Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Thursday, May 6, 2010

MAJAMBAZI YAKAMATWA NDANI YA TRENI YAKIWA NA SILAHA ZA KIVITA!!!
Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia watu wanne kwa tuhuma ya kupatikana na silaha mbili za kijeshi aina ya SMG zikiwa na risasi 492 kwenye treni ya abiria iliyokuwa ikitokea Mpanda mkoani Rukwa kuelekea Tabora.

Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Kamishna Msaidizi Lebelatus Barrow amewataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Ibrahimu Joseph Mnange maarufu kama Ibra(36), mkazi wa Nyakato mkoani Mwanza na mwanamke pekee Hadija Ibrahim Mtenyi maarufu kwa jina la Bugusi(20) Mkazi wa Nyamongo mkoani Mara.

Kamanda Barrow, amewataja watuhumiwa wengine kuwa ni Nassoro Said Mohamed maafufu kwa jina la Kalega(31) mkazi wa Kijiji cha Kangeme kilichop katika wilaya ya Urambo mkoani Tabora na Jafari Juma Mohamed maarufu kama Malega(50) Mkaziwa Kijiji cha Lingula Tarafa ya Kaliua pia wilayani Urambo mkoani Tabora.

Kamanda huyo amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa juzi majira ya saa 5.00 asubuhi na askari waliokuwa wakisindikiza treni hiyo baada ya kuishitukia mizigo waliyoibeba wakati wa safari yao ambapo baada ya kupekuliwa mizigo yao walikuwa wakiwa na silaha hizo moja ikiwa na namba 1966-AFU -3404 na nyingine ikiwa na namba2571 pamoja na Magazine tatu ambapo mbili kati ya kizo kila moja ikiwa imesheheni risasi 30 kila Moja.

No comments:

Post a Comment