Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, May 5, 2010

Msanii ambana mume wa mtu


Msanii chipukizi wa filamu Bongo, Lungi Maulanga, amebambwa ‘live’ akila ‘malavu’ na mume wa mtu ambaye jina halikuweza kunaswa ‘fasta’.
Tukio hilo lililoshuhudiwa kwa macho na masikio ya Risasi, lilichukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Lungi ‘Mwana Dar es Salaam Moto’ alikuwa akimpeleka puta jamaa huyo.

Katika ishu hiyo, wawili hao walikutwa wamesimama kaunta wakilamba kilaji ‘mma’, ambapo kuna muda waligeuka kero kwa majirani zao kutokana na kufanya mambo ya chumbani mahali hapo.

Hata hivyo, wawili hao wakiwa wamezama kwenye lindi la mapenzi mazito, Paparazi Wetu alifanikiwa kuwalamba picha, jambo ambalo Lungi alilishtukia na kumfuata mwandishi kisha kumcharukia akidai kuwa yeye ni mke wa mtu na huyo kijana aliyekuwa naye ni mume wa mtu pia.

“Aloo….(akimtaja jina paparazi wetu) nakuomba sana zifute hizo picha ulizopiga, hapa tunaibiana tu, yule jamaa niliyenaye ni mume wa mtu, nakuomba sana na unafahamu kabisa kuwa na mimi nina mtu wangu,” alisema Lungi ambaye kwa sasa ni mkodishaji wa bendi kubwa ambazo huzipeleka katika kumbi mbalimbali za starehe.

Wawili hao hawakuishia hapo kwani hata baada ya Lungi kuchimba mkwara kwa staili ya ‘ipotezee’, walirudiana tena na kuendeleza ‘libeneke la malavidavi’ hadi walipotosheka na kuzamia kusikojulikana.

No comments:

Post a Comment