Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, May 27, 2010

Denti afia kwenye gari aliloiba!


Matukio ya madenti wa skonga za sekondari mkoani Arusha kujihusisha na matukio ya ujambazi, yameendelea kuliandama jiji hilo ambalo linaaminika kuwa ndio 'Geneva ya Africa' baada ya denti wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari ya Makumira, Skadi Athumani (21) kupata ajali mbaya na kufa akiwa mwendo kasi ndani ya gari aliloliiba.

Tukio hilo lililotokea eneo la Community House, Kia usiku wa May 23 limethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Kilimanjaro, Hilda Kinabo.

Inaelezwa kuwa denti huyo aliiba gari lenye namba za usajili T 753 AVY aina ya Toyota Mark II, mali ya Albert Mgambila....aliyekuwa ameliegesha nyumbani kwake baada ya kutoka kazini.

Taarifa zaidi zinaendelea kudodesa kuwa..denti huyo (Athumani) alitumia funguo za bandia kupora gari hilo, wakati mwenye gari akiwa amepumzika ndani na kuondoka nalo kwa mwendo wa kasi.

Mara ya baada ya kuondoka eneo hilo kwa kasi ya ajabu, alipofika umbali wa kilometa moja na nusu eneo la National karibu na shule ya msingi Asanta, alishindwa kulimudu na kupamia mti na yeye kufa papo hapo.

No comments:

Post a Comment