Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Friday, May 7, 2010

‘Majambazi’ wawili wauawa na polisi

POLISI mkoani Kigoma imewaua kwa kuwapiga risasi watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi katika majibizano ya risasi baada ya kuwakuta watuhumiwa hao wamejificha shimoni.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kuvamia nyumba moja ya mkazi wa kijiji cha Mganza, katika Tarafa ya Nguruka, Kigoma vijijini mwanzoni mwa wiki hii.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kigoma, Damian Bukoke alisema wamekamata bunduki moja aina ya SMG iliyokuwa na risasi 53 .

Bukoke alisema kuwa awali majambazi hao walivamia nyumba ya Cheka Jumanne saa 7 usiku kwa kutumia jiwe maarufu kama fatuma na kuiba simu mbili aina ya Nokia na kamera moja ambavyo thamani yake haijajulika.

Baada ya kupora, inadaiwa walifyatua risasi tano hewani kuwatisha watu wengine wasiwafuatilie.

Polisi walifuatilia baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi na hatimaye kuwakuta wamejificha katika shimo.

No comments:

Post a Comment