Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, May 29, 2010

MICHAEL ESSIEN KUZIKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA


mchezeshaji wa Timu ya Taifa ya Soka ya Ghana na klabu ya Chelsea ya Uingereza,Michael Essien(pichani), atazikosa fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Kwa mujibu wa tovuti ya Chama cha Soka cha Ghana(GFA),kiungo huyo ambaye kwa muda sasa amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti,hatoweza kupona mpaka hapo mwishoni mwa mwezi wa saba(Julai) na hivyo kumaliza kabisa matumaini ya kuweza kucheza katika fainali hizo.

Uamuzi wa mwisho wa kumuondoa Essien katika kikosi cha Ghana(Black Stars) ulifikiwa na chama hicho cha soka kwa kushauriana kwa karibu na timu yake ya Chelsea pamoja na daktari wake na pia madaktari wa Timu ya Taifa ya Ghana.

Pamoja na kwamba hatocheza,habari zinazidi kupasha kwamba Michael Essien ataambatana na timu hiyo kwenda Afrika Kusini na kwamba atasaidia katika masuala mengine ya kiufundi.Ghana wapo kundi D pamoja na Ujerumani, Australia na Serbia. Wataingia uwanjani kwa mara ya kwanza tarehe 13 Juni kupambana na Serbia.

No comments:

Post a Comment