Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Sunday, May 30, 2010

Hausiboi aua watoto wa bosi kwa sumu!


Vilio, simanzi na butwaa vimeikumba familia moja na majirani zao wilayani Sengerema baada ya kushuhudia madenti watatu wakikata roho muda mfupi baada ya kula chakula kilichoandaliwa nyumbani kwao kinachosadikiwa kuwa na sumu.

Kwa mujibu wa mashuhuda, sumu hiyo iliwekwa na hausiboi katika nyanya zilizoungiwa mboga ambayo walikula watoto hao ambapo inadaiwa kuwa ilitokana na matajiri wa kijana huyo kutishia kutomlipa mshahara wake.

Imedaiwa kuwa kijana huyo, ambaye ni raia wa Burundi, aliuza nyanya za matajiri hao kwa bei nafuu, hivyo kuwapa hasira matajiri wake ambao waliahidi kutomlipa mshahara wake kisha kumuagiza kuwa aende shambani akachume nyanya kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwa siku hiyo.

Kutokana na hali hiyo, hausiboi huyo alichukia na ndipo alipokwenda dukani kununua sumu hiyo ambayo haijafahamika mara moja na kuiweka kwenye nyanya hizo.kisha kuzichuna kidogo na kuweka sumu hiyo.

Baada ya kumkabidhi hausigeli alizipikia chakula hicho na baada ya kuiva alitaka kula na mtoto mdogo wa miaka minne anayeshinda naye ambapo hausiboi huyo alimuonya kutokula chakula hicho kwa madai kuwa ni maalumu kwa ajili ya matajiri wake.

Kauli hiyo ilimfanya hausigeli yule ahamaki na kuhoji mbona siku nyingine huwa wanakula ndipo hausiboi huyo alipomtakia kuwa kama anataka kufa ale chakula hicho.

Kutokana na kauli hiyo, hausigeli huyo aliacha kula chakula hicho na baada ya saa chache watoto watatu wa mwenye nyumba hiyo walirejea nyumbani wakitoka shule na kuanza kula chakula hicho.

Baada ya muda wa dakika 30 watoto hao walianza kulalamika tumbo huku wakitokwa na jasho jingi. Ingawa walijitokeza wasamaria wema na kuwakimbiza hospitali, walifia njiani kabla hawajapatiwa matibabu.

No comments:

Post a Comment