Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, May 25, 2010

Maeneo mengi Dar kukosa umeme siku za Jumapili.!!!


Shirika la Umeme nchini (Tanesco), limetangaza kuzima umeme katika sehemu nyingi za jiji la Dar es Salaam kwa saa nne mfululizo, katika siku za Jumapili, kuanzia Jumapili ya wiki hii.

Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, umeme utazimwa katika sehemu hizo kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 6:00 mchana kwa sababu za kiusalama ili kuruhusu kazi kufanyika katika njia ya umeme ya msongo wa Kilo Volti 132 katika laini ya Makumbusho kutoka kituo cha kupokelea umeme cha Ubungo.

“Sehemu nyingi za Jiji la Dar es Salaam zitaathirika na katizo hili la umeme. Umeme utazimwa kwa sababu za kiusalama ili kuruhusu kazi hii kufanyika,” alisema Badra.

Baadhi ya maeneo yatakayoathirika na katizo hilo la umeme ni TBS, Ubungo Bus Terminal, Ubungo NHC, Ubungo Filling Station, Tanesco Staff Quarters, nyumba za wafanyakazi wa Wizara ya Miundombinu, TTCL Flats, Sinza Ukuta wa Posta, NBC Ubungo, Chibuku, Ubungo Portland Cement, Ubungo Flats, Urafiki Flats, Kituo cha Polisi Urafiki, Rombo Green View Hotel, Legho Hotel, Sinza Mugabe, Sinza Madukani, Rubada, UDSM Hostel na Millenium Business.

Mengine ni Ubungo Maziwa, Ubungo Kisiwani, Ubungo Container Terminal, Kiwanda cha Maziwa, TTCL Exchange, Chuo cha Usafirishaji (NIT), UFI, Ubungo Spinning, Mabibo Sahara, W-Bar, TGNP, Ubungo Kibo (Hunters Club) Msewe Uwanjani, Msewe Shuleni, Msewe Golani, Changanyikeni, Chuo cha Takwimu, Changanyikeni Kijijini, Changanyikeni Jeshini, Makongo Juu KKKT, Makongo Juu Kanisa Katoliki, Goba Kunguru, Wazo na Madale.

Kwa mujibu wa Badra, kazi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha Makumbusho na kwamba, kukamilisha kwa kituo hicho, kutasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika katika Jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment