Habari mbalimbali toka pande za bongo bila kusahau matukio mbalimbali yanayorindima pande zote za dunia
Psquare Ft. J.Martins- E No Easy
Monday, May 31, 2010
AY kupiga Collabo na Sean Kingstone!!
Habari zilizopo ni kuwa yule mwakilishi wa muziki wa Bongo Flava nje ya nchi Ambwene Yessayah anatarajia kuangusha mzigo na msanii Mkali toka Jamaica ambaye siku za karibuni alidondoka kufanya show ya nguvu nchini, si mwingine ni Sean KingStone.
Sean Kingstone mwenyewe akihojiwa na Radio mmoja nchini hivi karibuni alipoulizwa ni mwanamuziki gani ambaye anamtambua hapa bongo na angependa siku moja afanye nae kazi, jamaa bila kusita alisema AY.
“Nilipokutana na jamaa kweli alisema anavutiwa na kazi zangu, akaniomba tukapige colabo, ni mtu ambaye hana mapozi na ilikuwa nipige naye ngoma moja hapa Bongo lakini bahati mbaya Producer wangu, Hermy Bakawa amesafiri. Kwa kifupi amenipa moyo sana, nikienda huko natarajia kufanya maajabu,” alisema A.Y
Unaifahamu hii??
Hii ni Barrett M82 semi automatic a.k.a mali mpya ya wanajeshi wa Obama.
Mashine hii ndio iliyowakomesha wale jamaa waliokuwa wakileta fujo kulee Afghanistan. Risasi yake ina uwezo wa kwenda umbali wa mita 6,812 ambayo ni sawa na futi 22,349. Pia ina uwezo wa kupenya kwenye vifaru vya kivita!!
Hii sio ya kuchezea!!
Sasa ikikupata sijui kama utapona!
Nina mapacha tumboni mwangu!!
Hatimaye superstar aliyegonga wimbo mtamu wa "My heart will go On",Celine Dion, amejitokeza na kuwaeleza mapaparazzi waliokuwa wakimfwatilia na kumchunguza kila kukicha kama yeye ni mjamzito.
Mwanamama huyo machachari mwenye miaka 42 alisema ana uja uzito wa miezi 14 na anategemea kujifungua watoto mapacha!
Kabla ya mimba hiyo tayari alikuwa na mtoto Rene Charles mwenye miaka 9.
Pia aliwataka wapenzi wa muziki wake kukaa mkao wa kula sababu anakuja na album mbili mpya zilizoshiba!
Brazil kutua na makocha 27
Kikosi cha timu ya Brazil kinatarajiwa kutua nchini Juni 6 mwaka huu kikitokea Zimbabwe ambapo kitaongozana na jopo la makocha 27. Rais wa TFF, Leodgar Tenga amesema katika ujumbe wa watu 60 utakaotua nchini, makocha pekee watakuwa 27 huku wachezaji wakiwa 23.
“Huu utakuwa ni ugeni mkubwa wa kwanza ukiachilia tatu zilizowahi kufika hapa nchini ambazo ni Senegal, Cameroon pamoja na Ivory Coast. Kwa sababu hiyo utaona kuwa mambo mengi yatakuwa ni tofauti na ilivyokuwa imezoeleka wakati timu nyingine zinapowasili hapa Tanzania,” alisema Tenga.
Kwa upande wake wakala wa kuandaa mechi anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Philippe Huber alisema walichagua Brazil kucheza mchezo huo dhidi ya Taifa Stars nchini Tanzania kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo ukarimu na mazingira bora ya usalama yaliyopo tofauti na mataifa mengine ya jirani na Afrika Kusini.
Brazil itawasili Juni 6, mwaka huu kisha kucheza mechi moja dhidi ya Stars Juni 7, mchezo utakaofanyika kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
TID siyo Kioo cha Jamii!!
Mkali mpya wa rnb kwa bongo sasa Rama D ameibuka na kumpaka “Live” mkali mwengine kwenye miondoko hiyo na mkongwe kabisa kwenye game hili la bongo Fleva Khaleed Mohamed a.k.a Top In Dar.
Rama D ambaye alikuwa akihojiwa na kituo kimoja cha Radio Rama D alisema TID hawezi kuwa kioo cha Jamii hata sikumoja kutokana na tabia zake mbaya mbele ya jamii kila kukicha.
“Unajuwa jamaa kwa upande wa usanii kafika mbali kusema kweli anajitahidi sana, lakini kama kioo cha jamii alitakiwa awe mfano mzuri lakini badala yake yeye kila siku ndiyo anafanya vurugu kwa kuharibu ovyo"alisema Rama D.
Mahakama ya ICC kujadiliwa Uganda!!!
Wajumbe kutoka zaidi ya nchi 100 wanakutana mjini Kampala Uganda, kujadili mafanikio ya Mahakama ya Kimataifa ya jinai ICC, tangu ilipobuniwa miaka minane iliyopita.
Mahakama hiyo kwa sasa inaendesha uchunguzi wa kesi tano kuu, zote kuhusu washukiwa kutoka barani Afrika.
Hadi kufikia sasa mahakama hiyo haijatoa hukumu yoyote dhidi ya mshukiwa yeyote, ingawa mwendesha mkuu wa mashtaka, Luis Moreno-Ocampo, amefahamisha BBC kuwa kuwepo kwa mahakama hiyo kumebadili ambavyo majeshi, serikali na hata mahakama za nchi tofauti zinavyoendesha harakati zao.
Kongamano hilo pia litajadili uwezekano wa kufanyia mabadiliko sheria za makubaliano ya Rome yaliyopelekea kundwa kwa mahakama hiyo miaka kumi na mbili iliyopita.
Sunday, May 30, 2010
Hausiboi aua watoto wa bosi kwa sumu!
Vilio, simanzi na butwaa vimeikumba familia moja na majirani zao wilayani Sengerema baada ya kushuhudia madenti watatu wakikata roho muda mfupi baada ya kula chakula kilichoandaliwa nyumbani kwao kinachosadikiwa kuwa na sumu.
Kwa mujibu wa mashuhuda, sumu hiyo iliwekwa na hausiboi katika nyanya zilizoungiwa mboga ambayo walikula watoto hao ambapo inadaiwa kuwa ilitokana na matajiri wa kijana huyo kutishia kutomlipa mshahara wake.
Imedaiwa kuwa kijana huyo, ambaye ni raia wa Burundi, aliuza nyanya za matajiri hao kwa bei nafuu, hivyo kuwapa hasira matajiri wake ambao waliahidi kutomlipa mshahara wake kisha kumuagiza kuwa aende shambani akachume nyanya kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwa siku hiyo.
Kutokana na hali hiyo, hausiboi huyo alichukia na ndipo alipokwenda dukani kununua sumu hiyo ambayo haijafahamika mara moja na kuiweka kwenye nyanya hizo.kisha kuzichuna kidogo na kuweka sumu hiyo.
Baada ya kumkabidhi hausigeli alizipikia chakula hicho na baada ya kuiva alitaka kula na mtoto mdogo wa miaka minne anayeshinda naye ambapo hausiboi huyo alimuonya kutokula chakula hicho kwa madai kuwa ni maalumu kwa ajili ya matajiri wake.
Kauli hiyo ilimfanya hausigeli yule ahamaki na kuhoji mbona siku nyingine huwa wanakula ndipo hausiboi huyo alipomtakia kuwa kama anataka kufa ale chakula hicho.
Kutokana na kauli hiyo, hausigeli huyo aliacha kula chakula hicho na baada ya saa chache watoto watatu wa mwenye nyumba hiyo walirejea nyumbani wakitoka shule na kuanza kula chakula hicho.
Baada ya muda wa dakika 30 watoto hao walianza kulalamika tumbo huku wakitokwa na jasho jingi. Ingawa walijitokeza wasamaria wema na kuwakimbiza hospitali, walifia njiani kabla hawajapatiwa matibabu.
Saturday, May 29, 2010
MICHAEL ESSIEN KUZIKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA
mchezeshaji wa Timu ya Taifa ya Soka ya Ghana na klabu ya Chelsea ya Uingereza,Michael Essien(pichani), atazikosa fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Chama cha Soka cha Ghana(GFA),kiungo huyo ambaye kwa muda sasa amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti,hatoweza kupona mpaka hapo mwishoni mwa mwezi wa saba(Julai) na hivyo kumaliza kabisa matumaini ya kuweza kucheza katika fainali hizo.
Uamuzi wa mwisho wa kumuondoa Essien katika kikosi cha Ghana(Black Stars) ulifikiwa na chama hicho cha soka kwa kushauriana kwa karibu na timu yake ya Chelsea pamoja na daktari wake na pia madaktari wa Timu ya Taifa ya Ghana.
Pamoja na kwamba hatocheza,habari zinazidi kupasha kwamba Michael Essien ataambatana na timu hiyo kwenda Afrika Kusini na kwamba atasaidia katika masuala mengine ya kiufundi.Ghana wapo kundi D pamoja na Ujerumani, Australia na Serbia. Wataingia uwanjani kwa mara ya kwanza tarehe 13 Juni kupambana na Serbia.
Marekani yatoa onyo la ugaidi Kombe la Dunia!!!
Serikali ya Marekani imetoa onyo kwa raia wake kuwa Afrika Kusini inakabiliwa na tishio la ugaidi wakati wa Kombe la Dunia.
Imesema matukio yanayoshughulisha umati mkubwa wa watu huwavutia magaidi kufanya mashambulio.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema, ” Kuna hatari kubwa kuwa makundi ya wapiganaji yanaweza kufanya ugaidi ndani ya Afrika Kusini siku za usoni.”
Onyo hilo limetolewa wakati Rais Barack Obama akiitakia kheri timu ya soka ya Marekani.
Bw Obama, aliyeambatana na aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Bill Clinton aliwaaga wachezaji hao kwenye ikulu ya White House, ” Nataka tu kusema jinsi gani tunavyosikia fahari juu ya timu hiyo.”
Amesema, ” Kila mmoja atakuwa anawashangilia.”
“Na japokuwa mara nyingi hatukumbuki hilo hapa Marekani, hili litakuwa shindano kubwa zaidi la soka duniani.”
Katika taarifa iliyotolewa, wizara ya mambo ya nje imesema haina taarifa kamili ya vitisho wakati wa mashindano hayo, lakini vitisho vimeripotiwa na vyombo vya habari.
Afrika Kusini imeandaa maelfu ya polisi waliopitia mafunzo maalum kushughulika na usalama wa mashabiki.
Takriban watu 350, 000 wanatarajiwa kutembelea Afrika Kusini kwa ajili ya Kombe la Dunia, linalofanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika
Chadema yaungana na maaskofu!
Siku moja baada ya maaskofu kuzindua umoja wao na kuiomba serikali kubadili siku ya Uchaguzi Mkuu kutoka Jumapili kwenda siku za kazi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeunga mkono ombi hilo na kuitaka serikali kulifanyia kazi bila kusita.
Chama hicho kimesema kupanga Uchanguzi Mkuu kufanyika siku ya Jumapili inasababisha wakristo wanaotumia siku hiyo kwa ibada kukosa haki yao ya kuchagua viongiozi wao kutokana na baadhi yao kubanwa na masuala ya kiimani siku nzima na kushindwa kupiga kura.
Akikaririwa mapema jana Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe alisema suala la Uchaguzi Mkuu ni nyeti hivyo ni vizuri ikatengewa siku moja ya kazi badala ya kutumia siku ya Jumapili kama ilivyozoeleka.
“Hoja ya Maaskofu ni zuri na ina umuhimu wake, kimsingi Uchaguzi Mkuu ni suala nyeti sana na linatakiwa liwe na siku yake tofauti, badala ya kuchukuliwa kama ilivyo sasa, hata katika nchi zilizoendelea hawafanyi uchaguzi Jumapili, ni vizuri tukitenga siku moja ya kazi kuwa ni ya Uchaguzi Mkuu,” alisisitiza Bw. Mbowe.
Alisema siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili zinapaswa kutumiwa na viongozi wa dini na waumini wao kuombea Uchaguzi Mkuu, hivyo hazistahili kutumika kama siku za uchaguzi.
“Wapo baadhi ya watu wanakosa haki yao ya msingi ya kupiga kura kwa kuwa wanabanwa na mambo ya kiimani na haki yao kufanya hivyo, baadhi ya watu pia wanatumia siku hiyo kupumzika na hawako tayari kufanya kazi ya kujipanga kwenye mistari ya kupiga kura, siku moja ya kazi ikitumika kwa ajili ya uchaguzi Mkuu ni bora zaidi,” alisisitiza Bw. Mbowe.
Alipoulizwa kuhusu athari za kiuchumi kwa Taifa zima kupoteza siku nzima kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu badala ya kuzalisha, kiongozi huyo alisema manufaa ya uchaguzi ni makubwa kuliko siku moja ya kazi kwa kuwa watu wasipotumia siku hiyo moja vizuri athari zake ni kubwa na hudumu kwa kipindi cha miaka mitano.
Lakini Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Yusuph Makamba alipoulizwa msimamo wa chama chake kuhusu kauli hiyo, aliema kwamba yeye na chama chake ni watumishi wa bwana hivyo watafuata kile kitakachoamriwa na bwana wao (Tume ya Taifa ya Uchaguzi).
