha fedha ya thamani ya dola ya Marekani Milioni Moja ($1,000,000) sawa na pauni za Uingereza laki saba (£700,000) lakini mwenyewe amesema, "I'm not interested in money or fame".
Kukataa kwake si kuwa anadai dau kubwa bali ni kwa vile hataki hataki usumbufu wa kufuatwa fuatwa na kamera au kuandikwa ama kuwekwa kwenye kuta na mbao za matangazo kama sanamu, "I don't want to be on display like an animal in a zoo. I'm not a hero of mathematics. I'm not even that successful; that is why I don't want to have everybody looking at me." .
Mwanamahesabu huyo anaishi katika nyumba moja ya kupanga na mama yake na inasemekana nyumba yenyewe ina mende lakini mwenyewe anadai, "I have all I want".
Anaongeza kusema, "not very decent to look into other people's pockets and count other people's money".
20 Wanaswa Liberia Kwa Mauaji Ya Kishirikina!
Moja ya picha ikimwonyesha rais Ellen johnson sirleaf wa Liberia kushoto akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani na wakuu wa polisi Liberia.
Zaidi wa watu 20 wamekamatwa na polisi nchini Liberia, baada ya viungo vya mwili kupatikana katika makaazi ya afisa mmoja wa serikali.
Ripoti kutoka kusini mashariki mwa nchi hiyo zinasema, mama mmoja mjamzito aliuawa ili viungo vya mwili wake vitumike kwa matambiko. Afisa mmoja wa serikali katika mji mkuu wa Monrovia ameiambia BBC kuwa habari hizo ni za kushangaza na kuhuzunisha na kuwa uchunguzi umeanzishwa.
Waandishi wa Habari wanasema eneo hilo limekuwa na historia ya mauaji ya ushirikina. Viungo vya mwili vinatumika kutengeneza hirizi za kujaribu kuimarisha ushawishi na madaraka ya kisiasa
Precision Air sasa yaenda Kusini
SHIRIKA la Ndege la Precision Air linakamilisha mchakato wa kuanza safari za kwenda kusini mwa Afrika baadaye mwaka huu.
Safari hizo zitaanza mara tu shirika hilo litakapokamilisha ununuzi wa ndege nyingine aina ya Boeing 737. Safari hizo zitaunga miji ya Johannesburg, Afrika Kusini na Lusaka, Harare.
Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air pamoja na Mkurugenzi Mtendaji, Alphonce Kioko, wakati wa chakula cha usiku maalumu kwa ajili ya Mawakala wa Precision Air.
Pamoja na ununuzi wa ndege hiyo kubwa Precision Air pia ina mpango wa kununua ndege nyingine mpya tano aina ya ATR katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
"Tulianza na mpango wa kuboresha ndege zetu mwaka 2006 tulipoingia mkataba wa Dola za Marekani milioni 129 na ATR ya Ufaransa ili ituletee ndege mpya saba. Kati ya hizo ndege saba tayari tunazo tano, na mbili za mwisho zitaletwa mwezi Juni na Julai mwaka huu. Usafiri wetu utaweza kutegemewa zaidi, na tutazingatia zaidi muda, kadhalika wasafiri wataburudika sana kwa sababu ndege zetu mpya zina burudani ndani kwa safari fupi," alisema Kioko.
Pamoja na kuongeza idadi ya ndege, Kioko alisema kampuni yake ina mpango wa kuanzisha huduma ya SMS ili wateja wapate taarifa mbali mbali kuhusu safari za ndege kwa urahisi zaidi kupitia simu za mkononi.
Katika hafla hiyo, kampauni ya Uwakala wa Usafirishaji ya Bon Voyage Travels ndio waliotangaza washindi wakiongoza kwa mauzo ya tiketi za Precision Air na walipewa Tuzo.
Ngoma Inaposizi Katikati Ya Safari
Sunday, March 28, 2010
Ajali nyingine kama ya Kibamba yaua 2 Mbezi
SIKU moja baada ya ajali mbaya iliyohusisha lori lililolalia Hiace na kuua watu 11 katika eneo la Kibamba Darajani, wilayani Kinondoni, ajali nyingine imetokea juzi usiku katika eneo la Mbezi Mwisho ambapo lori liliacha njia na kugonga daladala na kisha kukanyaga watu wawili waliokufa papo hapo.
Watu wengine wanane walijeruhiwa vibaya wakiwemo abiria waliokuwa wakisubiri usafiri kuelekea Kibamba waliokuwa wamesimama pembeni mwa barabara, abiria waliokuwa wakishuka katika daladala iliyogongwa, waendesha pikipiki na wafanyabiashara ndogondogo waliokuwa pembezoni mwa barabara hiyo ya Morogoro, eneo la Mbezi Mwisho. Miongoni mwa watu waliojeruhiwa ni Neema Makundi, Mkazi wa Mbezi.
Mashuhuda wa ajali hiyo waliliambia gazeti hili katika eneo la tukio juzi usiku kuwa, dereva wa Lori aina ya Scania likiwa na trela lake ambalo lilikuwa likitokea Kibaha kwenda Ubungo, lilionekana kushindwa kushika breki kama umbali wa meta 20 hivi na kuacha njia.
“Wakati alipokuwa akijaribu kukwepa daladala iliyokuwa imejaa abiria hapa, alilivaa daladala hili lililokuwa linashusha abiria na hapa palikuwa na abiria wakisubiri usafiri, mwanamume mmoja na mwanamke mmoja wamekanyagwa vibaya na kufa papo hapo, ila wengine wamejeruhiwa na kuvunjika baadhi ya viungo vya mwili,” alisema Ali Abdu (Mboma).
Ajali hiyo ilitokea saa 3.30 usiku, na gazeti hili lilishuhudia mwanamke ambaye hakufahamika jina mara moja, akiondolewa chini ya lori hilo huku akilia na nguo zikiwa zimechanika na miguu yote miwili ikiwa imevunjika. Wasamaria walikodi teksi na kumkimbiza Hospitali ya Tumbi, Kibaha.
Makundi ambaye alisaidiwa na watu kutoka katikati ya watu waliokuwa wameangukia bondeni baada ya tafrani ya kila mmoja kujinusuru na ajali hiyo, huku akilia alisema kuwa haelewi kilichotokea kwani wakati anashuka kutoka katika daladala hiyo inayofanya safari kati ya Mbezi na Kariakoo, alisikia kishindo na kujikuta chini huku akiangukia bondeni.
Wafanyabiashara walionusurika na ambao hupanga bidhaa zao pembezoni kabisa mwa barabara kinyume cha sheria, waliamua kuchukua tochi na kuanza kutafuta mikoba yao ya pesa iliyopotea bila kujali wenzao waliokufa na kujeruhiwa vibaya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa katika ajali hiyo, mtu mmoja alikufa, abiria saba waliokuwa wakisubiri usafiri walijeruhiwa vibaya huku mmoja akiwa mahututi.
Alisema daladala hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Roggers Manka (35) mkazi wa Mbezi ambaye alieleza kuwa alikuwa akielekea Kiluvya ingawa basi lake liliandikwa Mbezi-Kariakoo.
Kenyela alisema maiti yupo Tumbi na majeruhi pia wamelazwa huko pia. Aliwataja waliojeruhiwa vibaya kuwa ni Agnes Semkwabi, mkazi wa Tandale, Jackline John (27) na Robert Mafuru wakazi wa Mbezi kwa Yusuf, Hamis Omari (22) mkazi wa Kiluvya, Angela Fredy (21) mkazi wa Msasani, Fua Ramadhani (23) mkazi wa Msasani na mwanamume anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 35 na 40 ambaye jina lake halikupatikana mara moja.

Polisi mbaroni kwa na dawa za kulevya
WAKATI Serikali kupitia vyombo vya Dola ikipambana na dawa za kulevya nchini na kutangaza kila mara watu inaowakamata kwa tuhuma za kuhusika na dawa hizo, polisi mwenye cheo cha Konstebo wa Dar es Salaam, ambaye anapaswa kuwa miongoni mwa wanaopiga vita biashara hiyo, amekamatwa na polisi wenziwe kwa msaada wa mgambo, akituhumiwa kuwa na shehena kubwa ya dawa za kulevya.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili juzi, zilibainisha kuwa askari huyo (jina na namba yake tunavyo), anayedaiwa pia kuwa mzoefu katika kushirikiana na majambazi na wauza dawa za kulevya, alikamatwa akiwa na dawa hizo ndani ya gari yake baada ya kufukuzwa na polisi wenzake kwa umbali wa zaidi ya kilometa saba.
Mtoa taarifa wetu alisema askari huyo anayefanya kazi katika Kituo cha Polisi Magomeni, Kitengo cha Upelelezi, alikamatwa juzi saa 10 jioni katika eneo la Kibamba, gari lake likiwa limebeba magunia nane ya mirungi na kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
“Hivi tunavyoongea anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay, alikamatwa na Kikosi cha Doria Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, alikuwa peke yake kwenye gari na dawa hizo za kulevya,” alisema mtoa taarifa wetu.
Kaimu Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Charles Kenyela aliithibitishia HabariLeo Jumapili kuwa askari Polisi huyo amekamatwa akiwa na raia mmoja na wote wanashikiliwa na Polisi.
Kenyela akielezea namna ilivyokuwa ngumu kumkamata polisi mwenzao huyo, alisema, “ni kweli alikuwa na raia mmoja, wamekamatwa na mirungi iliyokutwa kwenye buti garini mwake, iliteremshwa katika basi la abiria la Meridian linalofanya safari zake mikoa ya Kaskazini, na yeye aliipokelea Kiluvya lakini hakukamatiwa hapo.”
Kenyela alisema kulikuwa na tafrani kubwa kabla ya kukamatwa kwani baada ya kuiweka (mirungi) katika gari yake yenye namba za usajili T 287 ATL aina ya Toyota Cresta, alitaka kudhibitiwa na mgambo aliyekuwa akimhoji kitu alichobeba, lakini kwa mwendo wa kasi, alimtoka mgambo huyo jambo lililosababisha watu kupiga simu Polisi.
“Si unajua Polisi Jamii, askari wa doria walipopata taarifa, wakaanza kumfukuza, walimfukuza weee, umbali mrefu kutoka Kiluvya mpaka eneo la Msewe huko kwenye msitu wa bonde la Golani, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ndipo wakamkamatia hapo, baada ya kumshusha kwenye gari, walimtambua kuwa ni askari,” alisema Kenyela.
Alisema walipopekua gari, walikuta mirungi ikiwa katika viroba ambavyo vimefungwa kwa utaalamu wa hali ya juu na kama vingefunguliwa, vingejaa magunia tisa ya kawaida na kiroba kimoja.
Kenyela alisema bado hawajajua gharama ya mirungi hiyo na uzito wake na kwamba wanaendelea na upimaji huku raia na askari huyo wakiwa mahabusu.
Kaimu Kamanda huyo alisema watuhumiwa hao hawatatajwa majina kwa sasa kwa kuwa wamebaini kuwa wapo askari wengi zaidi wanaojihusisha na vitendo hivyo ambao upelelezi dhidi yao unaendelea kwa nia ya kuwanasa.
“Tutamshitaki kijeshi na endapo atabainika kuhusika na tukio hilo, atafikishwa mahakamani kama raia wa kawaida,” alisema Kenyela.
Naye Anna Makange, anaripoti kutoka Tanga kuwa, Polisi mkoani hapa inawashikilia vijana wawili kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 77.
Dawa hizo aina ya mirungi zilikamatwa Machi 25 mwaka huu saa 9 alasiri katika mtaa wa Kisosora, Kata ya Chumbageni wilayani Tanga.
Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Tanga (RCI), Jaffar Mohamed aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Victor Juma (26) na Kombo Bure (37) wote wakazi wa Kisosora.
Alisema watuhumiwa walikuwa wakisafirisha dawa hizo kwa njia ya pikipiki yenye namba T223 AYC aina ya Toyo iliyokuwa ikitokea mjini Mombasa katika nchi jirani ya Kenya kuletwa mjini hapa.
Matukio ya usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku nchini na kuharibu idadi kubwa ya vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Mohamed alisema kutokana na hali hiyo, serikali itahakikisha haitoi dhamana kwa mtu yeyote atakayekutwa akijihusisha na dawa za kulevya.

Saturday, March 27, 2010
Wanasiasa wampinga Shekhe Yahya
VIONGOZI wa vyama vya siasa nchini wameupuuza utabiri wa Mnajimu maarufu Afrika Mashariki, Shehe Yahya Hussein na kuitaka Serikali izipuuze ndoto hizo kwa kuhofia uchochezi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jana Dar es Salaam, baadhi ya viongozi wa vyama hivyo walikataa kutoa maoni yao kuhusu utabiri huo, ambao Shehe huyo alitabiri kutokuwapo kwa uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema hawezi kuzungumzia masuala yanayohusu unajimu kwa kuwa hayaamini na kwamba anachokiamini ni Katiba ya nchi na ratiba ya uchaguzi.
“Sina cha kusema juu ya mambo ya unajimu, ila naomba pia waulizwe wanajimu wengine na wapiga ramli, ili kujua na wao wana msimamo gani katika hili, ila kwa kweli mimi naiamini zaidi Katiba na ratiba niliyonayo ya uchaguzi,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema pamoja na hayo, ameshangazwa na ratiba ya uchaguzi ambayo inaonesha kuwa uchaguzi mkuu utafanyika Oktoba mwaka huu badala ya Desemba, kwa kuwa uchaguzi wa 2005 ulifanyika Desemba.
“Kwa mujibu wa Katiba Rais lazima akae madarakani kwa miaka mitano na ataapishwa mwingine kipindi kilekile alichoapishwa Rais aliyepita.”
Naye Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) Augustine Mrema, aliitaka Serikali isiupe nafasi utabiri huo, kwa kuwa una mwelekeo wa uchochezi na utaifanya nchi ionekane kama inaongozwa kwa utabiri.
“Mimi nasema Shehe Yahya asipewe nafasi na Serikali, kwani yenyewe haipaswi kuingia kwenye masuala ya imani, nchi hii ina waumini safi wa dini za Kiislamu na Kikristo, kwa hili asisikilizwe ili kuondokana na uchochezi wa ghasia,” alisema Mrema.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema kwa mujibu wa Katiba kila Mtanzania ana haki ya kuamini na kuabudu. “Serikali haina dini, lakini wananchi wana dini zao, SheheYahya ametumia nafasi ya Katiba kuzungumza anachoamini yeye, kwa hilo sina la kusema.”
Naye Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo, alisema hawezi kujiingiza katika mambo ya unajimu, hivyo asingependa hata kuuzungumzia.
Juzi alipozungumza na waandishi wa habari, Mnajimu huyo alitabiri kuwa kutokana na viashiria alivyoviona katika mwaka wa kinyota ulioanzia Machi 21 mwaka huu, hakutakuwa na uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.
Pia alikaririwa katika mkutano huo akisema: “Ninawahakikishia na kuwafahamisha kwamba mimi ninapotoa utabiri wangu huwa simlengi mtu wala simtabirii mtu, natoa utabiri kwa manufaa ya jamii, kwa hiyo ni wajibu wa kila mtu ama kukubali au kukataa haya ninayoyasema.”
Stars, Somalia vitani leo!!!
Kocha Wa Taifa Stars Marcio Maximo.
TIMU ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, leo inashuka katika Uwanja wa Uhuru kuwakaribisha Somalia katika mechi ya kampeni ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa nyota wa ligi za ndani-CHAN-zitakazopigwa mwakani nchini Sudan.
Ingawa mechi mbili baina yao ndizo zingeamua timu ya kusonga mbele, lakini kutokana na machafuko ya kisiasa nchini Somali, mechi ya leo ndiyo itaamua.
Akizungumzia mechi hiyo, Kocha Mkuu wa Stars, Marcio Maximo, alisema licha ya ubora wa wapinzani wao, vijana wake wamejipanga vizuri kushinda mechi.
Maximo alisema, ni muhimu kushinda mechi hiyo ya pekee na hasa ikizingatiwa kuwa Stars inacheza nyumbani ili kujiweka katika nafasi na mazingira ya kufanya vizuri katika mechi zitakazofuata.
“Kama ukianza vizuri katika mechi za mwanzo inakupa nguvu ya kufanya vizuri zaidi katika mechi nyingine, hivyo nina matumaini timu yangu itashinda mechi yetu hiyo iliyojaa ushindani mkubwa,” alisema Maximo.
Maximo amewasihi wapenzi, mashabiki na Watanzania kwa ujumla, kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo ili kuwapa wachezaji ari na nguvu ya kufanya vizuri.
Kwa upande mwingine, wadhamini wa Stars kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), jana ilikabidhi timu hiyo hundi ya sh milioni 50 ili kuwaongezea wachezaji hamasa.
Mshindi wa leo atacheza na Rwanda.
Akipokea hundi hiyo, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela, aliishukuru SBL kwa kuisaidia timu hiyo na kuomba makampuni na wadau wengine wazisaidie timu za taifa.
Mwakalebela alisema maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika na tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa leo kuanzia saa tatu asubuhi.
Viingilio vitakuwa shilingi 30,000 kwa viti maalu; 15,000 Jukwaa Kuu; 10,000 Jukwaa la kijani; na 3,000 mzunguko.
Somalia iliwasili juzi tayari kwa mchezo wa leo huku kocha wake Mohamed Abdulahi na nahodha wa timu hiyo, Yusuf Ali Nur, wametamba kuibuka na ushindi licha ya kukiri kuwa Stars ni wazuri.
MMILIKI WA LORI LILIOSABABISHA AJALI YA KIBAMBA ATIWA NGUVUNI MPAKA DEREVA APATIKANE!!!
Kamanda Msika akiongea na waandishi wa Habari.
Lori lililosababisha vifo vya watu 11, katika eneo la Kibamba jijini Dar es Salaam juzi amekamatwa, polisi wamemtaja mmiliki huyo kuwa ni Mahamoud Mohamed, na inasemekana amekuwa hatoi ushirikiano wa dhati ambao ungewezesha kukamawta kwa Dereva Kudra Adam, anayetuhumiwa kusababisha ajali hiyo. Kamanda wa kikosi cha Barabarani, Mo-hamed Mpinga, alisema; ‘Huyo jamaa tumemkamata leo, anakua anasitasita kutupatia ushirikiano ili tuweze kumpata dereva wa basi hilo,nachukua nafasi hii kuwahakikishia ni lazima tumkamate na hatutamuachia huyu mmiliki mpaka Dereva apatikane;alisema Kamanda Msika Jana.
Bw.Freeman Mbowe.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza vita dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Mtera, John Malecela na wabunge wenzake waliokaa bungeni kwa muda mrefu.
Vita hiyo ilitangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika mkutano wake wa Oparesheni Sangara uliofanyika wilayani Mpwapwa juzi.
Mbowe alisema kwa sasa umri wa Malecela kuendelea kuwa mbunge umekwisha na kwamba akisikia amechukua tena fomu kutetea nafasi hiyo mwaka huu atarusha helikopta katika kata zote za Jimbo hilo kuhakikisha anamng’oa.
“Mimi nazaliwa Malecela namsikia akiwa bungeni, nimesoma elimu ya msingi hadi sekondari, nimefanya kazi BoT, nimeacha kazi na sasa nafanya biashara, nimeingia kwenye siasa nimekwenda bungeni nimemkuta na nimemuacha, hivi huyu mtu amekuwa Sultani?,”alihoji Mbowe.
Alisema uwepo wa viongozi hao aliowaita masultani ndio unakokwamisha demokrasia nchini kwa kuwa hali hiyo ndiyo inayowajengea hofu wakazi wa Mkoa wa Dodoma.
Mbowe aliwataja wabunge wengine wa Mkoa wa Dodoma anaokamia kupambana nao mwaka huu kuwa ni Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje na Mbunge wa Jimbo la Bahi, William Kusilla.
Mbowe ambaye alisafiri jana kwenda Muleba kuhudhuria maziko ya Balozi Christopher Ngaiza ambaye ni alikuwa kada wa chama chake, alitoa wito kwa wakazi wa Mpwapwa na vitongoji vyake kuacha ushabiki wa vyama badala yake wachague viongozi bora na wenye sifa ya kuongoza.
Kwa mujibu wa Mbowe, utamaduni wa kushabikia vyama umepitwa na wakati kwani vyama vimeundwa na binadamu tofauti na ardhi na watu wake ambao wameumbwa na Mungu.
Kuhusu kukithiri kwa umasikini, Mbowe alisema kumetokana na mfumo wa mbovu wa serikali inayoundwa na CCM.
Alisema mfumo huo umekumbatia mafisadi na kuchana dhana ya mwaasisi wa taifa hili, Mwalimu Julius Nyerere aliyesema chama hicho ni cha wakulima na wafanyakazi.
Alisema Tanzania haina sababu ya kuwa maskini kwa kuwa ina kila aina ya rasilimali ikiwmao madini, mbuga za wanyama na ardhi yenye ruruba.
Kuhusu elimu alisema kuwa ujenzi wa madarasa katika kila kata umechangia kudidimiza elimu hapa nchini kufuatia shule hizo kuwa na upungufu mkubwa wa walimu na vitendea kazi.
Hata hivyo, Mbowe aliwashambulia baadhi ya wabunge wa CCM waliokuwa wakijinadi kuwa ni makamanda wa kupambana na ufisadi kuwa wameonyesha kutokuwa na uwezo wa kupambana na ufisadi.
“Hoja ya mapambano dhidi ya ufisadi iliasisiwa na Chadema, nyinyi ni mashahidi namna wabunge wa Chadema walivyopambana , mara wakajitokeza wenzetu kutoka CCM, kina John Malecela na wenzake na kujinadi ni wapambanaji wa ufisadi, lakini tulijua ngoma hii hawaiwezi na kwamba wangeishia njiani,”alisema.
Friday, March 26, 2010
SHEKHE YAHAYA ATOA TAMKO!
Sheikh Yahya Hussein, akiongea na wanahabari leo na kutabiri kuwa hakutakuwa na uchaguzi mkuu mwaka huu!
Waandishi wa habari,
Siku ya Jumatatu Tarehe 27/12/2009 niliitisha kikao kama hichi cha Waandishi wa Habari kuwapa utabiri wa mwaka wa 2010 na nilitabiri mambo mengi ambayo mengine mpaka leo bado yanazungumzwa kwa sababu aidha watu hawakunielewa au wengine hawakukubaliana na utabiri huo kwa maslahi yao.
Kuna wengine walifikiri nimewalenga wao, kuna wengine walisema nimetumwa niseme niliyoyasema, na kuna wengine watu binafsi na viongozi wa dini waliyakejeli maneno yangu kila mtu kwa sababu zake anazozijua yeye mwenyewe.
Kwanza napenda kuwafahamisha kwamba mimi ninapotoa utabiri wangu huwa simlengi mtu wala simtabirii mtu natoa utabiri kwa manufaa ya jamii kwa hiyo ni wajibu wa kila mtu aidha kukubali au kukataa haya ambayo niliyoyasema. Katika mkutano huo nilitabiri kutokea kifo cha kiongozi wa wa zamani wa kitaifa na baada ya siku chache alifariki Mhe Rashidi Mfaume Kawawa.
Nilitabiri atakayempinga Rais Jakaya Mrisho Kikwete ndani ya CCM kufa ghafla, kauli hiyo ilileta utata mkubwa lakini hilo bado lipo kwa sababu muda wake bado, na kwa ufafanuzi sikusema viongozi wa upinzani nilisema ndani ya CCM.
Nilitabiri upinzani ndani na nje ya CCM
Nilitabiri kutokea kwa serikali ya Serikali ya Mseto
Nilitabiri kwamba hali Hali ya uchumi Tanzania itaboreka
Nilitabiri kwamba Waziri Mkuu ajaye atatokea upinzani
Nilitabiri kwamba kutatokea Maandamano makubwa kupinga matokeo ya uchaguzi hasa katika uchaguziwa wabunge
Na Nilitabiri kwamba kutatokea Kutokea ajali nyingi kwa vyombo vya usafiri na vyombo vya angani
Katika hayo kuna mengi yameshatokea kimataifa na hapa nchini, na muda wake ukifika hayo niliyoyasema mtayaona.
Niliwaahidi kwamba kipindi hiki nitawaita tena ili kutoa tena utabiri kwa sababu mwaka wa kinyota unaanzia tarehe tarehe 21/ Machi kwa hivyo kinyota leo ni siku ya tano tangu mwaka wa kinyota kuanza.
Vile vile mnamo tarehe 15/1/2010 jua lilipatwa na hiyo kinyota ni ishara ya kwamba kuna mambo mengi ambayo sikuwaambia wakati ule yatatokea kwa kupatwa huko kwa jua Huu ni mwaka 2010 na mwaka huu unatawaliwa na nyota ya kumi ambayo ni nyota ya Mbuzi Nyota hii inasimamiwa na sayari ya Saturn au Zohal na inahusika na Mambo Mabaya, Kutenganisha wanandoa, vita, Kukusanya zana za vita, Kuvunjika mambo, kuvunjika Shughuli zozote, kufifia kwa mambo. kushamiri Fitina, na uvumi au mambo ya umbea, Kugombanisha watu, na kutokea magomvi kati ya viongozi wa kisiasa.
Kupatwa kwa jua tarehe 15/1/2010 kunaashiria vurugu , umwagikaji wa damu, harakati za kijeshi na kashfa za kipolisi , mabadiliko ya uongozi katika ngazi mbali mbali , uasi wa ghafla katika serikali katika nchi ambazo ambazo zilipitiwa na kupatwa kwa jua ,nchi za Chad, Somalia, Tanzania, Zanzibar ,Congo, Kenya, India, Sri Lanka, Bangladesh na Mayanmar, Vile vile kutokea vurugu za uchaguzi katika nchi hizo.watu kufanya maasi na matukio ya kigaidi kushambuliwa kwa vyombo vya usafiri, kupotea kwa maisha ya watu na mali
Vile vile kutatokea harusi za viongozi na mazishi ya kitaifa. Vifo vya watu maarufu, matatizo ya kifedha na uchumi, ukame, matetemeko ya ardhi, kulipuka kwa volcano na habari nyingi zitakuwa ni zile zinazihusiana na majanga ya kidunia.
Kutokana na hayo:-
Natabiri kwamba hakutakuwa na Uchaguzi Mkuu Mwaka huu
Natabiri kwamba Hakutakuwa na mpasuko ndani ya CCM
Natabiri Uchaguzi ujao robo tatu ya Wabunge wengi walioko madarakani wataanguka.
Natabiri Bunge lijalo litakuwa litakuwa na sura nyingi mpya na wanawake wataongezeka sana.
Natabiri Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume Kuongezewa Muda
Natabiri Nafasi ya urais Zanzibar itakuwa na ushindani mkubwa kuliko miaka mingine yoyote.
Sheikh Yahya Hussein
Mnajimu maarufu Afrika mashariki na kati
Alhamisi 25/3/2010
MREMA AMPELEKA SITA KORTINI!
MH Augustino mrema.
MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) Augustine Mrema, amemfungulia rasmi kesi ya madai Spika wa Bunge, Samuel Sitta na kumtaka amlipe fidia ya Sh bilioni moja kwa kumkashifu na kumdhalilisha kwa makusudi.
Mrema alisema jana Dar es Salaam kuwa kesi hiyo namba 32, aliifungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania na bado haijapangiwa Jaji wa kuisikiliza wala tarehe ambapo pamoja na Spika, pia Mhariri wa Mwananchi na kampuni ya Mwananchi Communications nao wamejumuishwa.
“Nimeamua kufanya hivi ili nirudishe heshima yangu ambayo nimeifanyia kazi kwa miaka 10 nikiwa waziri na kiongozi serikalini, lakini sasa nimetukanwa na kushushiwa hadhi kuwa eti ‘nimefulia’,” alisema Mrema.
Alisema Sitta katika gazeti la Mwananchi toleo namba 03548 la Machi 5 mwaka huu, alikaririwa akimwelezea Mwenyekiti huyo kuwa amekwisha kisiasa na kifedha na sasa anahangaika kujinasua katika hali hiyo.
“Katika gazeti hilo, Spika Sitta amediriki hata kunituhumu kuwa napata fedha ili kuipigia debe CCM, hali ambayo inaashiria kuwa nakula rushwa … siku hizi nikisikia hodi mlangoni napatwa na hofu nikifikiri ni polisi wanakuja kunikamata, maana Sitta ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM amesema nakula rushwa,” alisema.
Alisema kauli hiyo ya Spika kwa mujibu wa gazeti hilo, aliitoa alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu madai ya Mrema kwenye mkutano wake na waandishi wa habari Machi 4 mwaka huu, kuwa Sitta amekiuka maadili ya uongozi akiwa Spika wa Bunge, kwa kuendeleza mjadala wa kashfa ya Richmond na kushiriki ziara na baadhi ya wabunge wanaojipambanua kuwa ni wapambanaji wa ufisadi.
Akizungumzia madai hayo gazeti hilo lilimkariri Sitta akisema, “Mrema ni mhuni na amepitwa na wakati … pia amefilisika kisiasa na kifedha, sasa anatafuta njia ya kujinasua kutoka hali hiyo,” Mrema alilikariri gazeti hilo.
Mrema alisema kauli ya Sitta imemchafua mbele ya Watanzania ambao sasa wanamwona ‘amefulia’ na kwa watu ambao walikuwa wanamwamini na kumheshimu, sasa wamepoteza imani naye.
“Yaani mimi ‘nimefulia’ mnajua maana ya kufulia, ni mtu aliyekosa hata hela ya kula, mimi Mrema ninaongoza TLP ambayo katika uchaguzi wa serikali za mitaa imeshika nafasi ya nne kati ya vyama 18 vilivyopo, sasa nimefilisika vipi kisiasa, hii ni kashfa na matusi,” alisema.
Alisema Spika ni kiongozi wa chombo muhimu kinachowakilisha wananchi na kauli aliyoitoa kuhusu Sitta kuwa amekiuka maadili, ni ushauri, kwa kuwa akiwa kiongozi wa chombo hicho, hapaswi kuwa na makundi au kuegemea upande, hali ambayo itakuwa ni vigumu kwake kutoa uamuzi wa haki.
“Nimeifungua kesi hii kwa kuwa hata baada ya gazeti la Mwananchi kutoa taarifa hiyo, nilimwandikia barua ya kuniomba radhi na kunipa fedha ya kifuta jasho lakini amenidharau, kibaya zaidi kwa kauli yake hiyo, muda wowote naweza kukamatwa, sasa nataka anilipe Sh bilioni moja; yeye ni Spika hiyo ni fedha kidogo kwake,” alisema.
Alisema amehuzunishwa na kauli ya Spika kuwa amekuwa akiipigia debe CCM. “Kwa uwezo gani nilionao mimi Mrema na kwa nini anisingizie, CCM imeshinda uchaguzi tangu mwaka 2000 na 2005 bila msaada wangu.”
Mrema alisema anachojua yeye ni kwamba Spika Sitta anafahamu anataka kugombea jimbo la Vunjo, hivyo ili kumsaidia rafiki yake ambaye ndiye mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Aloyce Kimaro, aliamua kumchafua.
Alisema kwa kashfa ya ‘kufulia’ si kweli na ushahidi anao, kwani kwa mujibu wa taarifa ya akaunti yake katika benki ya NMB, ana akiba ya Sh milioni 37. “Mimi ni milionea, kuliko hata Waziri Mkuu wangu Mizengo Pinda ambaye ana Sh milioni 25 benki,” alisema Mrema.
Sitta naye alikaririwa kutaka kumfungulia kesi ya madai Mrema na kumtaka athibitishe matamshi yake ya kwamba alishirikiana na wabunge wanaojipambanua kama makamanda wa vita dhidi ya ufisadi na wafadhili wao kufanya ziara mikoani.
chanzo habari leo!
Breki chanzo cha ajali ya Kibamba
UKOSEFU wa breki umeelezwa kuwa ndicho chanzo cha ajali ya lori na daladala iliyosababisha vifo vya watu 11 katika eneo la Kibamba, nje kidogo ya Dar es Salaam jana.
Hadi jana maiti watano kati ya 11 waliokufa katika ajali hiyo, walikuwa wametambuliwa akiwamo mjamzito na kondakta wa daladala. HabariLeo ilishuhudia kazi ya uopoaji maiti katika ajali hiyo iliyohusisha daladala Toyota Hiace namba T 615 AJW ikitoka Kibamba kwenda Ubungo na lori la mafuta aina ya IVECO Fiat namba T 189 ABP na tela lake namba T192 ABP.
Abiria wote wa daladala walikufa papo hapo baada ya kugongwa na lori hilo na kutumbukia mtaroni na kulaliwa.
Lori inadaiwa lilikuwa na shehena ya lita 30,000 za mafuta ya taa. Lori hilo linalomilikiwa na Mohamed Mahmoud lilikuwa likiendeshwa na Kudra Adam (30) ambaye alikimbia baada ya ajali.
Hiace inamilikiwa na Seleman Khalfan Rajab. Mamia ya wakazi wa Kibaha walifika eneo la tukio kwa ajili ya kutambua ndugu zao huku baadhi wakidai kuwa ajali hiyo ilitokea saa 11 alfajiri kulingana na muda ambao ndugu zao waliondoka majumbani kuwahi shughuli zao.
Miongoni mwa waliotambuliwa ni Shukuru Hussein (27) aliyetambuliwa na baba yake mzazi, Hussein Saleh, ambaye alisema mwanawe alikuwa kondakta wa daladala lingine, na alikuwa anawahi kufuata gari lake Mbezi.
Mwingine ni Faraj Ismail Ngalamba aliyekuwa kondakta wa daladala lililopata ajali ambaye alitambuliwa na kaka yake, aliyedai kuwa asubuhi ile alimpigia simu lakini hakumpata.
Maiti mwingine aliyetambuliwa ni Abdultwaibu Twalib aliyetambuliwa na mkewe, Shani Mustafa ambaye alidai kuwa mumewe alikuwa akiwahi kazini bandarini Dar es Salaam.
Aliyetambuliwa mwingine ni Ester Paulo, aliyekuwa mjamzito na alitambuliwa na ndugu zake baada ya mwili wake kuvutwa huku tumbo likiwa limepasuka; na Zainabu Ali. Maiti wote wanasadikiwa kuwa wa Kibamba kutokana na daladala hilo kuanzia safari yake Kibamba njia panda.
Hata hivyo, kazi ya uopoaji ilionekana kuwa ngumu na kuchukua zaidi ya saa sita tangu ajali itokee kutokana na askari Polisi na kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, kufika eneo la tukio lakini bila vifaa madhubuti vya kuopolea miili hiyo.
Sambamba na uopoaji maiti, wananchi wengine mawazo yao yalielekea katika jinsi ya kujichukulia mafuta ya taa huku wakionekana na ndoo kwa ajili hiyo. Baada ya saa tano kupita, lilipofika gari la kuvuta magari mabovu aina ya Effco Crane kutoka kampuni ya BMK lililokodiwa kutoka Oysterbay likijikongoja polepole na baada ya kufika, lilisababisha barabara ya Morogoro kufungwa kwa zaidi ya saa mbili kupisha kazi ya kutenganisha magari hayo.
Tukio hilo lilivuta watu wengi wakiwamo wasafiri waliokuwa wakipita eneo hilo, ambapo kijana aliyejulikana kwa jina la Sijali alijikuta akiangua kilio kilichowashtua mashuhuda hao, baada ya kumtambua mama yake kupitia kiatu chake.
Askari walimsaidia kumpeleka katika gari lenye miili ili kumtambua mama yake zaidi, na alikiri kuwa ni yeye na kuendelea kulia. Inadaiwa mama huyo hakuwa na muda mrefu tangu ahamie Kibamba.
Baada ya kazi hiyo, maiti wawili waliotolewa mapema walipelekwa katika hospitali ya Tumbi, Kibaha na wengine hospitali za Mwananyamala na Muhimbili.
Akizungumzia ajali hiyo, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga, alithibitisha kuwa lori lilikuwa na lita 30,000 za mafuta ya taa na inadaiwa lilikosa breki na kulipamia daladala na kuliburuza meta kadhaa mtaroni na kulilalia.
Alisema maiti wanane waliopolewa na vipande vya mikono na viwiliwili ingawa inawezekana kuwapo zaidi, lakini hakuna aliyenusurika. Hata hivyo, alisema ipo haja ya barabara ya Morogoro hasa eneo hilo kufanyiwa marekebisho, kutokana na kuwa tishio kwa ajali.
Alikiri kuwa tatizo kubwa linalolikabili Jeshi la Polisi ni kukosa vifaa vya uokoaji kutokana na kwamba tangu walipopata taarifa, yalifika magari matatu ya kuvuta magari mabovu lakini yote yalikuwa hayana uwezo wa kulivuta lori hilo.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Mutani Suleiman, alisema alipokea maiti watano kati ya tisa ambapo wanne walipelekwa Muhimbili.
Wakati huo huo, kwa niaba ya uongozi wa Chadema mkoa wa Kinondoni Kanda Maalumu ya Dar es Salaam; Mwenyekiti wa Chama hicho katika kanda hiyo, John Mnyika, ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa wafiwa wa ajali hiyo.
Pia ametoa mwito kwa Serikali na vyombo vya Dola, kufanya uchunguzi wa kina kuhusu vyanzo vya ajali za mara kwa mara katika eneo la Kibamba, ambazo zimekuwa zikisababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.
“Ikumbukwe, kuwa Desemba 2007 ajali nyingine ilitokea Kibamba Hospitali, ikihusisha malori na kusababisha vifo vya watu saba akiwamo mjamzito na wengine 11 kujeruhiwa,” alisema Mnyika.
Aprili mwaka juzi, alisema jumla ya watu 181 walipoteza maisha kwa kugongwa na magari kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2007 katika eneo kuanzia Kibamba hadi Ubungo kwenye mataa.
“Mei mwaka jana, madereva wawili walikufa baada ya magari yao kugongana uso kwa uso maeneo hayo ya Kibamba … Januari mwaka huu, watu 18 walijeruhiwa katika ajali ya gari Kibamba Darajani ambapo magari matano yaligongana kwa wakati mmoja,” alisema.
chanzo habari leo

Thursday, March 25, 2010
JAMANI JAMANI JAMANI..................................
MAPYA YAIBUKA TENA NI KATI YA IRENE UWOYA NA KALALA...........
Baadhi ya wasomaji wetu wanasema wanashindwa kuamini kama kweli wawili hao wana uhusiano unaoweza kukaa kwenye vyombo vya habari ikizingatiwa kuwa, kila mmoja anawajibika mahali.
Utata unazidi pale inapobainika kuwa, Kalala Junior, licha ya kudaiwa ana ukaribu wa kimahaba na Irene, lakini ni mchumba wa mtu kwa asilimia mia moja huku Irene naye akiwa ameolewa kwa ndoa, tena ya kikristo, jambo linalozua ‘hatihati’ ya kuwepo kwa sintofahamu kutoka kwa pande za wenza wao.
“Hili jambo limejaa wasi wasi na shaka, hivi kweli watu wanaweza kuwajibika kwa wenza wao halafu ikaanikwa uhusiano mwingine kwenye vyombo vya habari kweli?” Alihoji msomaji wetu aliyepiga simu chumba cha habari cha gazeti hili.
Aliongeza kuwa, kinachoonekana ni kuwa, uhusiano wa wawili hao unakubalika kwa pande zote kwani hawajitokezi kila mmoja kusema kwa upande wake kuko vipi.
“Kama ingekuwa si kweli, wangechomoza kuweka wazi, lakini mbona kimya, labda wanakubaliana,” alisema msomaji huyo.
Aidha, aliendelea kuonesha wasiwasi wake kama kweli ndoa ya Irene yenye mwaka mmoja sasa inahema kwani aliko mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ (Cyprus) si mbali katika dunia ya sasa yenye utandawazi wa vyombo vya habari vya ‘kielektroniki’.
Katika mahojiano yake na gazeti hili Kalala, alipopigwa swali la hekima kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na Irene kuvujia magazetini, alikohoa kwanza, lakini mwisho wa yote alimjia juu Irene akidai mnyange huyo anataka kumvunjia penzi lake.
“Mimi nabisha, Irene sina uhusiano naye wa kimapenzi. Mimi nina mchumba wangu bwana, kama yeye (Irene) mji wake umemshinda huko (Cyprus), asiniharibie mji wangu hapa (Tanzania), Irene anataka kunivunjia penzi na mchumba wangu,” alikoroma Kalala.
Aliendelea kuweka wazi kuwa, mpaka sasa hajui skendo hiyo imechipukia mitaa gani, kwani hata yeye ameshtukia tu ipo kwenye ‘mapepa’.
Bado Irene amekuwa mgumu kupatikana kwenye simu yake ya mkononi ambapo inasemekana amebadili namba kutoka ile ya zamani (iliyozoeleka) na kujibanza kwenye namba mpya ambayo kila anayempa ‘wanaandikishiana’ kwanza kwa ahadi kuwa, naye hatampa mtu mwingine bila ridhaa yake.
BREAKING NEWZZZZZZ!
LEO MAJIRA YA ASUBUHI HUKO KIBAMBA DARAJANI KUMETOKEA AJALI MBAYA, ILIYOHUSISHA LORI LA MAFUTA NA BASI LA ABIRIA (DALADALA) NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU KADHAA. AJALI HIYO IMETOKEA BAADA YA LORI LA MAFUTA KULIANGUKIA GARI LA ABIRIA LILILOKADIRIWA KUWA NA WATU 25! MPAKA MUDA HUU WAOKOAJI WANAENDELEA KUTOA MIILI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI HIYO! TAARIFA ZAIDI PAMOJA NA PICHA ZA ENEO LA TUKIO ZITAWAJIA MUDA MFUPI!
Serikali yakiri hoja ya Dk. Slaa nzito
SIKU moja baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kudai Rais Jakaya Kikwete amepotoshwa kuhusu sheria ya gharama za uchaguzi, serikali imesema itaomba radhi na kurejesha muswada huo bungeni...Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema:
“Kama kweli ikithibitika, tuko tayari kuomba msamaha na kurudisha bungeni suala hili ili lifanyiwe marekebisho… namhakikishia Dk. Slaa kuwa tutarudisha bungeni ili makosa hayo yaondolewe.
“Siamini na si dhani kama ni kweli, kwa sababu eneo hilo nakumbuka lilijadiliwa kwa kina mno, tena Dk. Slaa na John Cheyo (Mbunge wa Bariadi Mashariki) walitoa mchango mzuri uliozua mjadala mrefu na hatimaye tukafikia mwafaka.”
Dk. Slaa alidai Rais Kikwete amepotoshwa katika baadhi ya vipengele, kikiwamo kipengele kinachohusu uthitibishwaji wa wajumbe wanaounda timu za kampeni kwa ajili ya wagombea urais, wabunge na udiwani.
Alisema Bunge halikukubaliana kuhusu kipengele hicho, wala hakimo katika kumbukumbu za Bunge; na kwamba kiliongezwa baadaye, kabla ya Rais Kikwete kusaini muswada huo kuwa sheria.
Hata hivyo, Jaji Werema alishtushwa na kauli ya Dk. Slaa, na kudokeza kwamba inawezekana hata mwanasiasa huyo hakukielewa vema kipengele hicho.
“Nimeshutushwa na kauli ya Dk. Slaa… wasaidizi wangu wameniambia haya mambo, saa sijui tatizo liko wapi… nafikiri anapaswa kuelimishwa tu.
“Tunajua sasa zipo kampeni, hivyo kila mtu anataka kufanya au kufuatilia kwa makini sheria hii, sasa namshauri Dk. Slaa aisome kwa makini,” alisema Jaji Werema.
Alisema kumbukumbu zinaonyesha kuwa wakati wa kujadili muswada huo kila kipengele kilipitiwa kwa umakini wa hali ya juu na kuridhiwa na wabunge.
“Nakumbuka katika kumbukumbu zangu wakati tunajadili muswada huu tulipitia kipengele kwa kipengele; sasa haya mengine yatakuwa yametoka wapi?” alihoji Jaji Werema.
Alisema kama kweli kutakuwa na baadhi ya vipengele ambavyo vitakuwa vimechomekwa kwenye sheria hiyo kinyemela, sheria hiyo inaweza kurudishwa bungeni kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho haraka.
Akizungumzia sheria hiyo, juzi Dk. Slaa alisema anashangazwa na kilichotokea Ikulu siku Rais Kikwete aliposaini sheria hiyo.
Dk. Slaa alisema atamchukulia hatua mtu aliyehusika kuongeza kipengele hicho bila idhini ya Bunge.
Katika kushangaa huko, Dk. Slaa alionyesha kitabu cha kumbukumbu za Bunge (Hansard), ambacho hakionyeshi viongozi wanaopaswa kufanya uhakiki wa timu za kampeni za wagombea.
“Katika sheria aliyosaini rais kuna kifungu cha 7 (3), ambacho hakikuwepo kabisa kwenye muswada uliojadiliwa na kupitishwa bungeni, kwa kweli nimeshangazwa sana, kwa sababu rais amedanganywa,” alisema Dk. Slaa.
Kabla ya kuzungumza na Jaji Werema, gazeti hili liliwasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, ili atoe msimamo wa Ikulu.
Alisema hana jibu, akamshauri mwandishi wa habari hizi kuwasiliana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, kwa kuwa ndiyo inayohusika zaidi na suala hilo.
“Sina cha kujibu katika hili, nakuomba uwatafute watu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, hawa ndio wako kwenye nafasi ya kuzungumzia suala hili kwa kina,” alisema Rweyemamu.
CHANZO: TANZANIA DAIMA
RISASI YAMKOSA JERRY MURO NA KUJERUHI MWINGINE!!
Habari ambazo gazeti hili ilizipata kutoka kwa chanzo chake cha kuaminika zilisema Jerry ambaye alikuwa mahakamani hapo katika kesi yake anayotuhimiwa kuomba rushwa na watuhimiwa wengine wawili, alinusurika kupigwa na kitu hicho kinachoaminika kuwa ni risasi na badala yake ikampata mtu aliyekuwa naye mahakamani hapo.
Mtu huyo alifahamika kwa jina la Dk. Paul Andrew ambaye ni mtaalamu wa tiba za binadamu na ilielezwa kuwa alikuwa amekuja mahakamani hapo kumsindikiza Jerry kwa maelezo kwamba ni ndugu yake.
“Sisi tunaamini aliyekusudiwa ni Jerry Muro kwa sababu Dk. Paul alikuja kwa bahati mbaya tu na hatufikirii kama waliorusha risasi walikuwa wakijua kuwa mtu huyo atakuja mahakamani lakini tunaamini waliofanya kitendo kile walijua kuwa Muro atakuwepo kortini na inawezekana walikuwa wakimngoja nje ndipo akapigwa mtu wake mguuni.” Kilisema chanzo hicho.
Habari zinasema, Dk. Paul baada ya kujeruhiwa akitokwa na damu nyingi, kitu kilichowashitua watu wengi walioshuhudia tukio hilo.
Mtoa habari huyo aliongeza kuwa walishuhudia gari moja dogo lenye ‘tinted’ ambalo hawakuweza kujua namba zake likitoka eneo hilo kwa kasi, kitu kilichowafanya waamini kwamba watu waliotenda kitendo hicho cha kurusha kitu kilichomjeruhi daktari huyo, walikuwa humo.
Chanzo hicho kilizidi kupasha kuwa baada ya watu, akiwemo Jerry kuona daktari huyo akivuja damu kupita kiasi mguuni huku akiwa ameanguka chini, waliamua kumkimbiza Hospitali ya Marie Stopes Mwenge ambako anafanyia kazi.
Habari zinasema alipofikishwa hospitalini hapo aliingizwa moja kwa moja chumba cha upasuaji ambako jeraha hilo lilishonwa.
Mwandishi wetu alimpigia Jerry ili kumuuliza kuhusu tukio la kurushiwa risasi iliyompata Dk. Paul lakini awali alikataa kusema chochote, hata hivyo, baada ya kubanwa sana akathibitisha kutokea tukio hilo.
“Ni kweli Dk. Paul nilikuwa naye mahakamani alinisindikiza na alijeruhiwa vibaya mguuni na watu wasiojulikana na akakimbizwa Hospitali ya Marie Stopes, lakini sitaeleza chochote zaidi ya hayo. Mtafuteni yeye awaelezee zaidi,” alisema Jerry.
Dk. Paul alipopigiwa simu alithibitisha kuumizwa mguuni na kitu anachoamini kuwa ni risasi na watu ambao hawajui.
Akisimulia mkasa huo, Dk. Paul alisema alikwenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumsindikiza Jerry anayekabiliwa na kesi ya kuomba rushwa na mara baada ya shauri kuahirishwa walitoka nje ya Mahakama.
“Tulitoka nje ya mahakama na nikiwa karibu na barabara ya lami gari moja lenye tinted rangi ya silver (fedha) lilipita kwa kasi na nikashitukia mlio wa chini pyuu, nikasikia mguu una ganzi na nilipoangalia nikakuta unavuja damu,” alisema Dk. Paul.
Alisema anaamini kitu hicho kilichomuumiza ni risasi kwa sababu kilitoboa hadi kiatu chake na kumjeruhi vibaya mguu wake, hali iliyosababisha avuje damu nyingi.
“Nilipata mshituko mkubwa ndipo ndugu na jamaa zangu wakanisaidia kunikimbiza Hospitali ya Marie Stopes ambako nilishonwa jeraha,” alisema Dk. Paul.
Wednesday, March 24, 2010
STIMU ZIMELIPIWA!!!
Mtoto huyu anaamua kulewa muda wote kwa ajili ya kupoteza mawazo,hapa alipo hana baba kwa hivyo hivi sasa anaishi na mzazi mmoja (mama anamuagiza kwenda mjini kuomba pesa na jioni akirudi wanagawana na mama yake kile alichokipata.
Wadau naomba maoni yenu juu ya tabia ya huyu mtoto,hatma yake nini?ameanza kuvuta kugundi mwishowe si ndio ataingia kwenye madawa ya kulevya na masuala ya ujambazi au nimekosea?Watoto kama hawa Serikali iwasaidieje manake ndio taifa la kesho……..Maoni yako tafadhali kama umeguswa….
IGP Said Mwema.
WAKATI habari za wizi wa kimafia wa Sh300 bilioni zikiwa zimeistua serikali, watu kumi wamekamatwa kwa tuhuma za wizi mwingine wa aina hiyo uliohusisha Sh360 milioni za benki moja nchini.
Kukamatwa kwa watu hao kumetokea siku moja baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti wizi huo mkubwa unaotumia teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta ambao ulifanyika kwenye benki nne kubwa nchini, taarifa iliyofanya Mamlaka ya Mapato (TRA) kuanza uchunguzi.
Mbali na taarifa za kukamatwa kwa watu hao, vyombo vya habari pia vimeripoti kukamatwa kwa mfanyabiashara mmoja aliyekuwa akifanya jaribio la kuiba kimafia Sh221 milioni kutoka benki ya NBC.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ambazo zilithibitishwa na msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Abdallah Msika zinasema watu hao walikamatwa kati ya Februari na Machi, katika msako wa jeshi hilo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga na Zanzibar.
Kukamatwa kwa watu hao kumetokea wakati benki zimekuwa zikihaha kubadili na kuboresha mifumo yake ya kuchukua na kutoa fedha kwa njia ya elektroniki kwa lengo la kukabiliana na uhalifu uliokithiri unaofanywa na watu walio ndani na nje ya nchi.
Akithibitisha kukamatwa kwa watu hao, Mssika alisema watano kati yao ni wafanyakazi wa benki hiyo (jina tunalo kwa sababu za kimaadili) na wengine ni kutoka nje ya benki hiyo na kuongeza: “Hadi sasa uchunguzi bado unaendelea.
“Wote wanatuhumiwa kwa wizi huohuo wa mtandao… baada ya kufanyika uchunguzi walibainika kuwa ni sehemu ya mtandao ambaon inatuhumiwa unahusika kwenye wizi huo.”
Kwa mujibu wa taarifa hizo zilizothibitishwa na Mssika, wizi huo ulifanyika katika kipindi cha kuanzia Januari lakini ulibainika kati ya Februari na ndipo uchunguzi ukaanza.
Msika alifafanua kuwa baada ya kufanyika uchunguzi ilibainika kiasi hicho cha fedha kilihamishwa kutoka tawi moja jijini Dar es Salaam na kupelekwa tawi jingine la mkoani Shinyanga.
Alisema baada ya kuhamishiwa tawi la Shinyanga, fedha hizo zilianza kuingizwa kwenye akaunti mbalimbali za wahusika ndipo baadhi yao waliponaswa.
“Fedha zilitoka tawi la Dar es Salaam na kupelekwa tawi la Shinyanga, baada ya kufika Shinyanga zilianza kuingizwa kwenye akaunti mbalimbali za watuhumiwa… tayari hao kumi wamekamatwa kuhusika na tukio hilo,” alifafanua msemaji huyo wa polisi.
Kuhusu kiasi cha fedha, alisema hadi sasa zimepatikana Sh319.5 milioni kati ya Sh360 milioni zilizoibwa na kwamba juhudi za kusaka nyingine na watuhumiwa zinaendelea.
Mssika aliongeza kwamba baada ya watuhumiwa wengine kukamatwa, watajumuishwa katika kesi inayowakabili watu hao kumi walio mikononi mwa polisi.
Katika hatua nyingine, Mssika alisema Jeshi la Polisi limetaka benki yoyote ambayo imekumbwa na tuhuma za wizi huo wa mtandao ziwasilishe taarifa zao polisi.
Mssika, ambaye alilirudia kauli ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba kuhusu taarifa za wizi mkubwa katika mabenki matatu, alisema hadi sasa hawajapata taarifa hizo kuhusu kiwango kilichoibwa na benki husika.
Wizi wa mtandao umekuwa ukikua kwa kasi nchini kutokana na matukio yaliyozikumba benki na tayari kuna kesi mbalimbali zinazohusisha wafanyabiashara wa Morogoro, walioba zaidi ya Sh1 bilioni katika moja ya benki nchini.
Lakini vyombo vya usalama ikiwemo polisi na mamlaka za serikali zimekuwa zikijaribu kufunika uhalifu huo.
Juzi wataalamu wa kubaini uhalifu wa kughushi kutoka Afrika Kusini walikuwa jijini Dar es Salaam kuangalia wizi mkubwa katika moja ya benki kati ya tatu zilizokumbwa na wizi huo wa kimafia wa Sh300 bilioni.
Benki hiyo ambayo inatajwa kuwa iliibiwa kiasi hicho kikubwa cha fedha, kwa sasa imeanza kurekebisha mfumo wake wa usalama wa fedha, hali ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu mkubwa kwa wateja wake kwa takriban wiki nne sasa.
Tayari maafisa wadogo wanne wa benki hiyo wameshaondolewa katika nafasi zao kwa ajili ya kupisha uchunguzi zaidi kubaini uhalifu huo na mtandao wake.
Uchunguzi wa wizi huo unahusisha pia maafisa waandamizi ambao wanatuhumiwa kuwa wanaweza kushirikiana na mtandao wa wahalifu wa kughushi kufanikisha wizi huo wa kimafia.
Mwaka 2005/2006 Benki Kuu (BoT) iliibiwa zaidi ya Sh133 bilioni katika akaunti moja ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) baada ya watu kughushi nyaraka zilizoonyesha kuwa walirithishwa madeni na makampuni ya nne na hivyo kujivunia mabilioni ya fedha.
Hadi sasa, wafanyabiashara kadhaa pamoja na wafanyakazi wa BoT wameshafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kula njama na kuiba fedha hizo,
Hata hivyo, baadhi ya walioiba hawakufikishwa mahakamani baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa msamaha kwa wale ambao wangezirudisha kabla ya Novemba mosi mwaka 2008.
Mbali na waliorejesha kiasi cha Sh70 bilioni, waliokwapua kiasi cha Sh40 bilioni pia hawajafikishwa mahakamani kutokana na wizi huo kuhusisha makampuni mengine yaliyo nje ya nchi na hivyo uchunguzi kuhitaji nguvu kubwa zaidi kuweza kuwabaini wahusika
blog ya jamii kutuwakilisha kongamano la pili la diaspora uingereza
Mwasisi wa habari za jamii mtandaoni (social media) nchini Bw. Muhidin Issa Michuzi anaondoka leo Jumatano kuelekea London, Uingereza, kuhudhuria kongamano la pili la Watanzania wanaoishi nchi za nje (Diaspora 2 conference) kwa mwaliko maalumu akiwa kama blogger.
Bw. Michuzi, ambaye ametoa mchango mkubwa katika kupromoti habari za jamii mtandaoni kupitia blog yake maarufu ndani na nje ya nchi iitwayo issamichuzi.blogspot.com, amealikwa huko mkutanoni na ubalozi wetu Uingereza ili kutoa mada inayohusu umuhimu wa habari za jamii mtandaoni katika kujenga daraja kwa walio ndani na nje ya nchi.
Akiongea nasi leo kabla ya kukwaa pipa la shirika la ndege la Emirates, Bw. Michuzi ambaye pia ni maarufu kwa majina kama Mzee wa Libeneke, Mdau na Ankal, amesema amefarijika sana kuona kumbe kuna wanaotambua mchango mkubwa unaoletwa na vyombo vya habari za jamii mtandano, hasa blogs.
Amesema anajisikia mwenye furaha sana kuona azma yake ya kuifanya tasnia hii ya kupashana habari kwa njia ya intaneti kwa waandishi wa hapa nyumbani unatambulika na kukubalika na kupewa heshima stahili kama ilivyo kwa vyombo vya kawaida kama vile magazeti, redio na luninga.
Bw. Michuzi, anayeweka rekodi ya kuwa bloga wa kwanza nchini kualikwa kama bloga kwenye mkutano muhimu kama huo, anaushukuru ubalozi wetu Uingereza chini ya Balozi Mh. Mwanaidi Maajar ambaye naye anakuwa miongoni mwa wazalendo wa kwanza kuutambua hadharani mchango wa wanahabari za jamii mtandaoni kwa kutoa mwaliko huo.
"Nilijua iko siku wanahabari za jamii mtandaoni tutatambulika na mwaliko huu hakika umekuja wakati muafaka kwani msisimkmo na mwitikio wa jamii kuikubali njia hii ya mawasiliano hapa nyumbani umekuwa mkubwa kuliko ilivyotarajiwa.
"siku hizi habari za jamii mtandaoni zinachukua kiti cha mbele katika kusomwa na wenye kuwa na intaneti kutokana sio tu na habari kuwa za uhakika, zisizochujwa na za haraka bali pia kwa kule wasomaji kupata fursa ya kuchangia habari waionayo tofauti na ilivyo kwa magazeti, redio na luninga."
Dunia imezidi kuwa kijiji kimoja kidogo kwa teknohama hii ambayo hata Rais Jakaya kikwete yuko mstari wa mbele kutaka iendelezwe mijini na vijijini ili kuwezesha wananchi wawe na habari za uhakika, za haraka na zenye kutoa fursa ya wasomaji kuchangia maoni" alisema Bw. Michuzi.
Blog ya issamichuzi.blogspot.com ilianza rasmi Septembe 8, mwaka 2005 katika jiji la Helsinki, Finland, ambako alikwenda kuhudhuria mkutano wa Helsinki Conference akiwa kama mwandishi na mpiga picha wa gazeti la Daily News.
Alikuwa ni bloga wa siku nyingi aliyekuwa anaishi Marekani wakati huo, Bw. Ndesanjo Macha, aliyemshawishi Bw. Michuzi kufungua blog yake na kuwa bloga wa kwanza wa Tanzania kuupasha ulimwengu ya kila linalojiri nchini, kazi ambayo ameifanya kwa ustadi mkubwa kiasi ni hivi majuzi tu ameweza kufikisha wasomaji milioni 8, kati ya hao asilimia 30 wakiwa ni wasomaji wa hapa hapa Tanzania.
Bw. Michuzi ameweka wazi kwamba amefurahi na kusisismkwa sio kwa sababu anakwenda ulaya, kwani ameshatembelea karibu miji mikubwa yote duniani, ukiondoa Australia na New Zealand, ila amefarijika kwa sababu hatimaye blog zimeanza kutambuliwa rasmi.
Anatoa masikitiko yake kwamba pamoja na fanaka hiyo, lakini bado hapa nyumbani jamii, hasa ya mahafidhina (conservatives) wasiotaka mabadiliko wamekuwa wazito kukubali kwamba vyombo vya habari za jamii mtandaoni vimeshapata nguvu sawa na vyombo vya kawaida kutokana na wingi wa wasomaji na hata kupelekea kujitokeza kwa wadhamini wanaotangaza biashara zao humo.
Pamoja na mambo mengine, Bw. Michuzi amesema anatamani sana kuanzisha umoja wa wanahabari za jamii mtandaoni ili kutetea na kulinda maslahi yao pamoja na kuindeleza tasnia hii ambayo inakua kwa kasi za ajabu.
Kwa mahesbu ya haraka haraka hivi sasa kuna blog zinazotumia lugha ya kiswahili zipatazo 200 ambapo pia blog takriban 10 zinaanzishwa kila siku, na kuifanya Tanzania kuw nchi zinazoendelea katika tasnia ya habari kwa njia ya mtandao.
umbea.com inakutakia safari njema mzee mzima
Tuesday, March 23, 2010
JAMANI HII MIGOMO ITAISHA LINI????
Adris John akizungumza na halaiki ya wanafunzi wa IFM leo juu ya adhma ya mgomo wao na kusalitiwa kwa viongozi wao.
Baadhi ya wanafuzni wa chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM Dar es salaam walikusanyika katika eneo la wazi chuoni hapo jana wakati wakihamasishana kuanza mgomo wa kupinga ongezeko ala ada lililopanda kati ya asilimia 50 na 70.
Makundi makubwa ya mijadala yalizuka kila mmoja akiteta lakwake.Migomo imeshakuwa swala la kawaida katika baadhi ya vyuo. Huu ni wakati wa kutafuta njia maalum ya kudhibiti migomo hii, mikakati kabambe ipangwe kuepusha migomo mingine huko mbeleni.

Wizi kupitia mtandao watinga nchini
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi Afande Abdallah Mssika
JESHI LA POLISI HALINA TAARIFA ZA KUIBWA KWA SHILINGI BILIONI 300 KUTOKA KATIKA MABENKI MBALIMBALI HAPA NCHINI
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi nchini limesema halina taarifa za wizi wa shilingi Bilioni 300 zinazodaiwa kuibwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta kutoka katika mabenki mbalimbali yaliyounganishwa na mtandao huo hapa nchini.
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, amesema jana kuwa taarifa zilizoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na wizi huo hazijafikishwa Polisi.
Kamanda Mssika amesema kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Ma
kosa ya Jinai Kamishna Robert Manumba, aliyedaiwa kukaririwa na chombo hicho cha habari, amesema kuwa hana taarifa ya tukio la wizi wa shilingi Bilioni 300.
Kamishna Manumba amesema kuwa mawasiliano kati yake yeye na Mwandishi wa taarifa hiyo kwa upande wake binafsi yalihusu tukio la wizi wa fedha katika benki ya NMB Tawi la Bank House Jijini Dar es Salaam ambapo mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu, ambapo Jeshi la Polisi lilibaini kuibwa kwa shilingi milioni 360 kwa njia ya mtandao wa kompyuta fedha ambazo zilihamishiwa katika tawi moja wapo la benki hiyo lililopo mkoani Shinyanga.
Kamanda Mssika amefafanua kuwa, mara baada ya fedha hizo kufika Mkoani Shinyanga, zilitawanywa kutoka katika tawi hilo na kupelekwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta kwenda katika akaunti mbalimbali za watu binafsi kwenye matawi mengine ya benki hiyo katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Kutokana na wizi huo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Benki ya NMB limeshafanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 319 kati ya shilingi milioni 360 zilizoibwa na kwamba tayari baadhi ya watuhumiwa waliohusika katika wizi huo wakiwemo watumishi watano wa benki wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu shitaka lao.
Hata hivyo Kamanda Mssika amesema kutokana na taarifa za kuibwa kwa shilingi bilioni 300, kama ilivyoandikwa, ametoa wito kwa Makampuni ama Taasisi za Kifedha zinazoweza kuwa zimefanyiwa hujuma hiyo ya wizi na iwapo rasimu zao za ndani kiuchunguzi zimekamilika, basi wawasiliane na Mkurugenzi wa makosa ya Jinai nchini Kamishna Robert Manumba, ili hatua za uchunguzi ipasavyo kwa kuvishirikisha vyombo vya dola ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Monday, March 22, 2010
UBALOZI WA NIGERIA NCHINI LIBYA WAFUNGWA SABABU YA GHADAFI!
