Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, May 25, 2010

Watano wa familia moja wateketea kwa moto!!!


WATU watano wa familia moja wamepoteza maisha baada ya nyumba yao kuteketezwa kwa moto unaodaiwa kuwashwa kutokana na ugomvi wa mapenzi uliomhusisha mmoja wa wanafamilia hao.

Walioteketea kwa moto wakiwa katika nyumba yao yenye chumba kimoja ni baba mwenye nyumba, John Onesmo (32) ambaye ni mfanyabiashara wa samaki eneo la Feri, Catherine John (25) anayefanya biashara ndogondogo, watoto wao Oliver (2) na Joyce John (5) na Esther Amos (20) ambaye ni mdogo wa Catherine.

Tukio hilo lilitokea saa 6 usiku wa kuamkia jana, baada ya mchumba wa Esther ambaye ni mlinzi wa shule ya sekondari Aboud Jumbe, Shemsa Mpelela (22), kutuhumiwa kuchoma moto nyumba hiyo kwa kutumia petroli.

Majirani ambao hawakupenda majina kutaja majina yao kwa sababu za kiusalama, walidai jana kuwa wakiwa wamelala walisikia mlipuko na kudhani pikipiki imepasuka tairi au mlio wa risasi na walipoamka waliona mwanga mkali na kugundua kuwa nyumba ya John ilikuwa ikiungua moto.

“Niliposikia mlio nilidhani pikipiki imelipuka, kumbe nadhani kichwa cha mtu kilipasuka na kusikia sauti mara moja ya mwanamke ikilia ‘mama nisaidie’, nilimwamsha mume wangu na alipotoka nje aliona nyumba ya John ikiungua … watu walikwenda kusaidia na kujaribu kuvunja mlango kwa jiwe, lakini ilishindikana na moto ulishashika kasi hauzimiki. Sehemu yote ile ilikuwa ikinuka petroli,” alielezea jirani mmoja.

Walisema walitoa taarifa Polisi na askari waliwahi kufika eneo la tukio, lakini Zimamoto walichelewa kwani walipotea njia na walipokaribia eneo la tukio gari lilikwamba kutokana na ubovu wa barabara.

Baada ya polisi kufika na moto kuzimwa, John alikutwa amekumbatia watoto wake kitandani na miili hiyo ikapelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Vijibweni.

No comments:

Post a Comment