“Mimi ni mtumishi wa bwana, na bwana wangu ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), nitafanya kile atakachoagiza bwana wangu, sina cha kusema hapo nasubiri bwana wangu apange iwe ni siku gani mimi nitafuata,”alisema Bw. Makamba.
Wananchi wavamia polisi na kuua majambazi!
Mamia ya watu wakiwa na silaha wamevamia na kuvunja kituo cha kidogo cha polisi cha kata ya Mbarika, wilayani Misungwi kisha kuua watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi sugu.
Imeelezwa kuwa askari polisi wa kituo hicho, walizidiwa nguvu na wananchi hao, hali iliyosababisha kukimbia ili kuokoa maisha yao.
Habari za kuaminika kutoka eneo la tukio zinasema majambazi hayo yalikamatwa wakati yakijiandaa kufanya uhalifu na kufikishwa kituoni hapo kwa ajili ya kufikishwa mbele ya vyombo vya dola.
Habari zinasema, majambazi hayo yameuawa vibaya kwa kuchanwachanwa huku baadhi ya viungo vyao kama vile utumbo vikiwa vimezagaa katika eneo la tukio.
Imeelezwa katika tukio hilo, polisi walizidiwa nguvu kutokana na kituo hicho kutokuwa na silaha hata moja wala mabomu ya machozi.
ZUMA LAIVU
Picha za rais wa Afrika Kusini mwenye ndoa tano mpaka sasa, Jacob Zuma, zinazomuonesha ‘akidendeka’ na mtalaka wa rais Mstaafu, Mzee Nelson Mandela, Winnie Mandela, zimesambaa katika mitandao mbalimbali, Ijumaa limegundua.
Winnie na Zuma walinaswa na mapaparazi wakiwa wamekumbatiana huku midomo yao ikiwa imegusana kitendo kilichotafsiriwa kwamba, walikuwa ‘wakidendeka’.
Tukio hilo la ajabu kwa baadhi ya mila, desturi na tamaduni za Kiafrika, lilijiri wakati wa sherehe za kumpongeza ‘mnene’ huyo wa nchi kuingia madarakani miaka miwili iliyopita.
Licha ya picha hizo kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali bila kuwahusisha wawili hao na mdudu wa mapenzi, wachangiaji wengi wa maoni wamekuwa wakitatizwa na denda hilo.“Nothing to hide” (hakuna cha kuficha) alisema mchangiaji mmoja alipotoa maoni yake katika moja ya mtandao ulioweka picha hizo.
“Kifupi picha hizi ni za kimahaba zaidi na kwa maadili ya kiongozi wa kiafrika si nzuri, inawezekana kwao kufanya vile si vibaya, lakini kwetu na nchi nyingi za kiafrika zinaashiria kitu kibaya,” alisema mmoja wa wasomaji wa mitandao.
Habari zaidi zinasema kwamba, wakati wa kampeni za kuwania uongozi wa nchi hiyo, Winnie, mwanamke mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini humo, alikuwa kambi ya Chama cha African National Congress (ANC) ambayo ilimuweka Zuma kuwa mgombea urais.
Rais Zuma amewahi kulaumiwa na baadhi ya watu wa nchi yake kutokana na tabia yake ya kupenda mahaba hasa baada ya ile skendo mbaya ya kudaiwa ‘kujirusha’ na mdada mmoja ambaye anatajwa kuwa ana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.Mara baada ya kuisawazisha skendo hiyo kisheria, Zuma alijikuta akitengeneza vichwa vingi vya habari pale alipofunga ndoa na kimwana mmoja, hivyo kuongeza idadi ya wake alionao, kutoka wanne hadi watano, licha ya mmoja kufa kwa kujinyonga na mwingine kutengana naye.
Hata hivyo, licha ya kiongozi huyo mwenye makeke mengi kuwa na wake wengi, bado ni kipenzi cha raia wake ambao wengi wanachukulia ndoa hizo kuwa ni kitu cha kawaida kikisimamiwa na mwongozo wa utamaduni wa kabila lake.
Hivi karibuni, kiongozi huyo wa taifa kubwa barani Afrika alikwenda kwenye kituo kimoja cha afya na kupima ‘ngoma’ lakini majibu yalitoka ‘HANA’ hali iliyomfurahisha sana ambapo hakusita kuonesha furaha yake.
Kwa upande wake, Mama Winnie Mandela naye aliwahi kupata skendo ya kudaiwa kutembea na kijana mmoja wakati mumewe (wakati huo) Mzee Nelson Madiba Mandela akiwa jela.
Kashfa hiyo ndiyo ilisababisha aachike na kiongozi huyo mstaafu mara baada ya mambo kuwa hadharani.
Thursday, May 27, 2010
Mliochoka Kuendesha Barabarani mjiandae kupaa!!
Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Tukae mkao wa kula, wanasayansi wanazidi kufanya mambo yao, sasa wanatuletea magari yanayopaa a.k.a Flying Cars. Usipate tabu kuunga foleni pale ubungo, wewe washa Engine yako ya ndege kisha ruka mwezini kama njiwa, au siyo!!
Magari hayo bado yanakaguliwa, endapo kila kitu kitakwenda sawa, yataruhusiwa kwenda angani mwaka 2012.
Microsoft Yapigwa Overtake na Apple!!
Apple a.k.a The new King of technology ambao ni watengenezaji wa Ipod, Iphone, Ipad na kadhalika hapo majuzi walitangazwa kuwa vinara katika sekta ya teknlojia ya kisasa hivyo kuifanya Microsoft inayomilikiwa na Bilionea Bill Gates kupigwa na butwaa huku ikitupwa chini na kushushwa hadi nafasi ya pili.
Habari ndio hiyo!
K’sher akacha camera za mapaparazzi Club!!
Msanii peke wa kike toka kundi la Tip Top Connection Khadija Shaaban a.k.a K'sher amedai kitendo cha kukataa kupigwa picha na paparazi siku za hivi karibuni bila ridhaa yake ni uamuzi wake mwenyewe. K'Sher aliyasema hayo baada ya mvutano uliotokea wiki chache za nyuma baina yake na wapiga picha wa magazeti tofauti nchini katika Club ya Sansiro iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
K’Sher aliyasema hayo baada ya mvutano uliotokea wiki chache za nyuma baina yake na wapiga picha wa magazeti tofauti nchini katika Club ya Sansiro iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
“Unajuwa unapotoka usiku huwa unavaa mavazi ya usiku zaidi ukiwa unaenda sehemu kama club, sasa siku ile pale Sun Cirro nilikuwa nimevaa aina hiyo ya mavazi ya Club na sikupendezwa kuonekana katika hali ile mbele ya jamii kwani haipendezi” alisema K’Sher
Zaidi aliongeza “Mimi ni kioo cha jamii, ninapopigwa picha nikiwa na mavazi ya Club sidhani kama ni maadili kwa picha hizo kusambaa magazetini kwani nipo katika sehemu ya burudani yangu na si kwa ajili ya kupigwa picha” alisema K’Sher
“Najua wapo kazini, wanaponipiga picha nikiwa jukwaani sikatai lakini katika sehemu za burudani ya mtu binafsi wanamvurugia mtu uhuru wake na si vema hata kidogo” alimaliza.
250 Ya Nauli yataka Kumtoa Roho
Kijana mmoja mtanashati a.k.a brotherman wa nguvu, leo amegombaniwa kama mpira wa kona baada ya kushindwa kulipa nauli ya Sh. 250 tu, kwenye Dalalada linalofanya safari zake kati ya Tandika na Mwenge Jijini Dar es Salaam. Tozi huyo ambaye alilipuka viwalo vya maana...
Tozi huyo ambaye alilipuka viwalo vya maana alijaribu kutaka kushuka katika kituo cha mabasi Karume Ilala, lakini aliwekewa ngumu na kondakta na kurejeshwa ndani ya basi kwa nguvu kisha kupelekwa hadi Mwenge na kuachwa kituoni ili atafute usafiri wa kurudia.
Maimamu wamkana dogo aliyetaka kulipua UBALOZI!
Shura ya Maimamu Tanzania, imekanusha taarifa kwamba yule dogo anayetuhumiwa kwa jaribio la ulipuaji wa Ubalozi wa Marekani nchini, alihamasishwa na mawaidha ya shehe wa msikiti wa Mtambani.
Aidha, imesema taarifa hiyo ilikuzwa kwa lengo la kuipaka matope shule ya msingi Mtambani ambayo mwaka jana ilitoa mwanafunzi bora wa somo la Sayansi katika mtihani wa Taifa wa darasa la saba.
Katibu Mkuu wa Shura hiyo, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema jana kwamba shule hiyo haina rekodi inayoonesha kwamba mtuhumiwa huyo, mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Biafra, Nassib Mpamka (15) aliwahi kufika hapo.
“Tukio hilo limepangwa kuharibu sifa nzuri ya shule ya Mtambani, kwani imepata mafanikio ya kitaaluma,” alisema.
Alipotakiwa kuzungumzia jaribio la kulipua Ubalozi wa Marekani, alikataa kuzungumzia chochote akidai kuwa suala hilo halijatolewa uamuzi na mahakama.
“Waislamu ni watu wazuri na wanapenda amani, lakini maadui zetu wanawafanya waonekane magaidi ili kutimiza malengo yao mabaya,” alisema.
Alisema Shura ya Maimamu imepanga kuandamana ili kusafisha picha mbaya iliyoenea kuwa walimu wa shule ya msingi Mtambani wanahusika na jaribio la kulipua Ubalozi wa Marekani.
“Inawezekana tukio hili limetungwa, ili kuwafanya Waislamu wasiuangalie Uchaguzi Mkuu ujao,” alisema.
Mei 16 mwaka huu saa 2.30 usiku, inadaiwa Nassib alifika katika ubalozi huo eneo la kuegesha magari na kurusha chupa iliyokuwa na mafuta ya taa na utambi kwa lengo la kulipua magari hayo.
Mwanafunzi huyo baada ya kuhojiwa na Polisi, alidai kuwa alihamasishwa na mahubiri ya shehe wa Msikiti wa Mtambani kuhusu majeshi ya Marekani kuua Waislamu duniani.
Denti afia kwenye gari aliloiba!
Matukio ya madenti wa skonga za sekondari mkoani Arusha kujihusisha na matukio ya ujambazi, yameendelea kuliandama jiji hilo ambalo linaaminika kuwa ndio 'Geneva ya Africa' baada ya denti wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Makumira, Skadi Athumani (21) kupata ajali mbaya na kufa akiwa mwendo kasi ndani ya gari aliloliiba.
Tukio hilo lililotokea eneo la Community House, Kia usiku wa May 23 limethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Kilimanjaro, Hilda Kinabo.
Inaelezwa kuwa denti huyo aliiba gari lenye namba za usajili T 753 AVY aina ya Toyota Mark II, mali ya Albert Mgambila....aliyekuwa ameliegesha nyumbani kwake baada ya kutoka kazini.
Taarifa zaidi zinaendelea kudodesa kuwa..denti huyo (Athumani) alitumia funguo za bandia kupora gari hilo, wakati mwenye gari akiwa amepumzika ndani na kuondoka nalo kwa mwendo wa kasi.
Mara ya baada ya kuondoka eneo hilo kwa kasi ya ajabu, alipofika umbali wa kilometa moja na nusu eneo la National karibu na shule ya msingi Asanta, alishindwa kulimudu na kupamia mti na yeye kufa papo hapo.
Wednesday, May 26, 2010
Brazil inakuja kucheza na Taifa stars, TFF yathibitisha!
Shirikisho la soka nchini TFF limethibitisha ujio wa timu ya taifa ya BRAZIL kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya TANZANIA TAIFA STARS kabla ya kwenda Afrika Kusini.
Rais wa TFF LEODGAR TENGA amesema kuwa Tanzania imepokea kwa furaha ombi la nchi ya Brazil hivyo kwa sasa mazungumzo bado yanaendelea kuhusiana na ujio wa timu hiyo
Aidha Tenga amesema kuwa ujio wa Brazil unahitaji maandalizi makubwa hivyo juhudi kubwa inafanyika ili serikali itoe msaada mkubwa kwa ujio wa timu hiyo namba moja katika viwango vya soka Duniani.
Brazil itacheza michezo ya kirafiki na TANZANIA pamoja na ZIMBABWE, kabla ya kwenda nchini AFRIKA KUSINI kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia.
michezo hiyo itachezwa June 2 na 7 kabla ya BRAZIL haijacheza mchezo wake wa kwanza wa fainali za kombe la dunia dhidi ya KOREA KASKAZINI june 15.
Hivi sasa BRAZIL ipo nchini mwake katika jiji la CURITIBA lilipo kaskazini mwa nchi hiyo wakiendelea na mazoezi
Tanesco yapata Mrithi wa Dk. Rashid
Kile kiti cha moto cha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kilichokuwa wazi baada ya Dk. Idris Rashid kumaliza muda wake tangu Novemba mwaka jana, kimepata mrithi.
Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco imemteua Mhandisi, William Geofrey Mhando, kuchukua nafasi hiyo. Uteuzi huo unaanza rasmi Juni mosi mwaka huu.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Tanesco jana, ilisema kuwa kabla ya hapo uteuzi huo, Mhando alikuwa ni Meneja Mkuu Usambazaji Umeme na Masoko katika shirika hilo lenye dhima ya kuzalisha na kusambaza umeme nchini.
Tangu Novemba mwaka jana Dk. Rashid baada ya kumaliza muda wake wa mkataba alikabidhi ofisi pamoja na nyumba ya Tanesco aliyokuwa akikaa na nafasi hiyo ilikuwa ikikaimu, Stephen Mabada.
Mhando aliajiriwa na Tanesco Oktoba 1987 kama mhandisi wa umeme, kabla ya kupanda cheo kuwa Mhandisi katika laini za umeme.
Mwaka 1990 hadi 1992 aliteuliwa kuwa Meneja wa Tanesco mkoa wa Singida na baadaye mwaka huo hadi 1994 alihamishiwa katika mkoa wa Mbeya kuwa Meneja wa mkoa wa Mbeya.
Vilevile Injinia Mhando alipandishwa cheo mwaka 1995 kuwa Mkurugenzi wa kanda ya Kusini Magharibi hadi mwaka 1999.
Taarifa hiyo imesema kuwa Mhandisi Mhando ana shahada ya uzamili ya umeme aliyoipata Havana, Cuba mwaka 1987, vile vile ana elimu aliyoipata katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Mhando anachukua nafasi iliyoachwa na Dk. Rashid ambaye aliingia Tanesco akiwa anatokea sekta binafsi alikokuwa akifanya kazi baada ya kuwa gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakati wa utawala wa awamu ya pili na tatu mwanzoni.
Tuesday, May 25, 2010
Sasa binadamu wa kutengenezwa waja!
Mabingwa wa mambo afya chini ya ardhi ya Uncle Obama (Marekani) kwa mara ya kwanza tangu zama za Adam na Hawa wamefanikiwa kuunda seli hai (living cell) kwa kutumia vinasaba vilivyotengenezwa na binadamu(manmade DNA) iliyounganishwa na vitu mbalimbali.
Hali hiyo ambayo inatafsiriwa na wengi kuwa ni mwanzo wa utengenezaji wa uhai bandia..imeshazua mijadala chungu tele duniani hasa baada ya tamko la mabingwa hao.
Habari zaidi zinasema kuwa katika ugunduzi huo wataalamu hao waliunda programu ya vinasaba na kuvipandikiza ndani ya seli pokezi.
Ilielezwa kuwa baada ya hatua hiyo matokeo yake yakazaa vijiumbe maradhi vinavyofuata nyenzo ileile ya DNA iliyounganishwa.
Ugunduzi huo uliochapishwa katika jarida maarufu liitwalo 'science', umeshangiliwa na ulimwengu wa sayansi kama hatua kubwa, ingawa wakosoaji wanasema viumbe sanisia vinaweza kusababisha madhara yasiyoelezeka huku wengine wakisema kuwa manufaa ya teknolojia hii yametiwa chumvi.
Hata hivyo wataalamu hao wanasema kuwa wana nia ya kuunda seli za bakteria hiyo ambayo itasaidia katika utengenezaji wa dawa, mafuta na kumeza gesi zinazochafua mazingira.
Magari ya JK ni mikweche au ya kichinaaaa???
Ziara ya mkuu wa nchi aliyoifanya jana mkoani Dsm iliingia kizungumkuti baada ya gari alilotumia kwenye msafara wake kuzimika ghafla mara mbili barabarani.
Gari hilo lilizimika kwa mara ya kwanza katika makutano ya barabara ya Morogoro na Mavurunza wilayani Kinondoni eneo la Kimara Mwisho majira ya saa 7:30 mchana ambako msafara wake ulisimama kwa dakika tatu.
Gari hilo lilizimika tena kama hatua 150 tu kutoka katika makutano hayo na ndipo rais akahamishiwa kwenye gari lingine lililokuwa kwenye msafara huo huku akiwa ananyeshewa mvua.
Tena majira ya saa 10:00 jioni msafara wake uliokuwa ukitokea Keko Toroli wilayani Temeke, ulikwama tena maeneo ya BP barabara ya Kilwa ambako gari hilo jipya nalo lilizimika ghafla.
Tukio hilo la kihistoria nchini, liliwapa wakati mgumu maafisa usalama ambao kila mara gari lilipokuwa limezimika, walishuka kwenye magari yao na kuondoa bendera na ngao.
Kusimama gafla kwa msafara wake eneo la Kimara, kulimlazimisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya kukimbilia eneo alilokuwapo rais huku umati wa watu uliokuwa umejibanza pembeni mwa barabara nao ukisogea karibu.
Ilimchukua takriban dakika mbili kwa maafisa wa usalama wa taifa kupata suluhu ya namna msafara huo utakavyoendelea kutokana na mkanganyiko wa gari ipi kati ya mbili zilizokuwa zinafanana aiangie rais.
Msafara huo uliendelea baada ya Rais Kikwete ambaye alikuwa amevaa shati la kitenge la mikono mirefu na akiwa analowa hasa miguuni kuhamishiwa katika gari jingine huku lile lililoharibika likiwa linasukumwa na umati wa watu hadi pembezoni mwa barabara.
Hata hivyo, baada ya dakika nane gari hilo aina ya Toyota Landcruiser VX V8 lililokuwa na rangi nyeusi, liliwaka baada ya dereva kujaribu kuliwasha kwa zaidi ya mara nne.
Kuzimika kwa gari lake eneo la PB kulifanya msafara wa rais usimame kwa takriban dakika kumi kabla ya kuendelea.
LIYUMBA AHUKUMIWA KWENDA JELA!!!
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imesoma Hukumu dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba,Katika hukumu hiyo Liyumba amepatikana na hatia ya utumiaji mbaya wa madaraka .
Awali Liyumba alifikishwa mahakamani hapo akiwa pamoja na aliyekuwa meneja miradi wa BoT Deogratius Kweka, ambapo kwa pamoja walikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo, jambo lililopelekea serikali kupata hasala ya sh bilioni 221, kupitia ujenzi wa majengo pacha ya BoT.
Hata hivyo kabla ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka, upande wa mashtaka ulimuachia aliyekuwa mshtakiwa mwenza wa Liyumba {Kweka}, na kumshitaki Liyumba kwa kesi hiyo.
Baada ya ushahidi huo kumalika kusikilizwa, Mahakama ilifikia uamuzi wa kumfutia Liyumba shtaka la kuisababishia serikali hasara ya bilioni 221 baada ya Upande huo wa serikali kupitia ushahidi na vielelezo vyake kushindwa kuithibitishia mahakama hiyo kama Liyumba alihusika na kosa hilo.Kufuatia uamuzi huo, mahakama ilimtaka Liyumba kujitetea juu ya uhusika wake katika shtaka la kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo.
Katika utetezi wake Liyumba alijitetea mwenyewe kama shahidi wa kwanza kutoka upande wa utetezi, na baadae alimwiita shahidi wa pili ambaye ni Bosco Ndimbo Kimela, aliyekuwa katibu wa BoT.
