Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, May 23, 2010

Mrisho Ngassa na Jackson Njovu rasmi ndani ya Azam FC!!



Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa wachezaji hao wapya Mwenekiti wa Azam Fc, Said Muhammad Said alisema kuwa baada ya kuwapata wachezaji hao lengo la klabu hiyo ambalo ni kuchukua Ubingwa wa ligi Kuu ya Vodacom katika msimu ujao.alisema “Wachezaji wazuri tunao hatuna sababu ya kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2010-2011″.


Nae mchezaji mpya wa timu hiyo,Mrisho Ngasa ambaye amehamishwa kwa kitita cha sh milioni 58, alisema “Nitahakikisha timu yangu mpya inafanya vizuri katika msimu ujao wa ligi kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu,Najua kuna kila aina ya ushindani huko niendako lakini nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha kiwango changu hakishuki na kuipatia Ubingwa wa Ligi Luu ya msimu ujao timu yangu mpya”. aliongeza Ngasa.


Naye golikipa mpya wa timu hiyo aliyehamishwa kwa kitita cha shilingi milioni tatu kutoka JKT Ruvu, Jackson Chove alisema kuwa,baada ya kukosa kusajiliwa na timu hiyo katika msimu uliopita sasa amefika katika timu ambayo alikuwa anaipenda kutokana na kuwa na mapenzi na klabu hiyo tajiri hapa Tanzania. “Najua kama kuna ushindani mkubwa katika timu yetu lakini nitahakikisha nafanya mazoezi na kuongeza juhudi zaidi ili kiwango changu kisishuke” alisema Chove.

No comments:

Post a Comment