Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, April 4, 2010

Kamanda Kova Are you Serious au Unatania??


Mtoto wa mjini Kamanda Suleiman Kova,ameagiza bar zote zilizo near vituo vya polisi jijini dsm zipigwe chini kwa ajili ya usalama wa vituo hivyo.

Mkwara huo wa Kova unakuja wakati akitoa ufafanuzi kuhusiana na malalamiko aliyoyapokea kutoka kwa baadhi ya wananchi wakidai uwepo wa sehemu hizo za kupatia moja moto moja baridi...unasababisha muingiliano kati ya bar na vituo vya polisi na hivyo kuondoa ufanisi wa uwajibikaji wa vituo hivyo...haswa pale polisi wanapochomoka mara kwa mara wanaposhikwa na kiu kwenda kutii kiu zao.

Kwa mujibu wa kamanda huyo mwenye maneno mengi ya kimjini,vituo hivyo haviwezi kuondoshwa na kubakizwa baa kwa kuwa baa siyo muhimu kama vituo vya polisi ambavyo vinahudumia jamii kubwa ya wananchi katika maeneo yao.

"Kwa mfano..kituo kama cha Kimara Bucha kipo karibu na baa hivyo naagiza kuwa baa zote zilizopo karibu na vituo vya polisi lazima zibadilishwe na kuuuza bidhaa nyingine ambayo haileti usumbufu wa kelele na ushawishi kwa vituo vya polisi." alisema Kova ambaye haijaeleweka ametoa wapi sheria hiyo ambayo kwa vyovyote itapingwa vikali na wafanyabiashara wa Bar mbalimbali jijini wakisaidiana na sisi wanywaji.

"Baa hazina umuhimu kama vituo vya polisi na tutafanya mpango ili viweze kubadilishwa kuendesha shughuli hizo na kupewa leseni za kuwa maduka ya bidhaa nyingine za kawaida kama uuzaji wa vifaa vya magari, na bidhaa nyingine tofauti na baa na kazi hiyo itaanza kufanyiwa kazi haraka ili kuimarisha ulinzi katika maeneo hayo," alisisitiza.

Hivi Kova utaweza kunilazimisha mimi niache biashara yangu ya kilauri..ili nifanye ya kuuza unga! kwasababu tu niko karibu na vituo vyake? ahhh hapa lazima tutakwazana...ni mtazamo tu lakini.

No comments:

Post a Comment