Matokeo ya Hukumu hiyo dhidi ya Amatus Liyumba yamekamilika leo tarehe 24 May kama ilivyopangwa kusomwa mahakamani hapo na kuamua kufungwa jela kwa Mda wa miaka 2,hivi sasa Liyumba atatumikia kifungo cha miaka 2 kwa kosa la utumiaji mbaya wa madaraka katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) akiwa kama Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
JK Ahutubua Bunge La Afrika Mashariki Leo Nairobi.
Rais Jakaya Kikwete(Katikati) Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Abdirahin Abdi(kushoto) na Spika wa Bunge la Kenya Kenneth Marende(kulia) wakiwa katika viwanja vya Bunge la Kenya Muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili na kupigiwa wimbo wa taifa ambapo baadaye Rais Kikwete alilihutubia bunge la jumuiya hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia bunge la jumuiya hiyo jijini Nairobi leo asubuhi.
Maeneo mengi Dar kukosa umeme siku za Jumapili.!!!
Shirika la Umeme nchini (Tanesco), limetangaza kuzima umeme katika sehemu nyingi za jiji la Dar es Salaam kwa saa nne mfululizo, katika siku za Jumapili, kuanzia Jumapili ya wiki hii.
Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, umeme utazimwa katika sehemu hizo kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 6:00 mchana kwa sababu za kiusalama ili kuruhusu kazi kufanyika katika njia ya umeme ya msongo wa Kilo Volti 132 katika laini ya Makumbusho kutoka kituo cha kupokelea umeme cha Ubungo.
“Sehemu nyingi za Jiji la Dar es Salaam zitaathirika na katizo hili la umeme. Umeme utazimwa kwa sababu za kiusalama ili kuruhusu kazi hii kufanyika,” alisema Badra.
Baadhi ya maeneo yatakayoathirika na katizo hilo la umeme ni TBS, Ubungo Bus Terminal, Ubungo NHC, Ubungo Filling Station, Tanesco Staff Quarters, nyumba za wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu, TTCL Flats, Sinza Ukuta wa Posta, NBC Ubungo, Chibuku, Ubungo Portland Cement, Ubungo Flats, Urafiki Flats, Kituo cha Polisi Urafiki, Rombo Green View Hotel, Legho Hotel, Sinza Mugabe, Sinza Madukani, Rubada, UDSM Hostel na Millenium Business.
Mengine ni Ubungo Maziwa, Ubungo Kisiwani, Ubungo Container Terminal, Kiwanda cha Maziwa, TTCL Exchange, Chuo cha Usafirishaji (NIT), UFI, Ubungo Spinning, Mabibo Sahara, W-Bar, TGNP, Ubungo Kibo (Hunters Club) Msewe Uwanjani, Msewe Shuleni, Msewe Golani, Changanyikeni, Chuo cha Takwimu, Changanyikeni Kijijini, Changanyikeni Jeshini, Makongo Juu KKKT, Makongo Juu Kanisa Katoliki, Goba Kunguru, Wazo na Madale.
Kwa mujibu wa Badra, kazi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha Makumbusho na kwamba, kukamilisha kwa kituo hicho, kutasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika katika Jiji la Dar es Salaam.
Watano wa familia moja wateketea kwa moto!!!
WATU watano wa familia moja wamepoteza maisha baada ya nyumba yao kuteketezwa kwa moto unaodaiwa kuwashwa kutokana na ugomvi wa mapenzi uliomhusisha mmoja wa wanafamilia hao.
Walioteketea kwa moto wakiwa katika nyumba yao yenye chumba kimoja ni baba mwenye nyumba, John Onesmo (32) ambaye ni mfanyabiashara wa samaki eneo la Feri, Catherine John (25) anayefanya biashara ndogondogo, watoto wao Oliver (2) na Joyce John (5) na Esther Amos (20) ambaye ni mdogo wa Catherine.
Tukio hilo lilitokea saa 6 usiku wa kuamkia jana, baada ya mchumba wa Esther ambaye ni mlinzi wa shule ya sekondari Aboud Jumbe, Shemsa Mpelela (22), kutuhumiwa kuchoma moto nyumba hiyo kwa kutumia petroli.
Majirani ambao hawakupenda majina kutaja majina yao kwa sababu za kiusalama, walidai jana kuwa wakiwa wamelala walisikia mlipuko na kudhani pikipiki imepasuka tairi au mlio wa risasi na walipoamka waliona mwanga mkali na kugundua kuwa nyumba ya John ilikuwa ikiungua moto.
“Niliposikia mlio nilidhani pikipiki imelipuka, kumbe nadhani kichwa cha mtu kilipasuka na kusikia sauti mara moja ya mwanamke ikilia ‘mama nisaidie’, nilimwamsha mume wangu na alipotoka nje aliona nyumba ya John ikiungua … watu walikwenda kusaidia na kujaribu kuvunja mlango kwa jiwe, lakini ilishindikana na moto ulishashika kasi hauzimiki. Sehemu yote ile ilikuwa ikinuka petroli,” alielezea jirani mmoja.
Walisema walitoa taarifa Polisi na askari waliwahi kufika eneo la tukio, lakini Zimamoto walichelewa kwani walipotea njia na walipokaribia eneo la tukio gari lilikwamba kutokana na ubovu wa barabara.
Baada ya polisi kufika na moto kuzimwa, John alikutwa amekumbatia watoto wake kitandani na miili hiyo ikapelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Vijibweni.
Jamani Kikwete na Ridhiwani Wasihusishwe na Kujiuzulu kwangu!
Pichani ni katibu mkuu wa UVCCM Taifa Bw.Martine Shigella (kulia) katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa akizungumzia kuhusu sakata la kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Hamad Yusuph Masauni , kulia kwake ni katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi Taifa Estar Bulaya.
BAADA ya sakata la kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UV-CCM) Hamad Yusuph Masauni kuzidi kuchukua sura mpya na baadhi ya makundi ya vijana kumhusisha mtoto wa mwenyekiti wa CCM Taifa Ridhiwan Kikwete na mwenyekiti mwenyewe kuwa wanahusika katika kumwondoa Masauni katika nafasi hiyo ,utata zaidi umezidi kuibuka katika sakata hilo baada ya katibu mkuu wa UV-CCM Taifa Martine Shigella kwa mara ya kwanza kujitokeza mbele vyombo vya habari kutolea ufafanuzi juu ya mwenendo mzima wa sakata hilo na kudai kuwa Rais Kikwete na Ridhiwani wasihusishwe katika sakata hilo ambalo mhusika mkuu ni yeye mwenyewe Masauni na si mtu mwingine.
