Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, May 19, 2010

Zimamoto yakana kugeuza gari lao Daladala!


Siku chache baada ya kuelezwa kuwa kiskosi cha zimamoto mkoani Arusha....kimekuwa kikitumia gari lake la kuzimia moto kama daladala kusanyia abiria badala ya kufanya kazi ya uokoaji

Mkuu kikosi hicho, Luhwa Rashidi, amekana vibaya tuhuma hizo zilizotolewa na kudai kuwa hazina ukweli wowote na kwamba waliozitoa hawakuzifanyia uchunguzi wowote.

Luhwa alisema haijawahi kutokea hata mara moja gari la zimamoto kutumika kwa kazi tofauti na ya uokoaji, kwani hakuna mtu atakeyeweza kukodisha gari la zimamoto kutumika kama teksi.

“Ni jambo la kushangaza kuona mtu anaweza kutoa taarifa kuwa gari kubwa kama la zimamoto linafanywa teksi ikiwa kuna magari ya kisasa ambayo yanafanya kazi hiyo. Naomba ieleweke kuwa kauli hiyo si ya kweli ni ya uchonganishi,” alisema Luhwa.

Aidha, taarifa ya jeshi hilo inaeleza kuwa mkurugenzi wa manispaa hiyo hajawahi kumwita wala kumweka kiti moto mkuu wa Zimamoto kwa madai ya matumizi mabaya ya vifaa vya ofisi.

No comments:

Post a Comment