Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, May 19, 2010

Tanzania yanyakua tuzo ya kimataifa ya Utalii!


BODI ya Utalii Tanzania TTB leo imeonyesha kwa waandishi wa habari TUZO waliyopata siku za hivi karibuni wakati wa maonyesho ya Utalii yaliofanyika mjini Durban, nchini Afrika Kusini kuanzia tarehe 8 hadi 11 Mei 2010. Maonyesho haya yanajulikana “INDABA, Travel Show” na yanafanyika kila mwaka nchini Afrika Kusini.Maonyesho ya INDABA ni kati ya maonesho makubwa matatu ya utalii duniani, maonyesho mengine ni World Travel Market (WTM) yanayofanyika nchini Uingereza na ITB yanayofanyika nchini Ujerumani. Kwa miaka miwili mfululizo Maonyesho yameelezwa kama ndio maonyesho bora barani Africa

Tanzania ilishiriki kikamilifu kwenye maonyesho haya na Taasisi za Serikali nne ziliweza kushiriki ambazo Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Hifadhi za Taifa TANAPA, Mamlaka ya Bonde la Ngorongoro (NCAA) na Kamisheni ya Utalii Zanzibar.(ZCT)

Pamoja na taasisi za serikali, pia kulikuwa na kampuni binafsi 52 ambazo kati ya hizo 22 zilikuwa ni za kuongoza watalii (Tour Operators), 27 kutoka sekta ya hoteli, na kampuni 3 za ndege ziliweza kuwakilishwa.

Kama yalivyokuwa mashindano mengine, Tuzo hii linatolewa kila mwaka na nchi zote za 14 za SADC zinazoshindanishwa. Kwa mwaka huu TANZANIA ndio iliyoibuka kidedea na kutapa Tuzo ya kwanza “Platinum Award” na kuwashinda nchi zote nyingine za SADC pamoja na nchi ya jirani (Kenya). Kigezo kilichoshindanishwa ni pamoja na ubora wa banda, ushiriki wa sekta binafsi kwa maana bidhaa zilizokuwa zinauzwa, pamoja kauli mbiu yetu tuliyotumia mwaka huu ambayo ni “Experience the Real Game in Africa na nyingine “Celebrate FIFA world cup in Tanzania” WELCOME TO TANZANIA”, (“Karibu Afrika kwa Kombe la Dunia, Tembelea Tanzania Ujionee Vivutio vya Utalii”).

No comments:

Post a Comment