Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Monday, May 31, 2010

Brazil kutua na makocha 27Kikosi cha timu ya Brazil kinatarajiwa kutua nchini Juni 6 mwaka huu kikitokea Zimbabwe ambapo kitaongozana na jopo la makocha 27. Rais wa TFF, Leodgar Tenga amesema katika ujumbe wa watu 60 utakaotua nchini, makocha pekee watakuwa 27 huku wachezaji wakiwa 23.

“Huu utakuwa ni ugeni mkubwa wa kwanza ukiachilia tatu zilizowahi kufika hapa nchini ambazo ni Senegal, Cameroon pamoja na Ivory Coast. Kwa sababu hiyo utaona kuwa mambo mengi yatakuwa ni tofauti na ilivyokuwa imezoeleka wakati timu nyingine zinapowasili hapa Tanzania,” alisema Tenga.

Kwa upande wake wakala wa kuandaa mechi anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Philippe Huber alisema walichagua Brazil kucheza mchezo huo dhidi ya Taifa Stars nchini Tanzania kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo ukarimu na mazingira bora ya usalama yaliyopo tofauti na mataifa mengine ya jirani na Afrika Kusini.

Brazil itawasili Juni 6, mwaka huu kisha kucheza mechi moja dhidi ya Stars Juni 7, mchezo utakaofanyika kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment