Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, May 4, 2010

Ujio wa Viongozi Dar!!!Hii ndio hali halisi ya Jiji la Dar,hapa wageni bado hawajafika je wakifika si ndio balaaa..tutapita wapi jamani na hizi barabar kufungwa?Picha hii kwa Hisani ya Issa Michuzi.

*Foleni zaongezeka mara mbili

*Vibaka watiwa mbaroni

*Wananchi waponda kufanyika Dar

Na Mwandishi wetu,

UJIO wa Viongozi wa nchi mbalimbali kuhudhuria mkutano mkubwa wa uchumi kwa Bara la Afrika, unaotalajiwa kufanyika leo umepelekea kero kubwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na majirani zake,pamoja na kusababisha vibaka na wazururaji kutiwa vizuizini.

Hali hiyo ilianza jana kuanzia majira ya alfajiri mapema katika maeneo kadhaa ya jiji, likiwemo swala daladala kukatisha ruti, huku baadhi ya wakazi hao wakitembea kwa mwendo wa miguu umbali mrefu kwenda katika shughuli zao za kila siku.

Baadhi ya maeneo hayo ya wakazi hao waliozipata ni pamoja na wakazi w3aliokuwa wakitoka nje ya mji ikiwemo maeneo ya Kibamba-Mbezi na maeneo yake ya jirani huku maeneo mengine ni yale ya Boko-Tegeta ambapo abiria walikaa kwa muda mrefu ndani ya magari yao kutokana na foleni kubwa.

Abiria hao katika vyanzo mbalimbali vya habari walikuwa wakilalamikia foleni hizo, kufuatia wao kuamka mapema ilikuepuka adha hiyo lakini matokeo yake muda huo wameweza kukumbana na hali hiyo mara mbili na ile ya kila siku, hali iliyowasababisha kukaa muda mrefu kufika Mwenge, kilisikika chanzo cha abiria aliyekuwa akitokea Tegeta kwenda Posta.

Mbali na kero hiyo ya foleni kubwa katika barabara ya Bagamoyo na maeneo yanayoizunguka, hali kama hiyo pia imewakumba wakazi wa wanaotumia barabara ya Morogoro wakiwemo waliokuwa wakitiokea maeneo ya Kihbaha,Kibamba na Mbezi ambapo walitumia muda mrefu hadi kufiakia maeneo ya Ubungo.

Mwandishi wetu ambaye alikuwa katika maeneo mbalimbali ya jiji alishuhudia msururu mkubwa wa wananchi ukitembea kwa miguu katika barabara za Morogoro, Bagamoyo, Kawawa na Ally Hassan Mwinyi kuekekea katikatii ya jiji.

Licha adha hiyo ya usafiri na foleni ya muda mrefu,MO BLOG, ilishuhudia vikosi mbalimbali vya jeshi la Polisi vikipita kila kona hususani katika Hoteli walizofikia wageni hao na kuimarisha ulinzi.

Sambamba na hilo , baadhi ya wapiga debe,vibaka pamoja na waosha magari nje ya Hoteli walizofikia wageni hao,MO BLOG, ilishuhidia wakikamtwa na kuhojiwa huku wengine wakifungishwa mashati na kuondoka nao.

Mbali na kukamatwa kwa vibaka hao, pia baadhi ya makachero mbalimbali wamemwagwa katika maeneo yote ya jiji kwa kuimarisha ulinzi.

Katika mkutano huo, ambao viongozi na wakuu wa nchi 11 utakuwa sambamba na watu 959 kutoka nchi 85 Duniani.

…….Maoni

Baadhi ya wakazi wa jiji wametoa maini yao tofauti juu ya ujio huo wa viongozi hao.

Wakizungumza na MO BLOG kwa nyakati tofauti walidai kuwa,licha ya Tanzania kupata nafasi ya pekee kwa mkutanoo huo kufanyika nchi, bado Serikali na idara zake hazijajipanga kutekeleza mambo yake.

“Utafanyika mkutano huo na utakapoisha kila kitu kitaishia katika makaratasi huku viongozi wakibakia kujisifia bila matekelezo” alisema Mkazi wa jiji aliyejitambulisha kwa jina la Reuben Kwezera.

Hata hivyo maoni ya wengi ya wakazi wa jiji waliponda juu ya kufanyika mkutano huo katika jiji la Dar es Salaam hususani mipangilio la jiji kuwa mibovu.

:Jiji mpaka sasa halina mipangilio mizuri kwa hali hii ni sawa na kujidhalilisha tu, alisema Joshua Emannuel.

:Kama Serikali ingesoma alama za nyakati ni bora mkutano huu ungefanyika Dodoma ama Arusha, lakini kwa kufanyia Dar huu ni kupeana ulaji tu.

:Miundo mbinu ya jiji bado haijatengamaa, hapo hapo wanaanza kufunga barabara na mambo mengine huku ni kuendelea kujididimiza pasipo kujijua, Serikali inafanya mambo kisiasa kuliko kuangalia ya mbele.

:Mikutano kama hii mara zote inafaanyika Arusha, lakini kufanyika hapa tena katika ukumbi wa ….ni biashara na makubaliano ya vigogo ambao wanaubia na hoteli pamoja na ukumbi waliofikia viongozi hao, kilisema chanzo cha habari ambacho akikutaka kuandikwa na MO BLOG.

Baadhi ya maeneo ambayo Mkuu wa Mkoa alitangaza kuwa wavumilivu ni pamoja na :barabara ya Nyerere kutoka uwanja wa ndege mpaka mjini.

Kwa kuanzia leo, saa moja mpaka saa tatu asubuhi, barabara ya Ali Hassan Mwinyi itatumika kusafirishia wageni kuelekea katika ukumbi wa mikutano, na baadaye saa tisa alasiri hadi moja usiku.

Huku barabara ya Sam Nujoma kutoka Mwenge itakuwa imefungwa. Wageni watakapokwisha itafunguliwa. Saa tisa jioni hadi saa moja.Licha kufungwa huko, pia aliwashahuri wakazi wa maeneo ya Sinza, Kijitonyama, Mwenge na wote wanaotumia barabara hiyo kutumia barabara ya Morogoro.

Vile vile wakazi wa Mbezi, Mikocheni, Kawe na Msasani, wanashauriwa kutumia barabara ya Old Bagamoyo.

“Wananchi wanaokuja kupata huduma katika maduka ya Mlimani City wanashauriwa kutumia barabara ya chuo kikuu Ardhi, kwa kuwa barabara ya Sam Nujoma itakuwa ikitumika kwa shughuli za mkutano huo,” alinukuliwa Lukuvi hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment