Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Tuesday, May 25, 2010

Jamani Kikwete na Ridhiwani Wasihusishwe na Kujiuzulu kwangu!


Pichani ni katibu mkuu wa UVCCM Taifa Bw.Martine Shigella (kulia) katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa akizungumzia kuhusu sakata la kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Hamad Yusuph Masauni , kulia kwake ni katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi Taifa Estar Bulaya.BAADA ya sakata la kujiuzulu kwa aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UV-CCM) Hamad Yusuph Masauni kuzidi kuchukua sura mpya na baadhi ya makundi ya vijana kumhusisha mtoto wa mwenyekiti wa CCM Taifa Ridhiwan Kikwete na mwenyekiti mwenyewe kuwa wanahusika katika kumwondoa Masauni katika nafasi hiyo ,utata zaidi umezidi kuibuka katika sakata hilo baada ya katibu mkuu wa UV-CCM Taifa Martine Shigella kwa mara ya kwanza kujitokeza mbele vyombo vya habari kutolea ufafanuzi juu ya mwenendo mzima wa sakata hilo na kudai kuwa Rais Kikwete na Ridhiwani wasihusishwe katika sakata hilo ambalo mhusika mkuu ni yeye mwenyewe Masauni na si mtu mwingine.

Asema mkakati wa UV-CCM ni kukiomba chama cha mapinduzi kumpitisha Rais Kikwete kuwa mgombea pekee katika uchaguzi mkuu na wanaomhusisha yeye na mtoto wake Ridhiwani na tuhuma za kumwondoa Masauni ni vizuri wakapeleka ushahidi kwake ili kuwajibishwa vinginevyo hawatamwajibisha kwa maneno ya mitaani.

“…Hatuwezi kumwondoa Ridhiwani kwa tetesi za mitaani na kama yupo mtu mwenye ushahidi wa tuhuma zake kuuvuruga umoja huo apeleke kwake ili hatua zichukuliwe ila vinginevyo itakuwa ngumu kumwajibisha”

Pia katibu huyo amesema kuwa pamoja na kuwepo na watu wanaohusisha sakata hilo na mbio za uchaguzi mkuu huko Zanzibar ni kutomtendea haki kwani hata katika maelezo yake na yale ya mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Kikwete hajapata kuzungumzia hilo.

Alisema kuwa yapo maneno kuwa tuhuma za Masauni zimetoka Zanzibar ambako kuna mwanamke ambaye mume wake anataka kugombea nafasi ya juu ya uongozi huko aliondolewa katika nafasi ya uongozi ndani ya UV-CCM kutokana na fitina za Masauni jambo ambalo halina ukweli kwani hakuna kiongozi wa UV-CCM Zanzibar aliyeenguliwa nafasi yake toka Masauni achaguliwe katika nafasi hiyo.

1 comment:

  1. SHIGELA ANAZUNGUMZA ASICHOKIAMINI APO KASHNIKIZWA ATA ESTA ANAONESHA RIZWAN NDIE ANAVURUGA NCHI KWA TAMAA ZAKE ZA PESA NA MADARAKA BT CDM IKICHUKUA NCHI LABDA AKIMBIE KAMA SEIF AL ISLAM

    ReplyDelete