Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, May 6, 2010

RAIS WA NIGERIA AFARIKI DUNIA


Rais wa Nigeria, Umaru Yar’Adua(pichani) amefariki dunia. Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari likiwemo Shirika La Habari la Uingereza(BBC), Rais Yar’Adua amefariki dunia leo hii huko katika mji wa Abuja ambao ndio mjii wa Nigeria. Alikuwa na umri wa miaka 58.

Rais Yar’Adua amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu hali iliyopelekea aliyekuwa makamu wake, Goodluck Jonathan kukabidhiwa madaraka na Bunge la nchi hiyo ili kunusuru mgogoro mkubwa wa kisiasa uliokuwa unanukia katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi yenye watu wengi kupita zote barani Afrika. Nigeria ina jumla ya watu wanaokadiriwa kufikia milioni 150.

Rais huyo ambaye aliingia madarakani mwaka 2007 ndiye Rais pekee wa nchi hiyo ambaye aliweka wazi mali alizonazo pindi alipoingia madarakani ikiwa ni ishara ya uadilifu na upingaji wa ufisadi.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.Amin.

No comments:

Post a Comment