Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, May 19, 2010

Asiyeendeleza ardhi ndani ya Miezi 6 Anyang'anywe!


Ni mkwara mpya kutoka kwa President JK kwamba..ardhi kwa ajili ya uwekezaji itatolewa kwa kuzingatia masharti na vigezo maalumu na mwekezaji akishindwa kuyatimiza atanyang’anywa na kupewa mwingine mwenye uwezo na nia, imeelezwa.

JK alisema upo mtindo wa watu wanaojiita madalali, kuhodhi ardhi yenye ukubwa wa maelfu ya hekta na baadaye huiuza kidogo kidogo kwa wawekezaji na wakati mwingine haiendelezwi, jambo ambalo linahitaji kudhibitiwa.

“Tusiache ardhi yetu mikononi mwa hawa matapeli ambao huhodhi ardhi ili waiuze kwa wawekezaji, hili si jambo jema hata kidogo, badala yake hawa watatuharibia na sisi hatutapiga hatua ya maendeleo,” alisema Kikwete.

Alisema jambo la msingi ni kwa ardhi kutolewa kwa misingi ya vigezo ili mwekezaji atakayepewa iwapo ni miezi sita bila kuendeleza eneo husika kwa sababu zisizoeleweka, anyang’anywe ili kupisha wawekezaji wenye uwezo wa kufanya hivyo.

“Kwa hili nasisitiza, kwani hata kama Sheria ya Ardhi haisemi hivyo, Mwanasheria Mkuu ibadilishwe, ipitiwe na kuboreshwa zaidi, wapo watu wana maelfu ya hekta za ardhi, lakini hawafanyi kitu, wanajinufaisha wao, ni lazima tabia hii ikomeshwe, haiwezekani wengine watakate na wengine wachujuke,” alisema.

No comments:

Post a Comment