Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, May 29, 2010

ZUMA LAIVUPicha za rais wa Afrika Kusini mwenye ndoa tano mpaka sasa, Jacob Zuma, zinazomuonesha ‘akidendeka’ na mtalaka wa rais Mstaafu, Mzee Nelson Mandela, Winnie Mandela, zimesambaa katika mitandao mbalimbali, Ijumaa limegundua.
Winnie na Zuma walinaswa na mapaparazi wakiwa wamekumbatiana huku midomo yao ikiwa imegusana kitendo kilichotafsiriwa kwamba, walikuwa ‘wakidendeka’.

Tukio hilo la ajabu kwa baadhi ya mila, desturi na tamaduni za Kiafrika, lilijiri wakati wa sherehe za kumpongeza ‘mnene’ huyo wa nchi kuingia madarakani miaka miwili iliyopita.
Licha ya picha hizo kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali bila kuwahusisha wawili hao na mdudu wa mapenzi, wachangiaji wengi wa maoni wamekuwa wakitatizwa na denda hilo.“Nothing to hide” (hakuna cha kuficha) alisema mchangiaji mmoja alipotoa maoni yake katika moja ya mtandao ulioweka picha hizo.
“Kifupi picha hizi ni za kimahaba zaidi na kwa maadili ya kiongozi wa kiafrika si nzuri, inawezekana kwao kufanya vile si vibaya, lakini kwetu na nchi nyingi za kiafrika zinaashiria kitu kibaya,” alisema mmoja wa wasomaji wa mitandao.

Habari zaidi zinasema kwamba, wakati wa kampeni za kuwania uongozi wa nchi hiyo, Winnie, mwanamke mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini humo, alikuwa kambi ya Chama cha African National Congress (ANC) ambayo ilimuweka Zuma kuwa mgombea urais.
Rais Zuma amewahi kulaumiwa na baadhi ya watu wa nchi yake kutokana na tabia yake ya kupenda mahaba hasa baada ya ile skendo mbaya ya kudaiwa ‘kujirusha’ na mdada mmoja ambaye anatajwa kuwa ana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.Mara baada ya kuisawazisha skendo hiyo kisheria, Zuma alijikuta akitengeneza vichwa vingi vya habari pale alipofunga ndoa na kimwana mmoja, hivyo kuongeza idadi ya wake alionao, kutoka wanne hadi watano, licha ya mmoja kufa kwa kujinyonga na mwingine kutengana naye.
Hata hivyo, licha ya kiongozi huyo mwenye makeke mengi kuwa na wake wengi, bado ni kipenzi cha raia wake ambao wengi wanachukulia ndoa hizo kuwa ni kitu cha kawaida kikisimamiwa na mwongozo wa utamaduni wa kabila lake.
Hivi karibuni, kiongozi huyo wa taifa kubwa barani Afrika alikwenda kwenye kituo kimoja cha afya na kupima ‘ngoma’ lakini majibu yalitoka ‘HANA’ hali iliyomfurahisha sana ambapo hakusita kuonesha furaha yake.

Kwa upande wake, Mama Winnie Mandela naye aliwahi kupata skendo ya kudaiwa kutembea na kijana mmoja wakati mumewe (wakati huo) Mzee Nelson Madiba Mandela akiwa jela.
Kashfa hiyo ndiyo ilisababisha aachike na kiongozi huyo mstaafu mara baada ya mambo kuwa hadharani.

No comments:

Post a Comment