Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, March 6, 2010

UWOYA RUDI KWA MUMEO KHAAA!Ishu hiyo imekuwa ‘hoti tauni’ siku chache baada ya mcheza filamu ‘brazameni’ Vicent Kigosi ‘Ray’ kuweka picha za matukio mbalimbali ya kurekodi filamu zikimuonesha Irene akiwa katika mapozi ya kihasarahasara ndani ya mtandao wake.

Kwa mujibu wa wadau waliotembelea ‘blogi’ ya Ray, mnyange huyo anadaiwa kujirahisi zaidi na mastaa wa kiume wa Bongo katika uandaaji wa filamu anayofanya chini ya Kampuni ya RJ Productions, jambo ambalo siyo maadili ya mke wa mtu.

Wadau hao walikwenda mbali zaidi na kudai kwamba, kwa mwanaume yeyote mwenye wivu kwa mkewe, akatokea kuziona picha hizo kwa namna moja ama nyingine, lazima atajihisi vibaya hata kama anamuamini mkewe kwa asilimia elfu moja.

Ishu hiyo ilipamba moto zaidi pale ilipotundikwa picha ya Irene na Dr. Cheni wakibusiana ambapo wadau hao walionekana kukemea kwa nguvu zote kitendo hicho hata kama ni kwenye filamu.
Baadhi ya maoni ya wadau hao yalisomeka kama ifuatavyo;
Machi 1, 2010 2:37 Mchana, mdau Clara alisema:

“Jamani huyu dada ni mzuri sana, hongera kwa aliyewahi, lakini jamani duh!”
Machi 2, 2010 2:55 Asubuhi, mdau ambaye hakujitambulisha jina lake alisema: “Jamani kwa hili, mimi naona Ndikumana anadhulumiwa kabisa! Hii michezo ya movie za kimapenzi kwa mke wa mtu haviendani walahi. Usikwazike Ray.”

Machi 2, 2010 6:40 Mchana, mdau mwingine alisema: “Huyo Irene anavyokula denda hivyo, si mke wa mtu huyo? Kazi nyingine bwana! Mimi angekuwa ndiyo mke wangu, wala nisingekubali. Khaa! Irene bora urudi kwa mumewe Cyprus.”
Machi 3, 2010 4:06 Asubuhi, mdau mwingine alisema: “Oya Cheni, kwanini sasa unaumiza mioyo ya wenzio? Shauri yako, Ndikumana anaumia huku, atakushukia bure.”

Wiki mbili zilizopita, Irene alikaririwa na UMBEA.COM akisema kwamba, yupo nchini kwa muda wa mwaka mmoja na katika kipindi chote hicho atakuwa ‘siriasi’ na kazi za filamu.

No comments:

Post a Comment