Asema mkakati wa UV-CCM ni kukiomba chama cha mapinduzi kumpitisha Rais Kikwete kuwa mgombea pekee katika uchaguzi mkuu na wanaomhusisha yeye na mtoto wake Ridhiwani na tuhuma za kumwondoa Masauni ni vizuri wakapeleka ushahidi kwake ili kuwajibishwa vinginevyo hawatamwajibisha kwa maneno ya mitaani.
“…Hatuwezi kumwondoa Ridhiwani kwa tetesi za mitaani na kama yupo mtu mwenye ushahidi wa tuhuma zake kuuvuruga umoja huo apeleke kwake ili hatua zichukuliwe ila vinginevyo itakuwa ngumu kumwajibisha”
Pia katibu huyo amesema kuwa pamoja na kuwepo na watu wanaohusisha sakata hilo na mbio za uchaguzi mkuu huko Zanzibar ni kutomtendea haki kwani hata katika maelezo yake na yale ya mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Kikwete hajapata kuzungumzia hilo.
Alisema kuwa yapo maneno kuwa tuhuma za Masauni zimetoka Zanzibar ambako kuna mwanamke ambaye mume wake anataka kugombea nafasi ya juu ya uongozi huko aliondolewa katika nafasi ya uongozi ndani ya UV-CCM kutokana na fitina za Masauni jambo ambalo halina ukweli kwani hakuna kiongozi wa UV-CCM Zanzibar aliyeenguliwa nafasi yake toka Masauni achaguliwe katika nafasi hiyo.
Monday, May 24, 2010
Navaa vimini kuongeza mvuto!
Mwite Jide,Lady Jaydee au 'Manka' kama anavyopenda ajulikane siku hizi..ameweka bayana kwamba anapendelea zaidi kuvaa vimini ili kuongeza mvuto na kusisimua mashabiki wake anapokuwa jukwaani.
Lakini hakuishia hapo msanii huyo ameliambia gazeti moja maarufu la nchini Kenya kuwa hapendi kurudia nguo kwa vile anawaogopa mapaparazi.
"Napenda kuvaa nguo fupi kwenye maonyesho na viatu virefu. Nywele zangu pia nazibadili kwa mitindo tofauti kila siku," alisisitiza msanii huyo anayemiliki Machozi Band inayotamba Dar es Salaam.
"Kinachonifanya nionekana tofauti na wasanii wenzangu ni kwamba ninajituma sana na ninapenda sana kutengeneza nywele zangu, ni nadra sana kunikuta kwenye staili moja ya nywele wiki mbili nzima."
"Kujirefusha huwa navaa viatu virefu wakati ninapokuwa jukwaani na magauni au sketi fupi ili miguu ionekane mirefu. Napenda sana staili za mitaa."
Ray C atest zali la Movie !
Mwanadada Ray C ambaye anatambulika zaidi kwenye fani ua muziki na kupachikwa jina la kiuno bila mfupa, amekuja huku
Ray C amecheza filamu iliyopewa jina la beautiful iliyoandaliwa na muongozaji Tuesday Kihangala
Filamu hiyo imechezewa mjini Morogoro na Tuesday amemfagilia saana Ray C amekamua vilivyo.
Je Ray C atahamia huko baada mambo yake kwenye muziki kwenda kombo?
Dada Irene Uwoya na Mumewe!!
Ni ndani ya Ukumbi wa bilicanas jijini Dar es Salam akiwa sambamba na Mumuwe Hamad Ndikumana wanayeishi nae nchini Cyprus.
Picha hii inanoga zaidi baada ya muigizaji huyo maarufu wa filamu Irene Uwoya kuzushiwa kuwa ndoa yake imefikia tamati kutokana naye kuwepo nchini kwa muda
Irene alikuwa nchini kwa ajili ya kuigiza filamu ya kampuni ya RJ iliyopewa jina la My Dream ambayo inafanya vyema sokoni
Jamani, Maunda Zorro si Ulee mtoto kwanza!!
Huku kichanga chake kikiwa na takribani miezi mitatu tangu kilipoingia duniani, Bongo fleva Diva, Maunda Zorro, amezua viulizo na kutoa ‘chansi’ kwa wadau wa burudani nchini kumpa ushauri wa bure wakimtaka atulie nyumbani na kulea mtoto.
Jamaa hao walifikia hatua hiyo baada ya Maunda kuonekana akijirusha ile mbaya ndani ya klabu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar wiki iliyopita kwenye ‘afta pati’ ya tuzo za Kili.
Wadau hao waliamua kumtolea uvivu walidai kwamba, ni mapema mno kwa Maunda kujiachia na kwamba mtoto alimwachia nani hivyo kumtaka atulie nyumbani ili kulea mtoto hadi atakapofikia ‘eji’ ya kufanya hivyo.
“Hebu muone Maunda anavyojiachia, mtoto atakuwa amemwachia nani? Maunda anatakiwa atulie nyumbani alee mtoto hadi akiwa na umri wa kumwacha ndiyo afanye haya anayoyafanya,” alisema mmoja wa wadau hao.
Eritrea yalambishwa Bao 8-1 na Twiga Stars
Timu ya Wanawake ya Twiga Stars imeibuka kidedea baada ya kuichapa Timu ya Wanawake ya Eritrea bao 8-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Mechi hiyo ilikuwa ni kivutio sana kutokana na kwamba haijawahi kutokea hapa nchini kwa Timu ya Wanawake kuweza kufungua mabao mengi kama ya leo.
Twiga Stars imefainikiwa kuvuka kipenga hicho na kujiwekea nafasi ya kwenda Bondeni Afrika ya Kusini kwa Mzee Madiba kushiriki mashindano ya nusu fainali za kombe la dunia kwa mataifa ya Afrika endapo tu watafanikiwa kulitetea taji hilo katika mechi ya marudiano na Timu ya Eritrea.
Sunday, May 23, 2010
Makamba akana kuingilia sakata la UV CCM!
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Yusuf Rajabu Makamba, amepinga vikali kuhusika katika kumlazimisha kujiuzulu aliyekuwa Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Hamad Massauni, na kusema Masauni aliwajibika mwenyewe.
Makamba amesema baada ya kupata uvumi kuwa mwenyekiti huyo aligombea uongozi akiwa hana vigezo kutokana na umri wake kuzidi, walifanya uchunguzi na kuthibitisha kuwa tayari alishatimiza miaka 35 wakati anagombea.
Amesema alichokifanya ni kujadiliana naye tu kuhusu suala hilo na kwamba hakumlazimisha kujiuzulu.
Mimi nilimwambia kama umekosa kalale, ufikirie na upime mwenyewe kwa kosa hilo; na asubuhi akarudi na kusema nimejiuzulu, ameeleza Makamba.
Taarifa hiyo imekuja baada ya wadau wengi kumhusisha Makamba na sakata hilo kwa kudai kuwa alimshinikiza kiongozi huyo wa vijana kuachia ngazi.
