Psquare Ft. J.Martins- E No Easy

Wednesday, May 19, 2010

Mwanafuzi wa shule ya msingi ajaribu kulipua Ubalozi wa Marekani


Denti wa shule ya msingi anayedaiwa kuhamasishwa na mafunzo aliyopewa na mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda amekiri kutaka kuulipua.

Taarifa kutoka ndani ya ubalozi huo, zimeeleza kuwa kijana huyo ambaye hakufahamika jina lake, amekamatwa, yupo katika kituo cha polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.

Habari zinadai kuwa,mwanafunzi huyo mwenye umri wa kati ya miaka 15 na 17 aliingia ndani ya ubalozi huo Jumapili iliyopita saa tatu usiku, akiwa na vifaa alivyotaka kutumia kufanyia ugaidi huo.

Inadaiwa alikuwa na dumu la lita tano la mafuta ya taa, utambi na kiberiti cha gesi.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari, baada ya kuingia ndani ya ubalozi huo, alikwenda moja kwa moja kwenye tangi linalohifadhi zaidi ya lita 1,000 za dizeli kwa nia ya kulilipua.

Habari zilidai kuwa, kijana huyo alipoingia ndani ya ubalozi huo akipitia geti namba tatu ubalozini hapo, walinzi walikuwa wamelala.

Alipolifikia tangi hilo, kijana huyo anayedaiwa kuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Mtambani wilayani Kinondoni, alijaribu kufungua koki za tangi hilo kwa nguvu na kuwaamsha walinzi hao usingizini.

Walinzi walimkamata na baada ya kumhoji, alikiri kuingia katika ubalozi huo kihalifu akitaka kuulipua, hatua ambayo ingesababisha mshituko mkubwa kama wa asubuhi ya Agosti 7, 1998, ubalozi huo ulipolipuliwa na kuua watu kadhaa wakiwamo Watanzania na Wamarekani.

Kijana huyo alidai kuwa yeye na wenzake wapatao 15 walipatiwa mafunzo kwa njia ya video na mtandao huo, kwa ajili ya maandalizi ya kuulipua ubalozi huo Juni mwaka huu.

Alidai baada ya kuhamasika na mafunzo hayo, yeye na mwenzake aliyekuwa amemwacha katika eneo linalotumika kuuzia maua karibu na ubalozi huo, walikwenda kujaribu kutekeleza mafunzo hayo kwa vitendo.

No comments:

Post a Comment