Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, May 18, 2010

Neno La Leo: Heri Niwe Na Chongo, Jirani Awe Kipofu!Kuna kisa cha bwana aliyemwomba sana Mungu amsaidie. Siku moja akaambiwa; sala zako zimeshasikilizwa, isipokuwa, Mungu atakusaidia kwa sharti moja; Kwamba kile atakachokupa wewe, basi, jirani yako atampa mara mbili yake. Bwana yule akahitaji muda wa kwenda kutafakari kabla hajampa Mungu jibu. Akarudi na jibu; ” E Mola wangu, naomba unipe chongo, utoboe jicho langu moja. Bwana yule alikuwa tayari awe na chongo ili jirani yake awe kipofu kabisa!
Ni katika mazingira haya, utamkuta mtu anamfanyia hila na hiyana Mtanzania mwenzake anayejitahidi kutafuta maendeleo yake kwa njia za halali tu, lakini, Mtanzania huyu mwenye roho mbaya atajitahidi kumvuta mwenzake asiende mbele kimaendeleo.Ukimwuliza; ” Kwanini uchukie maendeleo ya mwenzako anayejitafutia kipato chake kwa njia ya halali? Atakujibu; ” Mi namchukia tu huyu, akifanikiwa atajidai!
Anachoficha kusema ni ukweli kuwa anamchukia binadamu mwenzake kwa sababu ya ubinafsi na roho yake mbaya tu, kwamba hataki mandeleo ya mwenzake, basi. Na anachoshindwa kuelewa huyu anayechukia maendeleo ya mwezake ni ukweli kuwa maendeleo ya mtu huyo binafsi yatakuja kwa namna moja au nyingine kumnufaisha hata yeye. Kwanini uchukie maendeleo ya binadamu mwenzako yenye kutokana na bidii yake? Hilo ni neno la leo.

No comments:

Post a Comment