Meya jiji la Mwanza mbaroni kwa mauaji!!
Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Leonard Bihondo, leo amesomewa shitaka la mauaji ya Katibu wa CCM ngazi ya Kata, katika mahakama ya mwanzo ya Kata ya Isamilo mkoani Mwanza, sambamba na watuhumiwa wengine watatu.
Akifafanua kiini cha mkasa huo, Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza SAPC Simon Sirro amesema mtuhumiwa Leonard Bihondo na wenzake Jumanne Oscar, Baltazari Shushi na Abdulah Hausi walimuua Bahati Stephan katibu wa CCM Kata ya Isamilo Mei 14 mwaka huu, kwa kumchoma kisu akiwa ofisini kwake.
Katika shauri hilo linalosimamiwa na wakili wa Serikali Stephen Kakwega, watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote, kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kuendesha kesi hiyo na wamerudishwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena.
Hili ni mojawapo ya matukio makubwa matatu nchini kwa viongozi wakubwa wa Serikali kujihusisha na mauaji ya raia, ambapo licha ya kesi iliyokuwa ikimhusu kamanda Abdalah Zombe aliyeshutumiwa kuwaua Wafanyabiashara kwa kisingizio cha ujambazi,
kadhalika miaka ya hivi karibuni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kigoma marehemu Kapteni Ditopile Ukiwaona Mzuzuri alifikishwa mahakamani kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua dereva wa daladala katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam.
Kapteni Mzuzuri alifariki baadaye tarehe 20 April 2008 kwa kuugua ghafla akiwa hotelini na mkwewe mjini Morogoro, wakati kesi ilipokuwa ikiendelea.
Mrisho Ngassa na Jackson Njovu rasmi ndani ya Azam FC!!
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa wachezaji hao wapya Mwenekiti wa Azam Fc, Said Muhammad Said alisema kuwa baada ya kuwapata wachezaji hao lengo la klabu hiyo ambalo ni kuchukua Ubingwa wa ligi Kuu ya Vodacom katika msimu ujao.alisema “Wachezaji wazuri tunao hatuna sababu ya kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2010-2011″.
Nae mchezaji mpya wa timu hiyo,Mrisho Ngasa ambaye amehamishwa kwa kitita cha sh milioni 58, alisema “Nitahakikisha timu yangu mpya inafanya vizuri katika msimu ujao wa ligi kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu,Najua kuna kila aina ya ushindani huko niendako lakini nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kiwango changu hakishuki na kuipatia Ubingwa wa Ligi Luu ya msimu ujao timu yangu mpya”. aliongeza Ngasa.
Naye golikipa mpya wa timu hiyo aliyehamishwa kwa kitita cha shilingi milioni tatu kutoka JKT Ruvu, Jackson Chove alisema kuwa,baada ya kukosa kusajiliwa na timu hiyo katika msimu uliopita sasa amefika katika timu ambayo alikuwa anaipenda kutokana na kuwa na mapenzi na klabu hiyo tajiri hapa Tanzania. “Najua kama kuna ushindani mkubwa katika timu yetu lakini nitahakikisha nafanya mazoezi na kuongeza juhudi zaidi ili kiwango changu kisishuke” alisema Chove.
Saturday, May 22, 2010
Hukumu ya Liyumba Kusomwa Jumatatu!
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam itatoa hukumu ya kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Benki Kuu Tanzania (BoT), Amatus Liyumba siku ya jumatatu tarehe 24.
Liyumba kwa sasa anakabiliwa na shitaka moja la kudaiwa kutumia vibaya ofisi ya umma. Awali alishitakiwa pia kwa kudaiwa kuisababisha hasara ya Sh bilioni 221,upande wa mashitaka ulishindwa kudhibitisha shitaka hilo, likafutwa.
Liyumba alidai kuwa yeye hakuwa na mamlaka ya kuidhinisha mradi huo na kwamba, aliyekuwa Gavana kwa wakati huo, Daudi Ballali, ndiye aliyekuwa na mamlaka yote.
Katika ushahidi huo, Liyumba pia ameieleza mahakama kuwa,ingawa mradi huo ulikuwa chini ya kurugenzi yake, hakuwa anahusika kushughulika na mradi huo ingawa mara kadhaa alijibu barua zinazohusiana na mradi kwa maelekezo ya Gavana.
Mama Salma ashiriki katika Mjadala wa wanawake-Beijing!
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alihutubia mkutano wa wanawake wa dunia katika kuelezea mafanikio aliyoyapata katika taasisi yake ya wanawake na maendeleo (WAMA) na juhudi zake binafsi za kusaidia ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.
Mama Kikwete ambae ametajwa kuwa mfano bora kwa wake wa marais wa Afrika kufuatia taasisi yake ya WAMA kujikita zaidi katika kusaidia jamii na hasa jitihada zake binafsi za kusaidia wanawake,afya, na watoto wanaoishio katika mazingira hatarishi.
Akijibu maswali kwa kujiamini , Mama Kikwete Kiwete alisema madhumuni makubwa ya kuanzishwa kwa WAMA ni kumuendeleza mwanamke kielimu, kiafya na kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na wale wanaishi katika mazingira hatarishi.
Alisema kuwa vitu vingi amekuwa akifanya kupitia taasisi yake ya WAMA kusaidia wanawake wa Kitanzania ikiwemo suala la elimu kwa kuwa ndiyo njia pekee ambayo inaweza kumkwamua mwanamke katika maisha ya chini na hili amekuwa ameanza kwa wasichana wadogo kuwasisitiza umuhimu wa elimu na kujiepusha na mimba za utotoni na hususan swala la kujiepusha na ugongwa wa ukimwi.
Friday, May 21, 2010
Njama ya Al Qaeda kufanya Ugaidi Kombe la Dunia Yafichuliwa!
Pichani ni Abdullah Azam Saleh al-Qahtani anayedaiwa kuwa mfuasi wa al-Qaeda aliyetiwa kizuizini Iraq ambapo ametoa maelezo juu ya mpango wa kutaka kufanya shambulio Kombe la Dunia Afrika Kusini mwezi ujao.
Mtu huyo raia wa Saudi Arabia, amewaambia waandishi wa habari alipanga kushambulia timu ya Uholanzi na Denmark kwa kulipiza kisasi baada ya kuchora vibonzo vya mtume Muhammad.
Lakini amesema viongozi waandamizi wa al-Qaeda bado hawakuidhinisha mpango huo.
Aliendelea kwa kusema "Kama tusingeweza kufikia timu zao, basi tungewalenga mashabiki wao."
Mpango huo ungehusisha mabomu ya magari na mashambulio kwa kutumia bunduki.
Subscribe to:
Posts (Atom)