Nigeria imemwamuru balozi wake nchini Libya, arejee nyumbani kufuatia matamshi ya rais Muammar Gaddafi, aliyopendekeza taifa hilo ligawanywe mara mbili, moja ya wakristo na nyingine ya waislamu.
Wizara ya mambo ya nje ya Nigeria imetaja matamshi hayo ya Gadaffi, kama ya uchochezi. Rais wa bunge la senate nchini Nigeria, David Mark amesema, rais Gadaffi ni mtu asiyekuwa na akili timamu.
Mapema wiki hii kiongozi huyo wa Libya, alisema njia ya pekee ya kusitisha mauaji ya raia nchini Nigeria ni kuigawa nchi hiyo kuwa mataifa mawili.
Mamia ya watu wameuawa katika siku za hivi karibuni nchini Nigeria kufuatia ghasia za kidini na kikabila katika jimbo la Plateau kati kati mwa nchi hiyo.

MABANGO YA ASKOFU KAKOBE YALA NGWARA!!
Mshkaji akiwa amejiokotea taa ya bure iliyokuwa ikimulika mabango hayo!
Mzimu wa Shirika la umeme nchini umeendelea kumwandama Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Bible Fellowship la Mwenge jijini Dar es Salaam, Zachary Kakobe baada ya mabango ya kanisa lake kuvunjwa, kupisha ujenzi wa njia ya umeme wa msongo mkubwa.
Kutokana na hali hiyo Askofu Kakobe atawajibika kuilipa serikali fidia ya ubomoaji huo, kwa kile kinachoelezwa kuwa alikaidi kuondoa mabango mbele ya kanisa hilo ili kuruhusu njia ya umeme kupita.
Wiki chache zilizopita, serikali ilipuuzia mbali malalamiko ya Kakobe ya kutaka njia hiyo ya msongo mkubwa wa umeme kupita mbele ya kanisa hilo.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mkoa wa Dar es Salaam, James Nyabakari alisema jana kwamba tayari wametoa baraka zote kwa Tanesco kufanya tathmini ya kuondoa mabango hayo ili Kanisa la Askofu Kakobe liwajibike kuzilipa.
Mafundi wa Tanesco jana walishuhudiwa wakiyaondoa mabango hayo mawili yenye urefu unakadiriwa kufikia futi 40 na upana futi 20 chini ya ulinzi wa polisi.
"Tutatoa agizo kwa Kakobe kulipa fedha hizo baada ya Tanesco kumaliza kazi na kuleta gharama walizotumia," alisema Nyabakari.
Awali baadhi ya waamini wa kanisa hilo walionyesha kutaka kutoa upinzani ili kuzuia zoezi hilo, lakini walishindwa baada ya kuona linasimamiwa na polisi.
Tanroads ilikuwa imetoa notisi ya siku saba kwa kanisa hilo kuyaondoa mabango hayo, tangu Machi 9, mwaka huu kwa sababu yalikuwa yamejengwa kwenye eneo la hifadhi ya barabara.
Nyabakari alisema kwamba hadi jana siku 20 zilikuwa zimepita na Askofu Kakobe alionekana kukaidi amri hiyo.
ANISA, MBUNIFU ANAYEZIDI KUPAA LEVO ZA KIMATAIFA!
Ndiye mtanzania wa kwanza kwa ubunifu ambaye ameweza kushiriki katika onesho kubwa la mitindo la New York Fashion Week ambaye February mwaka huu 2010, ameshiriki kwa kuonesha mavazi yake huko na kung'aa sambamba na wabunifu wakubwa akiwemo Deola Sagoe,BCBG Maxazria,Tommy Hilfiger,Calvin Klein,Venexiana na wengineo wengi
Namzungumzia mtanzania, Anisa Mpungwe (24), mkazi wa jijini Dar es Salaam, ambaye ameshinda tuzo ya mwanamitindo mpya wa Elle, katika hafla iliyofanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Septemba 15, 2009
Shindano hilo liliandaliwa na Kampuni ya Mitindo ya Elle ya Afrika Kusini ambayo hujishughulisha na maonyesho ya mitindo na urembo.
Anisa ambaye ni mtoto wa aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Ami Mpungwe. kuanzia mwaka 1994 hadi 1999, aliibuka kidedea baada ya kuchaguliwa katika wanamitimndo 100 walioshiriki katika shindano hilo kutoka nchi za Kusini mwa Afrika, ambapo baada ya mchujo walibaki washindi sita tu.
Kisha washindi hao sita waliweza kuchujwa tena ili kuweza kupata mshindi wa tuzo hiyo ya fahari ya mitindo ya Elle New, ambapo Anisa alitangazwa kuwa mshindi.
Kutokana na ushindi huo, Anisa amejinyakulia kitita cha dola 2000, ambazo ni sawa na zaidi ya sh milioni mbili za Kitanzania.
Zawadi nyingine aliyoipata Anisa katika shindano hilo ni pamoja na kuingia mkataba wa kubuni mitindo kwa ajili ya kampuni ya nguo ya Mr. Price ambapo nguo hizo zinapatikana kwenye nchi mbalimbali linapopatikana duka la kampuni hiyo.
Kwa upande wake Anisa alisema kuwa fedha alizozawadiwa atazielekeza katika kukuza kampuni yake ya uanamitindo aliyoifungua huko Afrika Kusini inayofahamika kwa jina la Loins Clothes & Ashes, ambayo itakua ikibuni mitindo na kuionyesha mavazi katika maonyesho mbalimbali hapa nchini.
HAKUNA HELA MBOVU, ATAYEIKATAA KUSHITAKIWA!!
Serikali imewasihi na kuwaomba radhi baadhi ya wananchi kuacha kukataa baadhi ya fedha halali zilizoko kwenye mzunguko kwa madai kuwa hazifai kwasababu ya uchakavu wake.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa wizara ya uchumi na fedha, Ramadhani Kijah, hakuna sheria inayomruhusu mwananchi kuzikataa fedha hizo.
Alisema ingawa kuna malalamiko ya uchakavu wa koini za sh 100, alisema hiyo siyo sababu ya kuzikataa kwani zinatambulika na sheria.
"Fedha hizo zitumike hadi hapo zitapofika benki amabako ndiko zitakuwa mwisho wake kwani kule kuna watu maalumu waliojariwa kuteketeza pesa mbovu na hata hela chafu," alisema Kijah.
Kijah alisema kwa yeyote atakayepinga kupokea fedha hizo basi atambue kuwa anapingana na sheria zilizowekwa na serikali hivyo atakuwa anajijengea mazingira ya kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Saturday, March 20, 2010
“MO KUMSIMIKA KAMANDA WA UVCCM MAGU-MWANZA LEO”
Mh.Mohammed Dewji.
Mh.Mohammed Dewji Mbunge wa Singida mjini,ameondoka Dar es Salaam jana,kuelekea Mkoani Mwanza kwa ajili ya Sherehe za Kumsimika Ukamanda Mbunge wa jimbo Busega,Mh.Raphael Chegeni,Sherehe hizo zitafanyika katika Wilaya ya Magu,Mkoani Mwanza,Mh Dewji pia atashiriki katika Harambee ya Amani SACCOS katika kijiji cha Lamadi jimbo la Busega.
Hon. Lawrence Maasha Minister of Home Affairs hosted Samsung Miss Tanzania India Richa Adhia at his office at the Ministry on 19 March, 2010 where he
Hon. Lawrence Maasha Minister of Home Affairs hosted Samsung Miss Tanzania India Richa Adhia at his office at the Ministry on 19 March, 2010 where he handed her The Tanzanian Flag as She represents for the First Time TANZANIA at the 19 Miss India Worldwide Pageant to be Held in Durban South Africa on March 27, 2010.
Friday, March 19, 2010
KIBAKA AKILA KICHAPO TOKA KWA WANANCHI WENYE HASIRA KALI!
KWELI BONGO MISHEMISHE!
Ama kweli bongo misheshe kamera yetu ya UMBEA.COM ilikuwa mitaani kama kawaida yake ya huku na kule na bahati nzuri ilikutana na huyu kijana akifanya biashara ya kuuza kahawa maeeneo ya kariakoo sokoni huku akiwa vutia wateja wake kwa alivyo vaa na utani ndani yake!big up sana kaka uko creative kinoma
Picha na inno lyimo
Picha na inno lyimo
BABA NA MWANA MGONGONI.....................................
Adhabu hizi zinafundisha au udhalilishaji?
Wengi tiliosoma Saint Government aka St. Mchangani tushashika masikio kwa style hii sana tu!
Ukiona kama mchezo, ila unaumia, acha tu, miguu inakosa nguvu kabisa, afu kama una ugonjwa wa kutoka damu puani, au kusikia kizunguzungu inakua balaa!
Afu kuna ya kuita juu, mkiwa wengi mtu anaweza kudhani mnafanya choreography, maana inapendeza, kumbe mnateseka, ila fimbo ndio kiboko ya wote!
Ingawa siku hizi watoto wengi wanasoma St Private aka English Academy, no fimbo, no adhabu kali, je adhabu hizi zilikua zinasaidia?
picha na inno lyimo
Subscribe to:
Posts (Atom)