Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, May 11, 2010

Rage aanza kazi kwa kishindo!!!


MWENYEKITI mpya wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amesikitishwa na uduni wa jengo la klabu hiyo kukosa umeme kwa muda mrefu baada ya kukatwa kwa deni la sh mil. 3.7, licha ya klabu hiyo kuingiza zaidi ya sh bil. 5 ndani ya miaka 15!

Rage aliyechaguliwa juzi usiku kwa kura 785 akimbwaga Othman Hassan Hassanoo, aliyasema hayo jana katika ofisi za makao makuu ya klabu hiyo baada ya kiongozi huyo kufanya ziara na kuahidi kuweka mambo sawa mara moja kuanzia jana.

Rage aliyewahi kuwa mchezaji wa Simba kabla ya kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na Shirikisho la Soka Tanzania(TFF wakati huo FAT), alisema dosari hizo zitashughulikiwa ili majengo hayo yafanane na hadhi ya klabu hiyo.

Mbali ya kuboresha makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Mtaa wa Msimbazi, Rage alisema uongozi wake utatafuta eneo jingine kwa ajili ya kujenga ofisi za muda ili majengo ya makao makuu yatumike kibiashara zaidi.

Kwa lengo la kudumisha umoja na mshikamano ambao ni moja ya nyenzo ya mafanikio, jana mchana Rage alipanga kukutana na kundi la ‘Friends of Simba’ katika chakula cha mchana huku akimwalika mwenyekiti aliyemaliza muda wake juzi, Hassan Dalali na Mwina Kaduguda.

Baada ya kikao hicho na Friends of Simba, baadaye jioni Rage alipanga kukutana na viongozi wenzake wa kamati ya utendaji na viongozi wa matawi yote ya klabu hiyo, yote hiyo ni kujitambulisha na kuanza kuweka mambo sawa.

No comments:

Post a Comment