Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Saturday, May 15, 2010

WANAFUNZI GREEN ACRES WAFANYA VURUGU, WATIMULIWAWanafunzi kadhaa waliokuwa nje ya shule baada ya kutimuliwa.

WANAFUNZI wote wa Shule ya Sekondari ya Green Acres ya Mbezi Africana jijini Dar es Salaam wametimuliwa shuleni hapo leo, na shule hiyo kufungwa mpaka Jumanne wiki ijayo kufuatia wanafunzi hao kuzusha vurugu za kupinga mwalimu wao Mkuu, Ntipool Yesambi, kuondolewa shuleni hapo kufuatia matokeo mabaya ya mitihani.

Wanafunzi hao wanatakiwa kufika shuleni hapo na wazazi wao siku ya Jumanne na kulipa sh. 100,000 kila mwanafunzi kama fidia kwa uharibifu uliotokana na vurugu hizo.Mkurugenzi wa shule hiyo, Julian Bujugo, akiongea na wanahabari wetu kuhusu tukio hilo.Mwalimu Ntipool Yesambi akiongea na wanahabari (hawapo pichani).Sehemu ya mali zilizoharibiwa.Baadhi ya walimu wakiwa eneo la shuleni hapo baada ya shule kufungwa.Geti la shule likiwa limefungwa na kubaki mlinzi baada ya wanafunzi wote kutimuliwa.

1 comment:

  1. kha....laki moja??Bujugo jmn...anaona laki bei ndogo eeh?

    ReplyDelete